TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

TBC MPYA: Ushauri, Maoni na Mapendekezo ya ubora wa vipindi (Television Content)

Yaani mnaona heri kumuonesha mkuu wa mkoa live, Rais live, ujio wa ndege Live, lakini kila kitu mkiweke gizani. Mnaona raha hasa kutuonesha wanyama wa porini lakini. Timu za Taifa zikicheza ni gizani, saa hizi kuna hadi michuano ya timu ya Taifa wanawake, lakini kuiona hadi utafute Azam au ZBC, timu ya Taifa inacheza leo pia, hamjawahi kuthubutu hata kidogo kujua kwamba kuna watanzania zaidi ya milioni hamsini wanataka kuiona timu yao hata bure kupitia TBC ikicheza.

Hivi nyie mnakwama wapi, ni kipi kipau mbele chenu kwa umma huu wa watanzania? Makonda akiongea mnakuwa live (siyo kwa nia mbaya nalisema hili), bombardier zikija tena mnawahi vibaya mno, teuzi na watu wakiapishwa mko live, sasa basi kwa nini timu zetu za taifa zikicheza msione umuhimu wa kurusha hizi mechi? Zanzibar inaweza kurusha hizi mechi, kwa budget ipi ambayo nyie hamna? Muda wote mnaweka mavipindi ya ajabu ajabu ya marudio rudio tu, hivi mnakwama wapi?
Sio Tv ya kuangalia kama una timamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni kutumika kisiasa! Tunashindwa kuwelewa kama nyie ni Television ya Taifa au tawi la chama?
Ubora wa picha ni sifuri kabisa!
Nchi hii imejaa vijana zaidi ya 70% nyie asilimia 80 ya vipindi vyenu ni vya kizee!
Mnashindwa hata kuonesha mechi ya Taifa stars mmekalia ziara za viongozi wa chama wakitembelea matawi sijui kigoma gani huko!
Mmetangaza kufunga mitambo mipya ya kisasa na picha ndo kabisa zimerudi zile za kiwango cha chini kabisa!
Subirini na wengine wanakuja na mjiandae kwa POVU ZAIDI
haya ndio maoni yangu.
 
TBC kazi Yao ni kusifu na kusujudu muda wote hawaangali mapungufu mashuleni hospital mawasiliano vijijini nishati wao hawaangali hayo kabisa wako wanaunga juhudi za mkuu wa wanyonge mtu mwenye Akili timamu hawezi kukaa anafatilia uo ujinga wao
 
TBC katika
Matangazo yenu mnajinadi kuweka mitambo Namanga na Rombo. Nimebahatika kufika Rombo mwishon mwa mwaka jana sijayasikia matangazo yenu. Nimefika tarakea nkaisikia kwa mbali TBC FM na taifa kusogea hadi Tarafa ya usseri usikivu unakomea hapo. Nkajiuliza tambo zote za nini? Iweje radio za Kenya ziwe na usikivu mzuri kutoka Nairobi hadi Rombo lakin mtambo wenu uwe na usikuvu wa km 10 tu?? Kila kitu fake?? Radio moja tu ya Tanzania inayosikika vizuri Rombo Ni Radio Maria 107.10FM na kwa mbali radio safina na sauti ya injili. TBC mnakwama
Wapi kujiboresha?? Acheni tambo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
TBC katika
Matangazo yenu mnajinadi kuweka mitambo Namanga na Rombo. Nimebahatika kufika Rombo mwishon mwa mwaka jana sijayasikia matangazo yenu. Nimefika tarakea nkaisikia kwa mbali TBC FM na taifa kusogea hadi Tarafa ya usseri usikivu unakomea hapo. Nkajiuliza tambo zote za nini? Iweje radio za Kenya ziwe na usikivu mzuri kutoka Nairobi hadi Rombo lakin mtambo wenu uwe na usikuvu wa km 10 tu?? Kila kitu fake?? Radio moja tu ya Tanzania inayosikika vizuri Rombo Ni Radio Maria 107.10FM na kwa mbali radio safina na sauti ya injili. TBC mnakwama
Wapi kujiboresha?? Acheni tambo


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu,radio zenye mitambo yenye nguvu bongo ni radio maria,radio one(zote za ipp)radio free Africa,iliupate usikivu hewani mtambo uwe vzr sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu WanaJF,

Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa picha na ubunifu wa vipindi.

Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.

Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.

Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.

Karibuni sana.
1. Siipendi TBC kabisa kwa sababu ni chombo cha propaganda cha CCM
2. Sina tatizo na CCM ila nina tatizo na TBC jinsi inavyotumika vibaya.
3. angalau kwa sasa naweza angalia madam Rita jumapili pekee, japo kipindi cha tarehe 19/Jan 2020, nilimsikia akisema atapenda kukutana, na kiongozi moja wa CCM. Huku kujikomba kwa CCM nitaacha kuangalia kipindi chake.
4. Kujikomba kwa CCM kunaficha mengi, kwa sababu chama kilichoongoza tangu 1961 kwanini watu wanapenda kukibeba beba? Hivi CCM haiwezi simama yenyewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jambo moja pia ambalo hunikera sana na Televisheni hii. Nalo ni "INTERFACE COLOR" yake. Hivi hamuoni hilo li rangi la BLUE linafubahisha sana uzuri wa uso wa stesheni/chaneli hii?
Kama ni rangi ya bendera ya Taifa, ipo rangi zaidi ya moja. Rangi yenye mvuto na ya kupendeza CHANGANYA NJANO KIDOGO, KIJANI KWA MBAAALI, NA mkanda wa BLUE.
Cha kwanza ifanyeni muonekano wake wa mpangilio wa rangi /Interface ulete mvuto , kisha mpange vipindi vya kuweza kuwafanya watu wawahi kurudi majumbani mwao jioni ili kuwahi vipindi fulani. Siyo mara zote mabango ya CCM tuuuu, na SIFA za kijinga kwa viongozi wa CCM. Ifanyeni TV hii iwe ni ya watu wote bila ubaguzi. Kwa upande wa vipindi vyenye mvuto mbali na kuzungumzia kilimo, sayansi na teknlogia nk, no vema mkaweka vipindi vya watu wote kwa maana ya jinsia zote, ngazi zote, na watoto wa Umri wa kujitambua. Vipindi hivyo ni vile vinavyomuondoa mtu katika uchovu wa siku nzima wa kazi na mahangaiko mengine. Mind relaxing programs. Wekeni Maigizo yenye mvuto yasiyo ya kiitikadi yenye kufurahisha,kuelimisha,kuonya,na kuburudisha. Maigizo na TAMTHILIYA za kiswahili zinazoenda na wakati, . Pia tamthiliya za kimataifa nazo huwa zinavuta watu wengi kuipenda Televisheni. Msiwe WAJIMA sana ,enzi zimewapita sana, hii karne ni lazima kwenda nayo kwa kasi ya ushindani na uthubutu. Kuanzia usiku wa saa nne wekeni TAMTHILIYA ZA KIMATAIFA,/INTERNATIONAL, mfano TELENOVELA huko MEXICO, PHILIPPINES, ITALIA,COLOMBIA,nk. Mida ya jioni saa kumi na mbili hadi muda wa taarifa ya habari ya saa mbili wekeni Maigizo au na TAMTHILIYA za Kiswahili, ziwe zimechezwa na wasanii wetu, zinazokwenda na wakati. Baada ya habari ya saa mbili yaani saa tatu usiku UCHAMBUZI WA MICHEZO KWA KINA NA KWA WELEDI.
Panga siku za vipindi vya Sayansi na teknolojia, siku za vipindi vya shughuli za serikali, na siku za kumbukumbu na historia ya mambo yote yahusuyo Taifa letu, watu wake, Uongozi, Mali asili na madini nk nk.
Mkiona haya hayawezekani basi mjue kazi imewashinda.
Nitafuteni mnipe kazi . Nina idea nyingi tu za kuifanya Televisheni hii iwe namba moja AFRICA Mashariki. Inawezekana , ni suala la kuamua tu kubadilika. Baaasiiii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo hii wakati Rais wetu alipokuwa akizindua katakana kuu ya JWTZ' pale Lugalo, matangazo yenu yalikuwa yakikatika mara kwa mara. Kutoka hapo TBC makao makuu mpaka ilipo karakana hiyo sidhani kama zinazidi mita 5000 au kilometa 5.Mnashindwaje kutuletea matangazo bora yasiyokatika katika kama ilivyo kuwa leo. Hii ni aibu kwa taasisi yenu na Taifa zima.
 
Mimi ni mpenzi wa kipindi cha tunatekeleza napenda kufuatilia maendeleo ya taifa letu. Lakini kwa muda mrefu sasa nimegundua wanaohojiwa wengi ni wateule wa mheshimiwa, na wote husifia sana miradi ya maendeleo inavyofanyika na kutoa mifano ya namna wanavyopewa fedha za kutosha.

Ninajiuliza kila siku kwa nini wasihojiwe wananchi wa kawaida wakaongelea miradi iliyojengwa au kuanzishwa inavyowanufaisha? Mara chache nimesikia waliohojiwa wanasema mheshimiwa ni jembe anachapa kazi lakini tunaomba atuletee barabara, atuletee maji, atuletee umeme nk.

Unaelewa nini hapo? Tazama kwa ndani kabisa, ndani kabisa utaelewa mwananchi anamaanisha nini.

Jirekebisheni TBC
 
Naomba kutumia fursa hii kukuomba mkuu wa vipindi na maudhui TBC uongeze muda wa kipindi cha SAIKOLOJIA maana elimu inayotokewa ni nzuri mno.
Inaponya msongo wa mawazo
Inaponya sonona
Inarekibisha tabia kwa ujumla
Inaokoa maisha ya watu.NK.
 
Bado ninawashauri ongezeni muda kwa kipindi cha saikolojia ya mwanadamu ni kipindi kizuri mno tatizo muda ni mfupi
 
Hivi bado ipo.Mimi niliilock siku nyingi tangu walipomfukuza Tido na kumbambikizia kesi.Baada ya kuilock hiyo channel yao ya kijani ambayo hata kiongozi akienda kujisaidia alimradi amevaa shati la kijani wanatangaza nilitupa funguo chooni.Choo cha nje cha tundu moja.RIP TBC.
 
Jf wengi ni wadau wa kile chama hivyo comment za kuvunja moyo puuza.
1. Mimi kuanzia kimuonekano, rangi zenu sio nzuri. Yaani hata nikiiangalia tbc ktk king'amuzi cha dstv bado muonekano haivutii.
2. Jaribuni kuvuta watu kwa kuonyesha vipindi vya michezo hasa mpira wa miguu na mieleka. Ikiwezekana wwe tena sio mechi za zamani na pia ligi tofauti kama za Tz, uk, spain, italy etc.
3. Habari kwa upande wa watangazaji wanaume mmajitahidi, wanaume wamechangamka wanapotangaza habari. Wanawake wengi wamezubaa maana unakuta mtangazaji mwanaume anajaribu kumu-engage mtangazaji mwanamke kwenye mazungumzo ya kuchangamsha habari ila unakuta mwitikio ni mbovu. Wamezubaa wengi.
3. Kingine nafikiri kinawaangusha ila hamna namna ya kukizuia ni KUAJIRI vyeti badala ya vipaji. Ni bahati mbaya ila hamna namna. Kuna vijana wana vipaji na ubunifu wa hali ya juu ktk mambo ya journalism ila vyeti ndio 'taizo'.
4. Watengenezaji wenu wa documentaries za hapa kwetu wawe na ubunifu. Documentaries zimezubaa ma kupooza.

Kwa hiyo, Anzeni na muonekano wa tv yenu. Kweli Rangi imepooza sana. Hamna ule uHD.

Nawapa pongezi pia kwa kuwa na nia ya kutaka kubadilika na kuomba mawazo ya watu. Kwa ujumla, mjikite ktk quality amd contents ya vipindi na muonekano wenu.
Mnajitahidi.
Kambale akishakauka hakunjiki.Mwacheni tu,mkijaribu tu kumkunja atavunjika.Hasara utapata wewe
 
Back
Top Bottom