TCRA: Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji

Inaitwa 'a taste of your own medicine'.
 
😂😂😂,chakubanga enzi za mwendazake wakati anatembelea V8,ndipo zilipitishwa hizi Sheria za hovyo na kwasababu alijua haziwezi kumgusa basi akawa anakula tu bata kwenye V8 na kuwananga wengine!
Leo hii kisu kile kile kinapita kwake,na ana bahati maana angeweza kubambikwa kesi za uhujumu uchumi akasota jela bila dhamana!
 
Mbona TCRA imeshindwa kuwafungia akina Maria Sarungi TCRA wakati maudhui yao ni ya hovyo sana kuliko hayo ya Polepole?
 
 

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imemtaka aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM) ambaye kwa sasa ni Mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole kusimamisha maudhui ya kipindi chake cha Shule ya Uongozi kinachoruka kupitia Humphrey Polepole Online TV.

Uamuzi huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa TCRA, Hans Gunze ambapo amesema uamuzi huo unakuja baada ya kutenda makosa matatu ikiwemo kuzungumzia Deni la Taifa, Virusi vya Corona na suala la Machinga (Kwamba Wakuu wa Mikoa hawakufuata utaratibu).

"Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Humphrey Polepole Online Tv kinaamriwa kusimamishwa kwa muda hadi Mmiliki atakapohakikisha anakuwa na Wafanyakazi wenye taaluma ya Uandishi wa Habari na Utangazaji ili kuleta ufanisi na tija katika vipindi vyake, pili kuhakikisha vipindi vyake vyote vinazingatia sheria, kanuni, misingi na maadili ya uandishi na utangazaji wa habari na leseni yake"

"Pia baada ya kutekeleza maelezo hayo kipindi cha Humphrey Polepole Online kitatakiwa kutoa taarifa TCRA kuwa maelekezo yote yamezingatiwa na kuwa kipindi kitarejea chini ya Uangalizi wa TCRA kwa miezi 6, haki ya kukata rufaa ipo wazi ndani ya siku 21 Kisheria kuanzia siku ya kutolewa uamuzi"
#MillardAyoUPDATES
 
Pale mchinjaji anapochinjwa. Ila tuache Mungu aitwe Mungu. Leo hii mtu ambae alikuwa na uwezo wa kusema na kufanya lolote kwenye nchi hii anapangiwa cha kusema na kufanya. Ama kweli kila kitabu na zama yake.

Walio karibu na mzee kijana wampe moyo, maana huyu jamaa kwa jitimai anaweza jinyonga na zile toilet paper zake.
 

Polepole alichelewa kujua kunyamazishana ni dhuluma.

Tumedhulumiwa sana!

Hata hivyo tuungane kupinga dhuluma.

Kumshabikia dhulumati dhidi ya yeyote haina tija yoyote kwa yeyote.
 
Mwaka mmoja nyuma Polepole hakufikiria kabisa kwamba mapito anayopitia leo angeyapitia..

Hata ungemwambia hii sheria ya TCRA ni mbovu na inaumiza raia asingekuelewa ndio kwanza angekujibu ni sheria ya kuwanyoosha wahuni...

Leo Polepole amekuwa mhuni kwa kutofuata sheria na ananyooshwa kweli kweli ndugu zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…