TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

Ngorika a.k.a macedonia🙌🙌🙌🙌
 
kwani si kweli watoto wanafuja mali za kampuni kwa starehe... kampuni aliyoijenga kwa tabu alafu watoto wanakuja kula bata tu.. hamna wanachokijua
Vijana wengine ni shidaaa enzi hizo tuko sekondari kuna madogo walichukua Bus la baba yao linaitwa LANG'ATA BUS (Trip za Arusha to Dar) wakaja nalo shuleni aiseeee... Hii kampuni enzi hizo ilikuwa inachuana na NGORIKA BUS..
 
huyu bila shaka alikuwa mmoja wa miamba ya kusini....yeye na mwenzie amit simba.....dah ile nangurukuru na matandu walikuwa wanapasua kama kuna lami vile....tumetoka mbali sana...
Matandu ilikuwa balaa, tuliwahi kulala wiki nzima mpaka ikaletwa boti ndogo kutufaulisha.
 
Kuna ile ajali mbaya ya ABOOD BUS ambapo Lori lililokuwa limebeba bulldozer lilivaana na Bus. Yaani lile jembe la bulldozer likawakata watu vibaya sana daaah...
 
Ngorika watoto wapo na mabasi kwa majina mengine. Kiswele hatari, Sumri genesis yake Mbeya-Swanga, Tawaqal amazing, Summry luxury and Scandinavia luxury ni habari ya dunia
 
Sijaona bado super najmunisa enzi hizo vumbi tunalianzia dom mpaka shy. Asee wale ndio walikua madereva sio wa siku hizi kitu cha yuton hata hupati zile kash kash
Iyo kampuni mpaka leo bado ipo🙌🙌🙌
 
kuna kampuni zinaitwa super service na Hongera coach ni za Manyoni... hakuna mwenye kuzijua wakuu?
 
Aisee! Biashara Ina mbinu nyingi Sana. Ahsante kwa kutufunza na kutukumbusha.
 
Ni kweli kabisa mpaka sasa sijaona kampuni iliyofikia viwango vya juu kama hawa jamaa. Pale head office yao Kamata ukifika utadhani umeingia airport ndogo [emoji12][emoji12]
Ilikufa kwa sababu gani nayo hii? Kama una info.
 
Na ile iliyopo mizani ya wami shida ni nini mzee?
 
Mama yangu ulikuwa huambii kitu kuhusu HOOD,ile logo ya aigle(eagle) kila nikitafuta ya kushindana nayo sijaona...tangu nianze kuzipanda kutoka mbeya kwenda moshi sikuwahi kushuhudia ikiovertekiwa

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…