TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

1640257156986.jpg
 
Kiswele ilikuwa inatumia masaa mawili tu from Dar to Moro believe me!! ikiwa inashusha mlima kuitafuta msamvu mnaisikia sauti yake hiyooo mnajua kabisa hii ni Kiswele bjnafsi nimefanya kazi Hood Limited kuanzia mwaka 1996 mpaka 2010 mpaka ikafikia kipindi nikawa family friend wa wamiliki ikizingatia kwamba pia walikuwa wanafahamiana na baba yangu before..Nilipiga mzigo pale enzi zile Hood ni Hood hata nilipomaliza chuo sikuona umuhimu wa kuendelea na kazi nyingine kutokana na mavumba yaliyokuwa yanapatikana hapo na mimi ndio nilitoa wazo la kuwa na route ya Nairobi Arusha hapo ndio nikazidi kugongelea msumari wa kuaminiwa lakini kizuri hakidumu niliamua kufanya majukumu yangu mengine kabisa kwa hiyari baada ya kuhitaji changamoto mpya lakini maboss zangu ambao walinilea bado nipo nao karibu mpaka kesho hasa watoto zake..Hood sio kama amefirisika hapana ukweli ni kwamba kulitokea mgogoro mzee mwenyewe akiwatuhumu watoto kuwa wanafuja mali za kampuni kwa kutumia hela kwa starehe hivyo hana nia ya kuendelea na biashara hiyo ingawa bado kampuni ilikuwa top na tulikuwa kwenye process ya kuorder mabasi mapya makaliii so akaifunga taratibu kampuni mabasi kayafungia ndani na mengine anauza kwa bei ya kutupa mgogoro huu ulikuwa hasa kati ya mzee na watoto wake hasa Tiffu na Saidy ambao ni wakubwa na ndio walikuwa wakurugenzi ukiachana na yule mwingine aliyekuwa uarabuni mpaka leo Hood Hood..mzee kaamua kuwekeza kwenye biashara nyingine kama kwenye Real estates na kununua hisa kwa baadhi ya makampuni kama Azania..asante kwa uzi huu

View attachment 2054530
Jamaa aliyekuwa a anamchora yule mwewe nyuma ya basi alikuwa anaitwa MKAVINGA
 
Back
Top Bottom