Tetesi: TBC wafanya kikao usiku wa manane, kimeisha saa 11 alfajiri

Ukiona Juma Ponda Mali anapiga simu kusifia kipindi ama kituo chako basi uanze kujitathimin mapema...maake yeye huwaga hazingatii viwango wala maadili kwenye issue zake.
...sasa huyu mkurugenzi naye anaona kufanikiwa ni kupigiwa simu...loh...hili ni tatizo kubwa.

.....by the way nilikuwa na iman kubwa na mkurugenzi huyu-ila sijui Nani kamfundisha..uoga na unafki.
 
TBC inejiua yenyewe kwa kukubali kuwa wakala wa CCM na kuwa adui wa vyama vya upinzani wala wasitafute mchawi.
 
Waiite TBCCM nafikiri maudhuwi yatakuwa yamewakilishwa vizuri kabisaa
 
KAMA HATA IKULU HAIJUI KAMA KUNA TBC MIMI JE?......CHANNEL ZANGU NI EATV CLOUDS TV CHANEL.TEN
 
TBC inejiua yenyewe kwa kukubali kuwa wakala wa CCM na kuwa adui wa vyama vya upinzani wala wasitafute mchawi.
Wana anza anzaje kuacha kuitumikia ccm wakati ni channel ya chama ccm ni sawa sawa na kukataza gazeti uhuru wasiandike habari za ccm
 
Kwahiyo kikipendwa na rais ndio kitakuwa bora?mimi nilifikiri kupendwa na wateja ndio mwanzo wa kuboreka
 
TBC wanavuna kile walichopanda,sina uhakika kama kufanya kikao cha dharura usiku wa manane,kitasaidia kitu.Solution ni kuwajenga watumishi wake kisaikologia kupasha habari wakizingatia kanuni na wajibu wa wahandishi wa habari
 
Kulamba miguu ya ccm kunadhalilisha TBC na wafanyakazi wake , siku nikianzisha TV station Yangu ( NINA MPANGO HUO ) sitathubutu kuajiri aliyewahi kufanya kazi TBC , wamedharauliwa mno na wananchi , mijini na vijijini .

Poor TBC !
 
Nape alipokataza Bunge live ndio hapo TBC ilipojifia.
Bunge live ndio kipindi pekee kilichokuwa kinafwatiliwa na watanzania.

Wajitafakari wakiwa huru ndio wataweza kujinasua, lasivyo tope linazidi kuganda huku wakiwa wamezama
 
*Waache kuingiza siasa (TBC inaonekana ni ya CCM).

*Wawe wabunifu.
 
Waache ku act kizee zee,
Asilimia kubwa ya watazamaji ni vijana, wawe na vipindi vingi vya Vijana,
Waweke watangazaji Vijana wanaoenda na wakati,
Waandae hata matamasha kama ilivyo Clouds,
Otherwise Rais anawaangusha pia, kama anaona watoto wake hawafanyi vizuri basi hakuna haja ya kujivunia mtoto wa jirani, angeenda nao hivyo hivyo tu.
Kwenye Ule mkutano wa Jukwaa la Wahariri aliwasifia Fiesta na Clouds, juzi katuma kadi Coulds.
 
Wakati Alipo kuepo Tido Muhando Aliludisha Iman Kwawatazamaji Lkn Alipo Ondoka Wakaludi Ktk Mfumo Wao Kama Chombo Cha Kisiasa Mimi Kwangu Imekua Nikama Mwiko Kutadhama Chombo Icho Mpaka Watakapo Jirekebisha
Huyu walimwondoa.

TV inaendeshwa na Wanasiasa badala ya watalaamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…