TBT: Foleni ya kwenda kwa Babu wa Loliondo

TBT: Foleni ya kwenda kwa Babu wa Loliondo

Kulikuwa na matokeo chanya pia. Barabara za kufika huko ziliimarishwa, wasafirishaji na wafanya biashara za vyakula eneo lile walineemeka. Presha ilipungua Muhimbili na baadhi ya hospitali nyingine kwa manufaa ya wagonjwa waliobaki, Tanzania ilimulikwa, nk

Hivi hakuna recording ya lile tukio Tanzania Safari channel na wengine waoneshe?
 
Picha ilipigwa 2011 ambapo watu kutoka sehemu mbalimbali walifika kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kupata kikombe cha dawa kutoka kwa Ambilikile Mwasapile maarufu 'Babu wa Loliondo' ambayo watu wengi waliamini kuwa inatibu magonjwa mbalimbali
.
Source: Swahili times

Je, unakumbuka nini kuhusu Babu wa Loliondo? Naamini gen z wengi wamelisikia tu hili jina kwa juujuu.

View attachment 3120588
Haya matukio yanatengenezwa kuwapumbaza Watanganyika ili Chama Twawala waendelee kutawala!
 
Hili tukio lilitia aibu sana nchi yetu na kutupa sifa ya kuwa nchi ya wajinga wengi na inayoamini ushirikina zaidi duniani. Cha kushangaza mawaziri na viongozi wote almost walienda.. sasa elewa level hiyo ya ujinga, halafu tathmini kama viongozi hao wana uwezo wa kuleta, kushawishi, kuchochea maendeleo yoyote nchi hii.
Miti shamba siyo ushirika, labda ilipata sifa ya kuamini miti shamba ila siyo ushirikina.
 
Mpaka leo watu wa namna hiyo wapo wengi tu, kama huamini nenda kwa wauza dawa za asili/mitishamba uone,,,, hasa wale maarufu 🫣🫣🙌🏽
Kwani kutumia mitishamba ni ujinga?
 
Mkuu usilaumu watu

Chukulia mfano ndio wewe unaumwa upo mihimbili dawa zote zimedunda

Alafu unaangalia ITV chanel credible watu wanakunywa dawa wanapona na wewe ni bilionea kifo unakiona hiki hapa

Utashindwa kukodi hrlkopta uende loliondo?
Hahaha.............hiyo hela ya kukodi Chopa si Bora nifanye nauli niende kutibiwa Apollo ama South Africa

Ila angalia hao wanaoenda kukanyaga mafuta na kunywa Maji ya baraka

Utaona Ukubwa wa tatizo tulilonalo
 
Hiyo ilionesha Watanzania wengi ni wagonjwa, waliokosa kuelimika na waliokata tamaa ya maisha

Ilifikia kipindi mtu anamwondoa mgonjwa wake Hospitali ya Taifa Muhimbili eti anampeleka Kwa huyo Mzee huko Loliondo akanywe Kikombe cha dawa🙌

Sasa hivi wamehamia Kwa Mitume wananyweshwa Maji na kukanyaga mafuta 🙆

Tuna safari ndefu kama Nchi
🤣🤣🤣 bad enough kuna watu walikuwa ni phd holders nao walikwenda
 
Picha ilipigwa 2011 ambapo watu kutoka sehemu mbalimbali walifika kijiji cha Samunge, Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kupata kikombe cha dawa kutoka kwa Ambilikile Mwasapile maarufu 'Babu wa Loliondo' ambayo watu wengi waliamini kuwa inatibu magonjwa mbalimbali
.
Source: Swahili times

Je, unakumbuka nini kuhusu Babu wa Loliondo? Naamini gen z wengi wamelisikia tu hili jina kwa juujuu.
Nilishawahi kwenda mwaka 2010 mwezi wa tatu,kivumbi chake sio mchezo,shida tupu.......ilifikiwa wakati mpaka chaati moja ikauzwa kwa buku
 
Back
Top Bottom