Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unajidanganya eti BBC inatsngaza yote pole sanaaaHujaielewa sio kujitegemea kwa serikali kuondoka kuiendesha. Umeona ilivyo BBC? Hata kiongozi yoyote akikosea anazungumziwa kwa uwazi kabisa. Na anahojiwa maswali mazijo kbs na BBC (Ndivyo ilivyokuwa TBC ya Mhando). (Sivyo ilivyo TBC ya kuambiwa na wanaoiendesha kipi cha kuwekwa wazi na kipi achana nacho-hata kama kina manufaa kwa Taifa. Lakini kwa maslahi ya wachache itaambiwa hiki acha,utagusa watu fulani. Ijiendeshe yenyewe kwa namna ya habari za kiuchunguzi izilete kama ilivyozichunguza,sio mpaka tena watake watu fulani nje ya chombo chenyewe
TBC niwaulize mlisema
Mtajenga kituo kikubwa cha radio Arusha na kitakua na habari kemkem
Na usikivu mkubwa. Mmefikia wapi?
Kwa hiyo kwa tathmini ya haraka haraka inaonyesha toka uzi uanzishwe takrinsni mwaka 1 sasa, TBC hawajapokea maoni ya wadau kuhusu kuboresha vipindi vyao kwa zaidi 90%. Najiuliza je sisi wadau ndio hatujui tunachoshauri au?Yaani mnaona heri kumuonesha mkuu wa mkoa live, Rais live, ujio wa ndege Live, lakini kila kitu mkiweke gizani. Mnaona raha hasa kutuonesha wanyama wa porini lakini. Timu za Taifa zikicheza ni gizani, saa hizi kuna hadi michuano ya timu ya Taifa wanawake, lakini kuiona hadi utafute Azam au ZBC, timu ya Taifa inacheza leo pia, hamjawahi kuthubutu hata kidogo kujua kwamba kuna watanzania zaidi ya milioni hamsini wanataka kuiona timu yao hata bure kupitia TBC ikicheza.
Hivi nyie mnakwama wapi, ni kipi kipau mbele chenu kwa umma huu wa watanzania? Makonda akiongea mnakuwa live (siyo kwa nia mbaya nalisema hili), bombardier zikija tena mnawahi vibaya mno, teuzi na watu wakiapishwa mko live, sasa basi kwa nini timu zetu za taifa zikicheza msione umuhimu wa kurusha hizi mechi? Zanzibar inaweza kurusha hizi mechi, kwa budget ipi ambayo nyie hamna? Muda wote mnaweka mavipindi ya ajabu ajabu ya marudio rudio tu, hivi mnakwama wapi?
Kwa hiyo
Kwa hiyo kwa tathmini ya haraka haraka inaonyesha toka uzi uanzishwe takrinsni mwaka 1 sasa, TBC hawajapokea maoni ya wadau kuhusu kuboresha vipindi vyao kwa zaidi 90%. Najiuliza je sisi wadau ndio hatujui tunachoshauri au?
Ndugu WanaJF,
Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa picha na ubunifu wa vipindi.
Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.
Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.
Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.
Karibuni sana.
Sijui mnakwama wapi maana ukisema muongeze channel series tutakuwa waongo maana kuna TBC1, TBC2, TBC international...ambazo mna nafasi ya kuweka mpangilio mzuri wa vipi vinavyoweza kuwavutia watazamaji kamaNdugu WanaJF,
Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa picha na ubunifu wa vipindi.
Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.
Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.
Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.
Karibuni sana.
Ipo,kwani wewe unaishi njee ya Tanzania?Kumbe kuna channel inaitwa TBC!?[emoji44][emoji1549][emoji1549][emoji1549]
Sehemu kubwa uko vizuri, kuna mambo nimeshindwa kuyaelewa eti eti vyeti visiangaliwe iangaliwe kipaji? Ni TV gani isiyozingatia taaluma bali vipaji iko vizuri nipe mfano wake, umesema ccm ianzishe vyombo vyake(radio Uhuru,magic,na chanelten) viko,jee kwanini usiseme vyama vya upinzani vianzishe vyombo vyao vya habari kwanini useme ccm ndio waanzishe mantiki yako ni nini?Sijui mnakwama wapi maana ukisema muongeze channel series tutakuwa waongo maana kuna TBC1, TBC2, TBC international...ambazo mna nafasi ya kuweka mpangilio mzuri wa vipi vinavyoweza kuwavutia watazamaji kama
1.matangazo ya mipira live.
Katika kitu ambacho watanzaniwa wamejaribu kupenda kutoka moyoni na kuweka kando tofauti zao ni MPIRA hivyo zingatieni hili.
2. Vipindi vya technology
Tupo kwenye karne ya utandawazi ambayo technology inakuwa kwa kasi. Hapa ni vizuri kuwa na vipindi vizuri kuhusu technology waalike wataalam na kutoa mada nzuri ambazo hata watazamaji wataweza kuvutiwa navyo.
Mfano: namna gani ya kukuza kipato chako kwa kutumia fursa ya uwepo wa technology, lets say kutoka laki 5 mpaka million 5.
3. Wekeni kipindi maalum kila siku ambacho kitaeleza miongozo mbali mbali kwa watanzania.
Mfano: mnaweza leo mkatoa muongozo wa kiserikali....vitu gani vinahitajika ili mtu aweze kupata leseni ya biashara,,,leseni ya kumiliki vitalu vya madini,,,hati ya ardhi na vinginevyo vizuri ambavyo vinagusa watanzania.
Kwani watanzania wengi hawaelewi wapi waanzie na nini kinatakiwa wanajikuta wanapoteza gharama nyingi na muda mwingi kwa safari za nenda rudi nenda rudi.
3. Namba kubwa ya vijana sasa hawana ajira tafute vipindi maalum kwa ajili ya hilo tatizo na namna gani ya kuwafanya waweze kujiajiri wenyewe.
Mfano: mnaweza kutafuta wamiliki wa taasisi za kifedha wakawa na vipindi vyao maalumu na kutoa miongozo mizuri ya namna ya kupata mikopo kwenye taasisi zao.
4. Ondoe matangazo ya chereko chereko, biko, sportpesa na wengineo yapelekeni kwenye channel za michezo.
5. Wekeni kipindi maalum cha kuwaalika wanasiasa kutoka upinzani watoe ushauri wao jinsi ya kujenga taifa letu na kero zao kwani wana mchango mkubwa kwenye mabadiliko ya nchi hii.
6. Wekeni channel maalum kwa watoto.
7. Mnasema TBC ni ukweli na uhakika...? Lakini kuna makosa mengi yanatokea kwenye utoaji wa taarifa hupelekea uhakika kuwa zero, nanukuu,,,,mh.princess square amefanya ziara ya kutembelea uwanja wa ndege wa songwe mkoani ruvuma(makosa hayo yapo mengi yatazameni, pia watangazaji waache kupotezea wawe wepesi wa kusahihisha)
8. Mwonekano wa picha ni mbovu, kutatikakatika kwa mitambo kumekidhiri,
Mfano: mh.raisi alikuwa live mahali fulani mitambo ilikatika, hilo ni doa kubwa kwa uongozi mzima wa tbc.
9. Kwa kuwa station ni ya taifa wekeni masuala ya utaifa zaidi,
Jamii ina mambo mengi sana wamekosa pa kusemea hivyo kuweni wabunifu na kucheza na changamoto zilizopo kwenye jamii.
Mfano: kuwe na kipindi maalum kiitwe KERO NDANI YA JAMII
Namba zenu ziwe wazi watanzania waweze kutoa kero zao.
10. Ondoeni elimu vyeti tafuteni watu talented wapo wengi sana
Cheti bila ubunifu ni zero kwa karne ya sasa iliyotawaliwa na utandawazi na ukuaji wa technology kwa kasi.
11. Mambo ni mengi muda ni mchache lakini zingatie haya ni muhimu sana kuwe na vipindi vya maswali na majibu kwa viongozi haswa kuhusu
....uwekezaji
....aridhi
....kilimo
....ufugaji
....afya
...mifuko ya hifadhi ya jamii
....elimu
....usafiri
NB2: kipindi maalum cha miongozo sahihi.
Mfano: mgonjwa ameenda hospital amehudumiwa vibaya...sasa mkiwa na vipindi karibu kila idara, anaweza kujua wapi aanzie ili apate haki yake.
NB3: nashauri chama cha mapinduzi kianzishe media zake kiache kutumia station ya taifa nao wanachangia kuiharibu TBC.
Kwa leo niishie hapa.
Kuhusu channel za ccm zipo lakini TBC inatumiwa vibaya maana haiweki usawa kwa vyama vya siasa, kumbuka hiyo ni station ya taifa, rejea kipindi cha muhando TBC ilikuwa hivyo?Sehemu kubwa uko vizuri, kuna mambo nimeshindwa kuyaelewa eti eti vyeti visiangaliwe iangaliwe kipaji? Ni TV gani isiyozingatia taaluma bali vipaji iko vizuri nipe mfano wake, umesema ccm ianzishe vyombo vyake(radio Uhuru,magic,na chanelten) viko,jee kwanini usiseme vyama vya upinzani vianzishe vyombo vyao vya habari kwanini useme ccm ndio waanzishe mantiki yako ni nini?
Kutumiwa vibaya kivipi? Ukitangaza upinzani ni sawa siyo? Mengi nimekukubari ila baadhi sikubaliani nawe,elimu ni muhimu sanaa,jua Chanel ya serikali haiwezi kua kama nyingine kwa hali yoyote ile kwani kila chombo kina Sera yake.Kuhusu channel za ccm zipo lakini TBC inatumiwa vibaya maana haiweki usawa kwa vyama vya siasa, kumbuka hiyo ni station ya taifa, rejea kipindi cha muhando TBC ilikuwa hivyo?
Kuhusu vyeti sijamaanisha wasio na vyeti kabsa, mtu ana diploma au cerficate plus kipaji chake hachukuliwi kiurahisi hapo.
Wanaoangalia vipaji wapo wengi na wanafanya vizuri na wanaendelea kupendwa daily hakuna haja ya kutaja kama wewe mi mfuatiliaji utakuwa umeona
Elimu tu bila ubunifu kwa karne ya sasa ni failure.
NB: Tuna bahati mbaya kuwa kama binadamu tukiambiwa ukweli lazima tuumie lakini ukweli ni Tiba.
wanapata ruzuku kupitia kodi zetu, hivyo ni wajibu wetu kusema kasoro zao ili wajirekebishe.
Ingawa nashangaa mh.ayub pamoja na ubobezi wake ameshindwa kuisimamia TBC iwe the super brand Afrika masharik na kati[emoji20]
Sent using Jamii Forums mobile app
kweli mkuu, hii itakuwa wanafanya maksudi, muda wooote vipindi wanavyo weka na kuvifatilia ni vile vinavyosema Jiwe Jembe, hawana kipindi chochte live cha kumsisimua mtu, vyote ni praising programmes...