TBC wamekata matangazo ya Bunge kuficha Sheria ya Manunuzi inayoruhusu Serikali kununua ndege, treni na meli za mitumba?

TBC wamekata matangazo ya Bunge kuficha Sheria ya Manunuzi inayoruhusu Serikali kununua ndege, treni na meli za mitumba?

Mwigulu Nchemba amependekeza kwenye Sheria mpya ya Manunuzi Serikali inunue Ndege, Vichwa vya Treni, Mabehewa ya Treni, Meli zilizotumika badala ya kuagiza mpya na wabunge wanasherehekea bungeni kwa sababu wanajua wananufaika na nini kufanya maamuzi hayo.

Sheria hii ikipita iko siku taifa litakuja kuomboleza msiba mkubwa utakaosababishwa na maamuzi ya leo pale Meli zitapakuja kuzama, ndege kuungua angani, treni kuua watu wakati huo Mwigulu yuko zake ughaibuni hayuko tena tanzania. Sisi familia zetu zinakwenda kupoteza maisha kwa maamuzi ya leo kisa tu watu wamekula rushwa kufanya maamuzi hayo.

Hii Sheria ni moja ya Sheria mbovu na iliyojaa mazingira ya rushwa kwa watu wachache wenye madaraka kwa sasa kina mwigulu na washirika wake.

Tuliombee taifa letu tuko kwenye hatari kubwa.

Mbaya zaidi Bunge haliko live kwenye TV ili watanzania wasijue kinachojadiliwa na kupitishwa na Bunge.
Una uhakika?
 
Hakika ni kwamba tunarudi kuleee kwa kina Kikwete na Pinda....
[emoji116][emoji419]

Jikumbusheni hapa.
PAMOJA na jitiada za makusudi za Waziri Mkuu Mizengo Pinda Jumatano Julai 25 2012, alifanya kazi ya ziada kuzima hasira za wabunge waliokuwa wakitaka kuona Waziri wa Nishati na Madini, Pofesa Sospeter Muhongo, na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi, wakiwajibika kwa kujiuzulu nyadhifa zao vinginevyo wangekwamisha bajeti ya wizara hiyo.

Kwa kipindi cha wiki moja sasa, kumekuwa na mpango unaoratibiwa na baadhi ya wabunge wakiwamo wa CCM na upinzani wanaotaka hatua hizo zichukuliwe.

Chanzo cha habari hizo kinadai wabunge walifikia hatua hiyo baada ya vigogo hao kuripotiwa kuwa waliruhusu ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ya umma kwa kuipa zabuni kampuni ya Puma Energy (T) Ltd zamani BP.

Kampuni hiyo ilipewa zabuni ya kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na kuziweka kando kampuni zilizokuwa zimechaguliwa kupitia mchakato halali wa zabuni ya TANESCO.

Suala hilo linahusishwa na kusimamishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, William Mhando, kwamba alichukuliwa hatua baada ya kukataa kutii maelekezo ya wizar

....
Mkuu Edward Lowassa, kuachia ngazi.

“Tulimtosa Lowassa, baadaye ukweli umejulikana, na sasa makosa yetu yanaigharimu serikali na CCM. Tusirudie makosa yale yale, tuwaache hawa kwa maslahi ya CCM,” alisema.

Hata hivyo baadhi ya wajumbe walishikilia msimamo wa kuwajibishwa kwa Muhongo na Maswi kwa madai kuwa endapo wataachwa, wataimaliza serikali ya CCM.

Walisema kuwaacha ni sawa na kulitangazia taifa kwamba wao ni wavunjaji wa sheria walizozitunga wenyewe.
 
Hao maboya bungeni washazoea kununua 'K" papuchi za mtumba! Wanaleta haya maswala kwenye vitu serious!?
 
Madalali wa kimataifa wameshafanya lobbying ya kutosha hadi kubadilisha sheria. Hakuna mtumba wenye warranty. Kwa sheria hii, tumekwisha, watu watakufa, hakuna uwajibikaji wa mnunuzi, makampuni ya insurance yatakwepa kulipa fidia etc. Muuzaji wa ndege au train kukuu huuza zikiwa zimechoka na kuna uwezekano wa kuuziwa zisizofaa kwa matumizi tena.
 
Hao wajinga hawajielewi, nguo za mitumba NO, ndege za mitumba YES.

Umaskini mbaya sana, huwezi kuwa na msimamo.
Umasikini na misimamo havikai nyumba moja.

Masikini jeuri ni msemo tu usiuweke kwenye akili - Mwana FA
 
Mwigulu Nchemba amependekeza kwenye Sheria mpya ya Manunuzi Serikali inunue Ndege, Vichwa vya Treni, Mabehewa ya Treni, Meli zilizotumika badala ya kuagiza mpya na wabunge wanasherehekea bungeni kwa sababu wanajua wananufaika na nini kufanya maamuzi hayo.[emoji3064][emoji3064][emoji3064]

Sent using Jamii Forums mobile app
Imefika mahali natafakari wanangu kuwatolea laana ya utamzania
 
Mwigulu Nchemba amependekeza kwenye Sheria mpya ya Manunuzi Serikali inunue Ndege, Vichwa vya Treni, Mabehewa ya Treni, Meli zilizotumika badala ya kuagiza mpya na wabunge wanasherehekea bungeni kwa sababu wanajua wananufaika na nini kufanya maamuzi hayo.

Sheria hii ikipita iko siku taifa litakuja kuomboleza msiba mkubwa utakaosababishwa na maamuzi ya leo pale Meli zitapakuja kuzama, ndege kuungua angani, treni kuua watu wakati huo Mwigulu yuko zake ughaibuni hayuko tena tanzania. Sisi familia zetu zinakwenda kupoteza maisha kwa maamuzi ya leo kisa tu watu wamekula rushwa kufanya maamuzi hayo.

Hii Sheria ni moja ya Sheria mbovu na iliyojaa mazingira ya rushwa kwa watu wachache wenye madaraka kwa sasa kina mwigulu na washirika wake.

Tuliombee taifa letu tuko kwenye hatari kubwa.

Mbaya zaidi Bunge haliko live kwenye TV ili watanzania wasijue kinachojadiliwa na kupitishwa na Bunge.
Enzi za Nyerere ATC iliwahi kukodi ndege marehemu toka kwa mpalestina George Hallack, siku ya uzinduzi wa safari yake ya kwanza toka Dar es Salaam kwenda London ndege ilikuwa kama Dar Express, ilikwenda mpaka mwisho wa uwanja ikagoma kuruka! Ilibidi basi la uwanja wa ndege likawachukue abiria na kuwarudisha mjengoni, hiyo ndege iliishia hapo uwanjani na hakuna mtu yeyote aliyechukuliwa hatua. Magufuli, aliagiza meli kwa ajili ya abiria kati ya Dar na Bagamoyo, meli ilianza safari kwa mbwembwe zote za kiccm, ilichukua saa mbili toka bandarini Dar mpaka Kunduchi! Magufuli akateremka na kurudi mjini, meli ilitelekezwa bandarini na hakuna aliyechukuliwa hatua, pia kuna manyangarakasha mengine mengi tu yaliyokula pesa zetu huku tukiongezewa kodi kufidia hasara.
 
Una hela ya kununua vipya!?..Kodi unakwepa,tozo ulizisakama,kukopa unapigia kelele, kuwekeza bandari unafanyia maombi lisiwezekane
Lakini hel za Kununua silaha navitendeakazi vingine vya polisi Kwa ajili ya kusimamia uchaguzi wa siku Moja bil 125 zipo eti?
 
Madalali wa kimataifa wameshafanya lobbying ya kutosha hadi kubadilisha sheria. Hakuna mtumba wenye warranty. Kwa sheria hii, tumekwisha, watu watakufa, hakuna uwajibikaji wa mnunuzi, makampuni ya insurance yatakwepa kulipa fidia etc. Muuzaji wa ndege au train kukuu huuza zikiwa zimechoka na kuna uwezekano wa kuuziwa zisizofaa kwa matumizi tena.
Actually sheria mpya inawabeba zaidi wazalishaji na suppliers wazawa
 
Manyumbu bungeni huko yatapitisha kwa sauti moja kubwa ila yakitoka huko waje kutuambia hawakujua kilichoandikwa
 
Tunaiponda serikali wakati sisi wenyewe tunajipongeza na kujiona tumepiga hatua za kimaendeleo kwa kununua Magari mitumba, nguo za mtumba, vyombo vya majumbani vya mitumba. Wanaotuongoza hawatoki mwezini ni miongoni mwetu ndo maana sishangai wala kuwalaumu kwa hiyo sheria hao ndio sisi sasa. Kama wewe huwezi kununua gari 0 kilometre kuna mazingira pia serikali inaweza kushindwa kutumia fedha nyingi kwaajili ya kupata kipya ambapo vipo mitumba yake ambayo vinaweza kusukuma siku wakati huo uwezo wa kiuchumi wa kununua vipya unakusanywa
 
Ulevi wa Madaraka ukichanganya na Rushwa na Upigaji unapata Viongozi wa ajabu kabisa.
 
Back
Top Bottom