Kuna jambo moja pia ambalo hunikera sana na Televisheni hii. Nalo ni "INTERFACE COLOR" yake. Hivi hamuoni hilo li rangi la BLUE linafubahisha sana uzuri wa uso wa stesheni/chaneli hii?
Kama ni rangi ya bendera ya Taifa, ipo rangi zaidi ya moja. Rangi yenye mvuto na ya kupendeza CHANGANYA NJANO KIDOGO, KIJANI KWA MBAAALI, NA mkanda wa BLUE.
Cha kwanza ifanyeni muonekano wake wa mpangilio wa rangi /Interface ulete mvuto , kisha mpange vipindi vya kuweza kuwafanya watu wawahi kurudi majumbani mwao jioni ili kuwahi vipindi fulani. Siyo mara zote mabango ya CCM tuuuu, na SIFA za kijinga kwa viongozi wa CCM. Ifanyeni TV hii iwe ni ya watu wote bila ubaguzi. Kwa upande wa vipindi vyenye mvuto mbali na kuzungumzia kilimo, sayansi na teknlogia nk, no vema mkaweka vipindi vya watu wote kwa maana ya jinsia zote, ngazi zote, na watoto wa Umri wa kujitambua. Vipindi hivyo ni vile vinavyomuondoa mtu katika uchovu wa siku nzima wa kazi na mahangaiko mengine. Mind relaxing programs. Wekeni Maigizo yenye mvuto yasiyo ya kiitikadi yenye kufurahisha,kuelimisha,kuonya,na kuburudisha. Maigizo na TAMTHILIYA za kiswahili zinazoenda na wakati, . Pia tamthiliya za kimataifa nazo huwa zinavuta watu wengi kuipenda Televisheni. Msiwe WAJIMA sana ,enzi zimewapita sana, hii karne ni lazima kwenda nayo kwa kasi ya ushindani na uthubutu. Kuanzia usiku wa saa nne wekeni TAMTHILIYA ZA KIMATAIFA,/INTERNATIONAL, mfano TELENOVELA huko MEXICO, PHILIPPINES, ITALIA,COLOMBIA,nk. Mida ya jioni saa kumi na mbili hadi muda wa taarifa ya habari ya saa mbili wekeni Maigizo au na TAMTHILIYA za Kiswahili, ziwe zimechezwa na wasanii wetu, zinazokwenda na wakati. Baada ya habari ya saa mbili yaani saa tatu usiku UCHAMBUZI WA MICHEZO KWA KINA NA KWA WELEDI.
Panga siku za vipindi vya Sayansi na teknolojia, siku za vipindi vya shughuli za serikali, na siku za kumbukumbu na historia ya mambo yote yahusuyo Taifa letu, watu wake, Uongozi, Mali asili na madini nk nk.
Mkiona haya hayawezekani basi mjue kazi imewashinda.
Nitafuteni mnipe kazi . Nina idea nyingi tu za kuifanya Televisheni hii iwe namba moja AFRICA Mashariki. Inawezekana , ni suala la kuamua tu kubadilika. Baaasiiii.
Sent using
Jamii Forums mobile app