TCRA: Ukikutwa unatumia VPN Tanzania, faini milioni 5, kifungo mwaka mmoja

TCRA: Ukikutwa unatumia VPN Tanzania, faini milioni 5, kifungo mwaka mmoja

Wasitishe watu!... Wadhibiti kama wanaweza! Kitambulisho cha Taifa tu kimewashinda!.... Sembuse VPN!?

Wanaota!? Wanafahamu umuhimu wa VPN!?..... Kuna taarifa very classified! ....Ili uzipate ..... VPN haiepukiki....
Kama taarifa zipi mkuu
 
Mkali unaweza ukawa sahihi maana bongo hii uchaguzi ni suala nyeti sana kuliko nyeti tulizonazo. Yale yale ya Jiwe kuzima mtandao wiki mbili,, yule dingi kwenye aliko😁
Sasa ikifika muda.. hili TANGAZO litaibuliwa. Na kusema kwamba Tulitangaza mwaka 2023 mapema kabisa. Muda huo CHADEMA wapo nyuma ya nondo.
 
Badala ya kushughulikia upatikanaji wa umeme busy na vitu visivyokuwa na kuchwa wala miguu kisa Mange
😂😂😂 itakuwa wamekugusa na wewe ni miongoni mwa wanufaika wa VPN...

Sio kwa uchungu huo...🤣🤣🤣
 
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imewataka wananchi na makampuni kiujumla ambazo kwa asili ya kazi zao hawawezi kuepuka matumizi ya VPN kutoa taarifa juu ya VPN wanazotumia na taarifa muhimu kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.

Aidha mamlaka hiyo imesema iwapo itabainika umetumia VPN kinyume na kanuni zilizowekwa basi adhabu itakayotolewa kwa kosa hilo ni faini ya shillingi milioni tano, au kifungo cha mwaka au vyote kwa pamoja.

View attachment 2781209
Kuna komenti moja nilisema TCRA hawashughulikii malalamiko yetu, wao kazi yao ni kutukamata tu, mlidhani utani mnaona hii.
 
Katiba, Ibara ya 16

Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake,
maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.

===================================

HAKI YA FARAGHA kwenye katiba ipo imeandikwa lakini haitumiki, ni kama haipo. Ndio maana ni sawa hapa Tanzania polisi kukudukua na kukushitaki umemsimanga Rais kwenye simu, na ukafungwa kwa ushahidi uliopatikana kwa kuvunja katiba.

Rais Samia Suluhu alisema tuchukue miaka mitatu kwanza kusomeshana Katiba. Alikuwa sahihi kabisa, kwa saab hata yeye haijui, anaivunja kila uchwao, majaji hawaijui, viongozi hawaijui, na wananchi hatuijui.

Majaji wetu, wanasheria nguli, mawaziri wa sheria, magwidi na wakufunzi wa vyuo, wa kina Mwalimu Palamagamba Kabudi na wenzake huwa wanasemwa wamesoma nje, vyuo vizito, University of Berlin, Ujerumani na kwingineko Ulaya na Marekani. Mbona kule hivi vitu ndivyo wanavyofundishana, misingi hii ya haki kali za raia, hawa wa kwetu kule walipasije mitihani ya hao wajerumani ?????????
 
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imewataka wananchi na makampuni kiujumla ambazo kwa asili ya kazi zao hawawezi kuepuka matumizi ya VPN kutoa taarifa juu ya VPN wanazotumia na taarifa muhimu kabla ya Oktoba 30 mwaka huu.

Aidha mamlaka hiyo imesema iwapo itabainika umetumia VPN kinyume na kanuni zilizowekwa basi adhabu itakayotolewa kwa kosa hilo ni faini ya shillingi milioni tano, au kifungo cha mwaka au vyote kwa pamoja.

View attachment 2781209
AKili za ujima hizi
 
Back
Top Bottom