TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

Sina Picha zote ila kumbuka enzi za
Tanganyika Bus Service pale Mwanza na rangi.za buy mpauko kiaina
Trans Africa na kahawia take kiaina
Songoro bus service
Nzegenuka Nyota ya Bwana
Nyehunge Express ingawa bado wapo wapo
Mashiku Investment
Matema Beach
Mohamed Trans
Bukwaya
.....hao most ni lake zone huko from Mwanza to various destinations
...Wengine ni down hapo...
Kwacha
Safina
Gold Line
Widambe
Mwaafrika
Makete
Siri Yako
Super Star
Railway
Kamata
Bin Klebo Bus Service
Kiswele
Sharuks
Air Msae
Air Chalinze
No Challenge
Air Shen
Bin Klebo Bus Service
Kiswele
Sharuks
Air Msae
Air Chalinze
No Challenge
Air Shengena
Zainab
Scandnavia
Special Video Coach
Tawaqal
Comfort Video Coach
Living Light
Yarabi Salama
Safari Master
Big Mayai
Jupiter
Mbarak
Ruvuma Tours Line
Matema Beach Coach
...

Nb: za chini hapo I.credit JF member mkongwe bwana yutong /yutong

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app

Songoro bus service nafikiri waliachana na huduma za usafirishaji abiria kwa njia ya basi. Wakajikita majini na hadi sasa ndio watengenezaji wakubwa wa vivuko vya serikali na binafsi
 
waTanzania waliozaliwa miaka ya karibuni hawakuyaona mabasi haya ya Railway.
Wanafunzi walikuwa wanasafiri kwa warrant halafu wizara ya elimu ilikuwa inalipa bili.

1640381116341.jpg
 
Kiswele ilikuwa inatumia masaa mawili tu from Dar to Moro believe me!! ikiwa inashusha mlima kuitafuta msamvu mnaisikia sauti yake hiyooo mnajua kabisa hii ni Kiswele bjnafsi nimefanya kazi Hood Limited kuanzia mwaka 1996 mpaka 2010 mpaka ikafikia kipindi nikawa family friend wa wamiliki ikizingatia kwamba pia walikuwa wanafahamiana na baba yangu before..Nilipiga mzigo pale enzi zile Hood ni Hood hata nilipomaliza chuo sikuona umuhimu wa kuendelea na kazi nyingine kutokana na mavumba yaliyokuwa yanapatikana hapo na mimi ndio nilitoa wazo la kuwa na route ya Nairobi Arusha hapo ndio nikazidi kugongelea msumari wa kuaminiwa lakini kizuri hakidumu niliamua kufanya majukumu yangu mengine kabisa kwa hiyari baada ya kuhitaji changamoto mpya lakini maboss zangu ambao walinilea bado nipo nao karibu mpaka kesho hasa watoto zake..Hood sio kama amefirisika hapana ukweli ni kwamba kulitokea mgogoro mzee mwenyewe akiwatuhumu watoto kuwa wanafuja mali za kampuni kwa kutumia hela kwa starehe hivyo hana nia ya kuendelea na biashara hiyo ingawa bado kampuni ilikuwa top na tulikuwa kwenye process ya kuorder mabasi mapya makaliii so akaifunga taratibu kampuni mabasi kayafungia ndani na mengine anauza kwa bei ya kutupa mgogoro huu ulikuwa hasa kati ya mzee na watoto wake hasa Tiffu na Saidy ambao ni wakubwa na ndio walikuwa wakurugenzi ukiachana na yule mwingine aliyekuwa uarabuni mpaka leo Hood Hood..mzee kaamua kuwekeza kwenye biashara nyingine kama kwenye Real estates na kununua hisa kwa baadhi ya makampuni kama Azania..asante kwa uzi huu

View attachment 2054530
Nilikuwa namchukulia hood poa but kuna siku natokea tunduma nikapanda bus yenu tulipofika moro ikawa na khitilafu ikaingizwa yard kurekebishwa duh nilikuta buses kama hamsini zime poa ndio nilitia akili
 

USAFIRI HUU HAUVUMI LAKINI BADO WAMO​



Huu ni usafiri wa kutoka Songea kuelekea Namtumbo maarufu kwa jina la 'Matimbula' ingawa kuna magari mengine ya kisasa yanayofanya safari kuelekea huko lakini gari hilo limekuwa na wapenzi wengi ingawa mwendo wake ni wa polepole kama wa kinyonga.

Huyu ni abiria aliyekuwemo kwenye basi hilo ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Abdul
[emoji1787][emoji28] mkuu hapo unatujaza bhana, inamana hiyo njia haina trafiki? Au inawanga usiku mnene?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji28][emoji28][emoji28]kha basi kama treni?abiria 200[emoji23][emoji28][emoji28]
Wenyewe wanasema mtu 70 na zingeweza fiti mle ndani lilikuwa linakimbia sio poa likifika pale ruaha Mbuyuni nje unaona blurred tu jinsi jamaa alivokuwa anapiga mwendo hatari
 
[emoji1787][emoji28] mkuu hapo unatujaza bhana, inamana hiyo njia haina trafiki? Au inawanga usiku mnene?
Mkuu Hadi 2019 mwisho mi nililiona gari hili stendi kuu songea
 
Halafu kulikuwa na NGORIKA T 150 AAD.
Hili basi jamaa alikuwa kama Burushi hivi,niliwahi kupanda hili basi mpaka leo sijaelewa kwanini sikutapika siku hiyo kutokana na ule mwendo!!.
Mkuu na mimi niliwahi panda hii chuma jamaa alimwaga moto ikabidi tuchil Chalinze kama lisaa muda usogeesogee 😀 .
 
Back
Top Bottom