Mkurugenzi mkuu, watu wako si wabunifu bado wana mind sets za kuzamani, wanajua wajitahidi wasijitahidi awawezi kukosa mshahara - Serikali itawapa TBC ruzuku ya kujiendesha na kulipa wafanyakazi mishahara kwa nini wapoteze muda wa kuangihika kuwa wabunifu.
Wakati mwingine huwa najiuliza hivi TBC isingeshirikiana na Startimes mambo yangekuwaje?
Chukulia mfano mdogo wa kusambaza matangazo nchi nzima, kwa nini wali g'ang'ania kutumia njia ya terrestrial ambayo inagharimu fedha nyingi kuitekeleza na ina changa moto lukuki kusambaza nawimbi yake nchi nzima - je mainjinia Wantanzania wa TBC na wakurugenzi husika wanaweza kuwaeleza Watanzania blunder/zoezi hilo ambalo halijakamilika litagharimu fedha za walipa kodi kwa kiasi gani.
Miaka ya nyuma niliwahi kutoa ushauri kwa nia nzuri kwamba Serikali/Startimes watumie mfumo wa satellite kusambaza mawimbi nchi nzima wakapuuzia, baadae kaja AZAM akatumia mfumo wa satellite na kuweza kusambaza mawimbi nchi nzima and beyond kirahisi kwa kutumia Satellite at a record time ndio na TBC/Startimes wakashituka na kuanza kutumia mfumo huo huo na wa satellite na terrestrial at ago !!
Sasa swali ni: Nani atagharimia blunder hizo, je mafundi/mainjinia/wakurugenzi wakuu wa ufundi wa TBC kazi zao ni nini? kuwasikiliza Wachina bila ya wao kutoa mchango wowote wa kuifundi, mradi kasema mbia nyinyi hamna mamlaka ya kubishana nao hata kama wanayo taka kutekeleza yataigharimu sana kifedha Serikali au ujenzi wa kusambaza mawimbi nchi nzima Wachina awatatutoza chochote i.e ni msaada!