TBT: Foleni ya kwenda kwa Babu wa Loliondo

Kulikuwa na matokeo chanya pia. Barabara za kufika huko ziliimarishwa, wasafirishaji na wafanya biashara za vyakula eneo lile walineemeka. Presha ilipungua Muhimbili na baadhi ya hospitali nyingine kwa manufaa ya wagonjwa waliobaki, Tanzania ilimulikwa, nk

Hivi hakuna recording ya lile tukio Tanzania Safari channel na wengine waoneshe?
 
Haya matukio yanatengenezwa kuwapumbaza Watanganyika ili Chama Twawala waendelee kutawala!
 
Miti shamba siyo ushirika, labda ilipata sifa ya kuamini miti shamba ila siyo ushirikina.
 
Mpaka leo watu wa namna hiyo wapo wengi tu, kama huamini nenda kwa wauza dawa za asili/mitishamba uone,,,, hasa wale maarufu 🫣🫣🙌🏽
Kwani kutumia mitishamba ni ujinga?
 
Mkuu usilaumu watu

Chukulia mfano ndio wewe unaumwa upo mihimbili dawa zote zimedunda

Alafu unaangalia ITV chanel credible watu wanakunywa dawa wanapona na wewe ni bilionea kifo unakiona hiki hapa

Utashindwa kukodi hrlkopta uende loliondo?
Hahaha.............hiyo hela ya kukodi Chopa si Bora nifanye nauli niende kutibiwa Apollo ama South Africa

Ila angalia hao wanaoenda kukanyaga mafuta na kunywa Maji ya baraka

Utaona Ukubwa wa tatizo tulilonalo
 
🤣🤣🤣 bad enough kuna watu walikuwa ni phd holders nao walikwenda
 
Nilishawahi kwenda mwaka 2010 mwezi wa tatu,kivumbi chake sio mchezo,shida tupu.......ilifikiwa wakati mpaka chaati moja ikauzwa kwa buku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…