Mwigulu Nchemba amependekeza kwenye Sheria mpya ya Manunuzi Serikali inunue Ndege, Vichwa vya Treni, Mabehewa ya Treni, Meli zilizotumika badala ya kuagiza mpya na wabunge wanasherehekea bungeni kwa sababu wanajua wananufaika na nini kufanya maamuzi hayo.
Sheria hii ikipita iko siku taifa litakuja kuomboleza msiba mkubwa utakaosababishwa na maamuzi ya leo pale Meli zitapakuja kuzama, ndege kuungua angani, treni kuua watu wakati huo Mwigulu yuko zake ughaibuni hayuko tena tanzania. Sisi familia zetu zinakwenda kupoteza maisha kwa maamuzi ya leo kisa tu watu wamekula rushwa kufanya maamuzi hayo.
Hii Sheria ni moja ya Sheria mbovu na iliyojaa mazingira ya rushwa kwa watu wachache wenye madaraka kwa sasa kina mwigulu na washirika wake.
Tuliombee taifa letu tuko kwenye hatari kubwa.
Mbaya zaidi Bunge haliko live kwenye TV ili watanzania wasijue kinachojadiliwa na kupitishwa na Bunge.
Hakika ni kwamba tunarudi kuleee kwa kina Kikwete na Pinda....
[emoji116][emoji419]
Jikumbusheni hapa.
PAMOJA na jitiada za makusudi za Waziri Mkuu Mizengo Pinda Jumatano Julai 25 2012, alifanya kazi ya ziada kuzima hasira za wabunge waliokuwa wakitaka kuona Waziri wa Nishati na Madini, Pofesa Sospeter Muhongo, na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi, wakiwajibika kwa kujiuzulu nyadhifa zao vinginevyo wangekwamisha bajeti ya wizara hiyo.
Kwa kipindi cha wiki moja sasa, kumekuwa na mpango unaoratibiwa na baadhi ya wabunge wakiwamo wa CCM na upinzani wanaotaka hatua hizo zichukuliwe.
Chanzo cha habari hizo kinadai wabunge walifikia hatua hiyo baada ya vigogo hao kuripotiwa kuwa waliruhusu ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ya umma kwa kuipa zabuni kampuni ya Puma Energy (T) Ltd zamani BP.
Kampuni hiyo ilipewa zabuni ya kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na kuziweka kando kampuni zilizokuwa zimechaguliwa kupitia mchakato halali wa zabuni ya TANESCO.
Suala hilo linahusishwa na kusimamishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, William Mhando, kwamba alichukuliwa hatua baada ya kukataa kutii maelekezo ya wizar
....
Mkuu Edward Lowassa, kuachia ngazi.
“Tulimtosa Lowassa, baadaye ukweli umejulikana, na sasa makosa yetu yanaigharimu serikali na CCM. Tusirudie makosa yale yale, tuwaache hawa kwa maslahi ya CCM,” alisema.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe walishikilia msimamo wa kuwajibishwa kwa Muhongo na Maswi kwa madai kuwa endapo wataachwa, wataimaliza serikali ya CCM.
Walisema kuwaacha ni sawa na kulitangazia taifa kwamba wao ni wavunjaji wa sheria walizozitunga wenyewe.