TBC ni TV ya waislam na wakristo wakatoliki?

Kwa nini TV ya taifa inabeba jukumu la kutangaza dini za watu. Hizo taasisi husika hazina majukwaa ya kufanya hayo mambo yao ?
Sio jukumu la la Tv ya Taifa kutangaza dini za watu. Tv ya Taifa ni jukwaa la wananchi wote, kupata habari na taarrifa mbalimbali za kitaifa na kimataifa kuhusu masuala kadhaa wa kadhaa mathalani sanaa na michezo, kilimo, ufugaji na uvuvi, biashara na masoko dini, mila na desturi njema za kuendelezwa n.k.

Kuhusu Tv ya Taifa kubeba jukumu la kutangaza dini si kweli.
Wahusika wenye dini zao ndio wanajukumu hilo. Tv ni platform tu ya kuwafikia watu wengi zaidi kwa pamoja na kuwafikishia ujumbe mahususi kwa muda mfupi...
 
Walipaswa kutumia platforms zao kutangaza mambo yao sio television ya taifa kutangaza mambo yao
 
Tanzania ina watu milioni 66 wakatoliki ina wafuasi milioni 49 Waislamu milioni 16 KKKT (Waprotestant) laki 3, Waadventista Wasabato/Walokole Laki 2.5 pentekoste laki 1.2 Anglican elfu 70 Wahindu 21,732 Kakobe 13,123 Kuhani Mwacha 7290, Mwamposa Bulldozer 6200, Mzee wa upako 5400, Judaism 2 (CAG mstaafu na Mzee mmoja anakaa maeneo ya Goba)
 
Walipaswa kutumia platforms zao kutangaza mambo yao sio television ya taifa kutangaza mambo yao
kesho utasema na wasanii wanapaswa kutumia platform zao, keshokutwa utasema walemavu na wenye mahitaji maalumu watumie platform zao pia, kwasabb hii ni Tv ya Taifa....

Hutaishia hapo bado utasema wavuvi, wafugaji na wakulima wasaitumie TV ya taifa kutangaza mipango yao ya kilimo watumie platform zao kufanya mambo yao....

Ukiona wasanii na kazi zao utasema hao nao watafute platform yao hii ni Tv ya Taifa.

Hutaishia hapo utakuja kusema tena wanasiasa wasitumia Tv ya Taifa watumie platform zao huko mtaani....

Baadae utasema watu weusi na weupe kila moja atafute platform zao maana hii ni Tv ya Taifa.....

Ubaguzi hautaishia hapo ntaendelea baada ya muda kidogo...
 
Huu mfumo wa hizo dini mbili kutangazwa TBC, ulianzishwa enzi za Nyerere, wakati huo tulikuwa na kituo cha Radio tuu, na hizo dini zilina wakilishwa na katoliki na Suni, japokuwa kuna Madhehebu mengi ya Kikristo na Madhehebu mbili za kiislamu. Mfumo unaendelezwa kama Nyerere alivyo penda, kwani Nyerere aliupigania sana UKATOLIKI
 
We kichwa maji kweli...Walutheri 300,000
 
Binafsi sijakuelewa kwani wewe uko upande gani?unasema ukristo na uislamu sasa itangaze upagani au!Hiyo ni biashara bro kama na wewe unataka kujitangaza kalipie tu utakuwa hewani.acha kulalamika kama vile ulikataliwa kujitangaza vile!
 
This is a matter of no public interest.
Wengi wammeshtuka - duh! hivi kuna watu wanaangalia TBC?
 
ACHA WAENDELEE KUTAFUTA VIEWERS KWA MGONGO WA DINI, NA WATAWAPATA SANA
 
Mimi ni Msabato nitaanza kuangalia kipindi hicho.
 
Na ibada za Wahindu pia, wanalipa kodi kubwa sana waumini wake.
 
Masahihisho : Kwa Waislam wanaotangazwa ni BAKWATA tu , wengine hawahusishwi
 
Na ibada za Wahindu pia, wanalipa kodi kubwa sana waumini wake.
kwa kweli wale watu sijawahi kuona ibada zao zinafanyikaje wala kuwajua viongozi wao wa dini. Kama hawaoni mwiko ibada zao kuonekana kwenye media wapewe airtime/coverage na wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…