Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
- Thread starter
-
- #201
Tunataka muonekano angavu sio wavumbivumbi, pia navipind view vya kisasa zaidi
Mimi hicho kipindi chake ndo nimeki miss hicho wakikirudisha nitaanza kuangalia TBCYule Mzee yupo nadhani, vipindi vya aina kama ile nashauri vingeanzishiwa mgawanyo wake,hapa namaanisha kuwe hata na TBC 3 kwaajili ya issues pasua kichwa kama zile.
Ndugu WanaJF,
Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa vipindi na ubunifu.
Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.
Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.
Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.
Karibuni sana.

Kwa haya uliyoeleza yote ni uzembe na lack of seriousness. Hapo wazidishe umakini na u serious.1. Rekebisheni volume (ukubwa wa sauti) za matangazo ya biashara.
Mtu unasikiliza taarifa ya habari kwa sauti ya kawaida, mara linatokea tangazo la tigo, volume iko juuuuuu, tunanza kutafuta remote ili kupunguza sauti. Tangazo likiisha inabidi kupandisha tena.
2. Usomaji wa habari za kimataifa:
Someni kwa vituo. Sio mnasoma kama mnaimba.
Mnashindwa hata kuchomekea maneno ya kuunganisha/kutenganisha habari kiasi kuwa habari ya Uturuki haijaisha vizuri, tayari inakuwa imeunganishwa na habari ya Marekani as if ni taarifa moja.
3. Ukamilifu wa habari.
Kamilisheni taarifa. Sio mnajiunga na mtangazaji aliye nje ya studio anaeleza kidogo na kabla taarifa haijaeleweka vizuri, mnakatisha.
4. Nitarudi kesho nikiwa kwenye computer.
Hao ni sikio la kufaHuu ni ushauri bora kabisa... Plus muonyeshe shughuli za kitaifa ikiwemo BUNGE
Tena yenyewe ndio itakuwa no 1 kwenye hyo list.top10 ya tv mbovu ulimwenguni TBC inavigezo vyote vya kuepo
TBC mpaka iwe mpya sio rahisi.
1. Mwandaaji na aina ya vipindi ni vya kizee mno. Ubunifu ni zero.
2. Mnavaa kama madereva na sio watangazaji. Mnekukula mmenenepeana haswa wanawake ni vipipa. Hao rudisha nyuma kuandaa na kuongoza vipindi. Eleweni kutangaza kwenye tv ni zaidi ya kazi ya PR. Muonekano ndio branding. Get people with best voice and appearence plus brains. WAPO TELE.
3. Hamjaweza tumia teknologia ipasavyo. Quality ya video zenu inasikitisha. TV ya Taifa? No way. Mnashindwaje na madogo kama ayo, itv nk ?
4. Wekeni channels tofauti. Say TBC 1 huko wekeni watu wa serikali na programme za kuisifu serikali. Fine. TBC 2 ya biashara na programme zilizochangamka za vijana, kisasa, nk
TBC 3 say International hii ni ya utalii na kwa kiingereza. Huko unaiuza Tanzania duniani na sera ya viwanda na ipatikane free duniani kote na balozi zetu na airport zote na portal zote kubwa. Weka vivutio, mahoteli, mbuga, na quality ya picha iwe ya kimataifa.
5. Hiyo serikali mtandao ionekane kimataifa. Mambo ya passport, viza, uwekezaji na fursa. Wawepo watu wanaojua lugha na sio kiingereza cha kihaya.[emoji2][emoji1]
Sijajua kwa sasa ila hapo nyuma TBC zilikuwa zimegawanyika, 1,2...maana Kwa Ss tbc hawaelewi wako mlengwa gani, siasa, Habari, makala Au burudani... Kila sehemu wanajaribu jaribu, Kwa maoni yangu tbc 1 ingejikita zaidi kwenye Habari pasipo ubaguzi, mf kama habari za siasa ziwe kote kote isiwe chama fulani tu, sawa haiwezi kuwa 50,50 basi angalau chama pendwa kiwe angalau 60 na vilivyo salia viwe 40,Nimepitia maoni. Nasikitika kwamba bado wengi mmejikita kwenye kulalamika zaidi badala ya kupendekeza angalau program ideas ili kulimaliza tatizo.
Nyuzi za malalamiko zipo nyingi sana na tayari yanafahamika. So nasisitiza tujielekeze zaidi kwenye mapendekezo kuhusu kinachotakiwa kufanywa huku tukitoa ideas ambazo zinaweza kufanyiwa kazi.
TBC ni mali yetu sote. Ni lazima tutoe mawazo yanayojenga ili ifanikiwe.
Naelewa tuko disappointed kwa sababu ya itikadi zetu na jinsi tunavyohisi hakuna fairness, lakini tuweke grudges pembeni na tuelekeze njia sahihi ya kupita.
Tusilalamike tu ili kuponya nafsi zetu. Tutoe constructive ideas ili kuiponya TBC yetu.
Travic unaangukia kwenye mtego ule ule wa kukataa maoni ya wananchi ambayo yapo kinyume na matarajio yako
Kumbuka hapa ni JF wadau wanaongea openly. Na anayekwambia ukweli anakupenda.
Ushauri mkubwa umetolewa katika nyanja kuu kama tatu hivi.
Moja, kuweni fair/impartial. Mnafahamu maana yake. Kama ni TV ya umma na ionekane hivyo. Hilo wamelisema na ndio kubwa sana.
Pili, boresheni ubora wa vipindi pamoja na ubora wa picha. Wadau wametoa mifano tatizo lilipo (aina ya vipindi) na vipi viongezwe. Wengine wamesuggest aina ya quality ya picha. Hadi wengine wamejitolea kuja kuwasaidia upande wa graphics.
Tatu, wadau wameshauri kuwa na channel zaidi ili kuaccommodate mahitaji ya vijana watoto wazee wapenda michezo nk lakini pia muonekano wa kimataifa wa TV yetu! Tunaweza kiwa na channel ta habari tu (TBC news) kisha nyingine ya mambo ya kawaida (documentaries-wildlife, elimu, ziara za tunatekeleza, this week in perspective, shuleni/watoto, science and engineering) halafu TBC Sport/music/emtertainmenr ( mpira wa nje na ndani tafuteni haki za kuonyesha japo mara moja moja, mieleka, muziki kwa sana wa vizazi vyote, bongo/nigerian movies, mambo kama hivyo kwa mpangilio maalumu).
Kutekeleza hayo ni dhahiri mnahitaji revamp ya hali ya juu, kuanzia staff training/upgrading, vifaaa, ubunifu nk.
Hamu yangu ni kuona kuwa mtanzania anaweza kuyapata haya yote in one package yaani TV station ya taifa ambayo kwa uchungu analipa kodi kuiwezesha. Lakini pia mtaweza kujiendesha na hata kutoa dividend kwa serikali kama mtatekeleza ushauri wa wadau humu.
Nawatakia utekelezaji mwema.
1. Rekebisheni volume (ukubwa wa sauti) za matangazo ya biashara.
Mtu unasikiliza taarifa ya habari kwa sauti ya kawaida, mara linatokea tangazo la tigo, volume iko juuuuuu, tunanza kutafuta remote ili kupunguza sauti. Tangazo likiisha inabidi kupandisha tena.
2. Usomaji wa habari za kimataifa:
Someni kwa vituo. Sio mnasoma kama mnaimba.
Mnashindwa hata kuchomekea maneno ya kuunganisha/kutenganisha habari kiasi kuwa habari ya Uturuki haijaisha vizuri, tayari inakuwa imeunganishwa na habari ya Marekani as if ni taarifa moja.
3. Ukamilifu wa habari.
Kamilisheni taarifa. Sio mnajiunga na mtangazaji aliye nje ya studio anaeleza kidogo na kabla taarifa haijaeleweka vizuri, mnakatisha.
4. Nitarudi kesho nikiwa kwenye computer.
Nilihama huko maana taarifa za habari hamnaPia ulijitahidi sana mm nilitazama kule alipo tido mhando yani kupitia azam two