Majani sio yale yale yameongezwa mara dufu,kama hujui uliza kule kwa mpwa wa mzee wanavyochotewaga bila idadi.Kule ni kujumlisha tu hakuna kutoa.Mimi sijuagi siku nyingi huko kwenye kioo picha ikoje maana funguo nilitupa chooni choo cha tundu kwa hasira siku nyingi.Hapo naomba kutofautiana na wewe. Kwa Rais aliepo madarakani swala ni kujenga hoja baada ya kujitathmini. Taasisi kama TBC imezeeka kimuundo na kimfumo. Kwa kutizama tu vipindi vyao unajua jinsi wanavyoplan. In incremental. Ya mwaka ujao ni ya mwaka jana badilisha hapa na pale ...maisha yasonge. TBC inahitaji total overthaul. Unapotafuta mkuu wa taasisi na vitengo unatafuta mtu mwenye vision na uwezo wa kusimamia vision. Nani asieikumbuka National Housing ilivyobadilika baada ya kupata viongozi sahihi? CRDB Je, nk. Taasisi zimekuwa tamu mpaka watu wameanza kupigana vikumbo kwa fitna.
Tubadili mbinu jinsi ya kutafuta CEOs na waachwe watekeleze vision zao. Political interference iwe pia tamed.
Utamlaumu Rais kama kweli anaingilia kazi nzuri. Lakini kama kazi ni mbaya unamtegemea akae kimya?
Tuwasaidie TBC kwa kuwaeleza njia na mbinu sahihi za kupitia watoke hapo walipo maana kweli wana hali mbaya.
Its too sad to see our cash cow being mismanaged.
Ng'ombe huyo alipaswa kutoa lita 20 lakini anayoa lita 5 japo anakula majani yaleyale.
Hapa nataka kushauri.Watanzania tumshauri mzee awabambikize vituo vingine vyote kesi za uhujumu uchumi,kukwepa kulipa kodi akianzia na Azam,Itv,ile kule Mwanza,claud Abood,Upendo nk.Wapelekwe mahakamani,hukumu itoke kwa mzee vifungiwe milele. Hapo labda watapatikana watazaji.Lakini sio mimi.Funguo sina niacheni.