Hakika hii nchi tunapoelekea sasa naamini tunaanza kuingia katika zama za kidictator kwa kubana uhuru wa kupata habari pamoja na kupata habari sahihi kwa muda muafaka.
Tangia rais mpya (JPM) aingie madarakani, ilionekana ameanza vizuri kwa kasi ya ajabu katika mambo mbali mbali iliyoamsha mategemeo mengi ya wananchi wa Tanzania walioamini kweli sasa amepatikana rais bora atakayeweza vusha watanzania katika wimbi hili la umaskini uliokithiri miongoni mwa watanzania wengi, zaidi ya nusu.
Ila cha kushangaza democrasia ikaanza kukandamizwa taratibu na sarakasi za hawa wanaojiita watenda haki (ccm) kwa ujumla wake katika chaguzi za mameya hapa jijini dar es salaam katika wilaya mbili muhimu lakini baadaye ukawa waliibuka kidedea kutokana na mshikamano wake katika kuamini kuwa hawa wezi (ccm) watakondolewa tu umoja wao usipotetereka. Na cha kushangaza wakati haya yanatendeka aliyejiita rais wa wote wala wasaidizi wake hawakujitokeza kukemea hujuma za wanachamama wao katika hili suala, huku sheria zikionekana wazi kujaribu kupindishwa ili tu kuwabeba.
Pili likaja suala la gazeti la mawio kufungiwa moja kwa moja kwa sababu dhaifu kuwa habari zake zinachochea vurugu. sasa hapa unajiuliza, hivi hii nchi kweli ni yenye kujali democrasia na uhuru wa vyombo vya habari, maana imeonekana wazi kuwa magazeti yanaoandika habari na makala za kipelelezi (investigative journalism) zenye kugusa moja kwa moja serikali na madudu yake hayatakiwi katika nchi hii. Hili liliwahi kujitokeza huko nyuma kwa gazeti la mwanahalisi kufungiwa kwa sababu kama hizi ila baadaye likaja kushinda kesi na kurudi mtaani huku watu wakiendelea kulisoma.
Tatu ni hili la leo kusema kuwa vikao vya bunge havitakuwa vinarushwa live tena bali vitakuwa vinarekodiwa na kurushwa kwa saa limoja usiku, sababu ikiwa dhaifu mno (bilioni 4 kwa mwaka ni nyingi sana). katika watu walio na mtindio wa akili, huyu jamaa au aliyemtuma, mtindio wake ni wa hali ya juu. Katika zama hizi, zinazosemekana ni za ukweli na uwazi, bilioni 4 kwa mwaka kurusha matangazo ambayo ni roho ya nchi, ni pesa gani? Na bado hapo hapo tbc inapokea ruzuku kutoka serikalini ambazo ni kodi zetu sisi wananchi. Hii nchi ni kituko sijawahi ona. Hakika naona taratibu tunafungwa midomo pamoja na kutotakiwa kusikiliza mijadala mbali mbali inayoendelea bungeni ambako ndiko hoja mahsusi na nzito zinapoibuliwa na wabunge mbali mbali kutokana na accessibility yao ya taarifa na pia sisi wananchi kupata taarifa ambazo tunaweza kuwahoji tuliowapigia kura pale tunapokuwa na mashaka na mambo kadha wa kadha yaliyoibuliwa katika chombo hiki nyeti nchini.
Kwa mwenendo huu, wa kuminya democrasia kila kukicha kinachofanywa na hawa ccm, kitakuja kuzua tafrani kubwa sana nchi hii, maana mtu anapojiona kama mungu na kuamuru kuwafanyia watu anachoamua tu bila kujali mapokezi ya upande wa pili hakika athari zake ni kubwa mbeleni. Zanzibar washindwe lakini bado wang'ang'anie, bado huku bara waje na kauli kama hii.
Amani huletwa na haki na usawa, na sheria iliyopindishwa sio sheria hata kidogo.
Mungu naomba utupe nguvu na ujasiri wa kupinga hizi hujuma kwa watanzania unaofanywa na hawa mafisiemu.