GE2025 TEC: Ewe Mungu, Tuma Roho wako, afanye upya uso wa Nchi kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025

GE2025 TEC: Ewe Mungu, Tuma Roho wako, afanye upya uso wa Nchi kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mimi ni mkatoliki, Father Kitima anatukwaza wengi katika ukatoliki wetu kudhani kwamba hisia zake za kisiasa zinawakilishwa na kanisa zima.

Kuiombea nchi ni kitu chema sana lakini lengo likiwa na uhusiano na siasa za kuipinga CCM kana kwamba wote makanisani tuna kadi za CHADEMA au tupo nae kihisia, kwa kweli hapo anatukosea.

Alipinga uwekezaji wa DP World bila ya kujua kwa kina ni kipi kinachokwenda kufanyika. Hivi sasa bandari inaingiza mabilioni ya pesa kwenye hazina, yeye na wote wenye mitazamo hasi wapo kimyaaa kabisa.

Alipata aibu kwa kuutafsiri vibaya mkataba na akaisoma tafsiri hiyo potofu makanisani!!, baadae ikaja kutangazwa tender ya uendelezaji wa bandari ya Bagamoyo. Ile ilikuwa ni aibu kwake na bahati nzuri kwenye nafasi za kanisa hakuna suala la kiongozi kujiuzulu, alipaswa aachie ngazi kwa kupotosha mamilioni ya wakatoliki kwa suala ambalo halielewi vyema.
Nashukuru Mkatoliki mwenzangu kwa kuliona hilo. Ashauriwe tu avue kanzu avae gwanda la khaki kama mwenzie Dr Slaa
 
Fr Kitima anahudhuria mikutano ya CHADEMA kama alivyokwenda pale MWEMBE YANGA mwaka 2024 wakati wa mkataba wa Bandari. Nieleze ni ni ukurasa gani wa Misale ya waamini unaomtuma Padre kwenda Mwembe Yanga

Unachanganya maembe na machungwa. Unapoteza kumbukumbu. Unakurupuka. Fr kitima yupi alihudhuria mwembeysnga??
 
This post is question begging. How do you know that God is not? This claim must be demonstrated to be the case with evidence provided Only then can your argument insinuating mass delusion stand
It is self evident that the omnipotent, omniscient and omnibenevolent God does not exist.

Had this God existed, prayers wouldn't even be necessary.

That God would give everybody what they need before they even knew they needed it.

The very fact that you feel the need to pray to God is confirmation that this God does not exist.
 
Mungu alisema "tuumbe mtu kwa mfano wetu.... " kwa hiyo yanayofanyika sasa yana baraka za Mungu kwa kuwa wanaofanya ni mfano wa Mungu. Ulishajiuliza vita walizopigana Israel na mauaji waliyofanya bado Mungu alikausha? Au Mungu hakuona Nazism ya Hitler? Ukoloni na biashara ya watumwa?kanisa katoliki liliua watu 70,000,000 lakini mpaka leo lipo linakenua meno. Nani hajui kwamba kanisa katoliki ndio wale waliitwa mawakala wa ukoloni (agents of colonialism)?
Ilikua ni lazima utoke pangoni ili utetee unapokulaga!!
 
Mfa maji. Kwanza nyie tunawachukia kama nini. Makafiri tunajua ni wapagani. Hakuna mkristo atakayeenda mbinguni never. Njoo uislam kabla kiama hakijawadia
Shindwa pepopunda!! Usi brainwash watu!!
 
Kuna namna Waislamu nao wanapasws kujiandaa kwa ajili ya kugawana hii nchi, ni dhahiri TEC wamedhamilia kabisa kumuonea na kumdhulumu Haki yake ya kuongoza huyu mama. Hilo liko wazi kabisa na yule polepole ni mtu wao wanayemuwezesha na kumpa jeuri ya kufanya anayofanya......kinachokera hawana sababu nyingine zaidi ya udini.
Wajiandae na nn mzee, ukiwapa tafrija za mara kwa mara huku pilau, soda na ndizi mbivu havikauki hutowaona kweny hizo hekaheka!!!
 
Kwani wanaomba kwako!! We usubiri tu. Kama Eliya peke yake aliomba mvua isinyeshe kwa miaka mitatu na akasikilizwa. Hao wacha Mungu unawajua?
Kwamba watanzania ninyi wapenda ngono, pombe na betting mna usafi gani mpk Mungu awasikilize?
 
It is self evident that the omnipotent, omniscient and omnibenevolent God does not exist.

Had this God existed, prayers wouldn't even be necessary.

That God would give everybody what they need before they even knew they needed it.

The very fact that you feel the need to pray to God is confirmation that this God does not exist.

This is not a refutation of the Theistic God Hypothesis. My philosophical defense of a petitionary prayer that I previously gave under this thread is a case in point. Revisit it.
 
This is not a refutation of the Theistic God Hypothesis. My philosophical defense of a petitionary prayer that I previously gave under this thread is a case in point. Revisit it.
If you have to pray to the omni God, the omni God does not exist.

The very need for prayer proves that that God does not exist.

It is as simple as that.

If you have to pray, the omni God does not exist.

If that God existed, prayers would not exist. Prayers would be unnecessary and unknown.

You may create a story with a fictional character called God, but outside that story, that purely fictional story, that God does not exist.
 
Ewe Mungu Wetu, Tuma Roho wako, Afanye Upya Uso wa Nchi Kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025” (Zaburi 104:30)
Kaa hyo wao kusolve ishu ni mtu kuuwawa tukiwaita wauwaji je nmkwa hyo jpm walìmuuwa wao kwa vifungu hv mlivovitoa ama kweli kondoo wanangamia kwa kukosa maarifa tena ndio ety wanajiita wamesoma wapumbavu sana hawa so akiingia rais mwengn hawaenda wanasoma ilinafe sonnchi kila mwaka ifanye uchaguz dah huko mlipopewa elimu kaulizeni tena kama hayo ndo matumizinyake
 
Kuna jitu linaenda kufa
Atakufa mtoa mada na hao akina Kitima, na hao mnaowaombea wafe kwa unafiki wenu wata survive mpaka wamalize majukumu yao. Hakuna UKATOLIKI wa kuombea mtu afe. HAKUNA, msijifanye ni WAKATOLIKI kuliko Vatican

Mungu siyo mali ya Fr Kitima na Doctor Mama Amon
 
Mfa maji. Kwanza nyie tunawachukia kama nini. Makafiri tunajua ni wapagani. Hakuna mkristo atakayeenda mbinguni never. Njoo uislam kabla kiama hakijawadia
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Aje apewe mabikra 72 siku akifa au siyo. Kobazi ni wajinga sana. Lakini imani ya mtu iheshimiwe 😂😂😂
 
Kaa hyo wao kusolve ishu ni mtu kuuwawa tukiwaita wauwaji je nmkwa hyo jpm walìmuuwa wao kwa vifungu hv mlivovitoa ama kweli kondoo wanangamia kwa kukosa maarifa tena ndio ety wanajiita wamesoma wapumbavu sana hawa so akiingia rais mwengn hawaenda wanasoma ilinafe sonnchi kila mwaka ifanye uchaguz dah huko mlipopewa elimu kaulizeni tena kama hayo ndo matumizinyake
Hivi kwanini kobazi hata kuandika tu huwa ni shida sana kwenu. Ningekuwa na mamlaka kobazi wote ningefutilia mbali
 
labda kama h
View attachment 3438148
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa.​

Sasa ni wazi kwamba Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) wameamua kushiriana na Mungu wa Haki na Amani kuufanya upya uso wa nchi ya Tanzania kwa Kutumia nyenzo ya kawaida kabisa iitwayo Misale ya Waumini, hasa Misa Namba 30 iliyoko ukurasa wa 931-932.

Kutokana na maudhui ya Misa Naomba 30, hakuna shaka kwamba kibwagizo cha Sala na Mfungo wa kuombea haki na amani siku ya tarehe 23 Agosti 2025, kinapaswa kutoka kwenye Zaburi ya 104:30 isemayo kwamba:

“Waipeleka roho yako, Ee Bwana, Wanaumbwa upya, Nawe waufanya upya uso wa nchi” (Zaburi 104:30)

Maaskofu Katoliki Tanzania kwa kushirikiana na mapadre, masista, waseminari, WAWATA, VIWAWA, UWAKA, KWAYA na Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo wanakusudia kufanya yafuatayo:

  • Watafafanua tamko kwamba "amani ni tunda la haki, usawa, ukweli, mshikamano na ustawi wa wote.”
  • Watataka “chuki ishindwe na upendo”
  • Watashawishi “kisasi kiuachie nafasi msamaha”
  • Watahimiza “ugomvi ugeuzwe kuwa urafiki.”
  • Watahamasisha "maadui warejee kwenye mazungumzano"
  • Watahanikiza "wapiganao wapeane mikono"
  • Wataomba "waliopotea wapatikane"
  • Watapaza sauti "waliotekwa wapate uhuru wao"
  • Watapiga kelele "walioumizwa wapone"
  • Watasali "waliouwawa wapate uzima wa milele"
  • Watakemea "uovu ukome katika nchi yetu"
Mipango hii imetajwa Katika barua ya tarehe 05 Agosti 2025, kutoka Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, na kufafanukiwa katika barua ya tarehe 8 Agosti 2025 yenye kubeba maagizo ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar Es Salamaam, Jude Thaddeus Ruwaichi.

Sekretarieti ya TWC imetoa mwongozo wa kitaifa, wenye rejea namba TEC/P/05/08/25 05/08/2025, kuhusu utaratibu wa kutekeleza “Ratiba ya Mfungo Kuomba Haki na Amani Nchini Tarehe 23 Agosti 2025.”

Mwongozo huo ni sehemu ya utekekezaji wa maagizo ya Maaskofu Katoliki kupitia Barua Yao ya tarehe 19 Juni 2025.

Barua hiyo ilitoa wito wa kuandaliwa kwa siku maalum ya “sala na mfungo” kwa ajili ya kuombea “amani” ambayo ni “tunda” la “haki, usawa, ukweli, mshikamano na ustawi wa wote.”

Kila Jimbo litajipangia utaratibu wake wa kutekeleza wito wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, kama ambavyo tayari Jimbo Kuu la Dar Es Salaam limefanya.

Lakini mwongozo wa Sekretarieti ya TEC unatoa mapendekezo ya kitaifa yatakayotumika katika kuiadhimisha siku hii maalum kwa sala na mfungo.

Mwongozo huo kutoka Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, umesainiwa na Padre Alister Makubi, Mkurugenzi Wa Uchungaji wa TEC.

Viongozi wote wa Kanisa Katyoliki nchi nzima wanaagizwa kutekeleza mkakati wa Kanisa Katoliki wa kuombea Haki na Amani kwa kutumia mwongozo wa “Misa Namba 30.”

Misa hii inapatikana kwenye kitabu kinachoitwa “Misale ya Waumini,” au tusema “Misale ya Kiroma,” ukurasa wa 931-932.

Kurasa hizi ndizo zinabeba ujumbe rasmi wa Kanisa Katoliki kwa Waumini wote na Taifa kwa Ujumla.

Ujumbe huu umetapaa kwenye salama kadhaa zikiwemo cifuatazo:

  • Sala ya kuanza ibada,
  • Sala ya kuombea dhabihu,
  • Sala ya Ekaristi ya Upatanisho,
  • Wimbo wa Komunyo
  • Sala baada ya Komunyo, na
  • Sala ya Kuiombea Tanzania.


Sala ya kuanza ibada inabeba maneno yanayomwomba Mungu, awape “amani” wamngojao na ukatuongoze “kwenye nijia ya haki”; kwamba, kwa vile amefunua kwamba “wapatanishi wataitwa wana wa Mungu,” basi asiache mwaka huu upite bila ahadi hii kutumia.

Aidha, Sala ya kuanza ibada inabeba maneno yanayomwomba Mungu atujalie uwezo wa kuimarisha “bila kukoma haki ile ambayo peke yake inaleta kwa uhakika amani ya kudumu na ya kweli”; kwamba, kwa vile anawashughulikia “watu wote kwa wema,” basi awe “radhi kuwajalia wanadamu” aliowapa “chimbuko moja wawe familia moja yenye amani’; na kwamba watu wote “waunganishwe daima kwa roho ya udugu.”

Sala ya kuombea dhabihu inabeba maneno yanayosema kwamba, sadaka ya Misa Takatifu “ambayo inatolewa kwa ishara hizi za sakramenti zinazoonyesha amani na umoja, ifae kwa kazi ya kuimarisha uelewano kati ya wana” wake wote.

Sala ya Ekaristi ya Upatanisho inabeba maneno yanayosema kwamba, “japo familia ya wanadamu imefarakana na kutengana kwa fitina, tumefahamu na kutambua kwamba wewe unaweza kulegeza mioyo, ili watu wawe tayari kupatanishwa”.

Aidha, Sala ya Ekaristi ya Upatanisho inabeba maneno yanayosema kwamba, Mungu ana uwezo wa kuishawishi “mioyo ya watu, ili maadui warejee kwenye mazungumzano, wapiganao wapeane mikono, na mataifa watafute njia ya kukutana kwa amani”; na kwamba, kwa sababu hii, basi, “chuki ishindwe na upendo, kisasi kiuachie nafasi msamaha, na ugomvi ugeuzwe kuwa urafiki.”

Wimbo wa Komunyo unabeba maneno yenye ujumbe kwamba “Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu (Mt 5:9)” na kwamba “Amani nawaachieni, amani yangu nawapa, asema Bwana (Yn 14:27).”

Na sala baada ya komunyo inabeba maneno yasemayo kwamba, “tunakuomba utujalie roho ya mapendo,” ili kwa sababhu hiyo “tustawishe kwa ufanisi kati ya wote ile amani ambayo wewe mwenyewe umetuachia.”

View attachment 3438159

Padre Kitima, Katibu Mkuu wa TEC​

Ratiba ya Sala na Mfungo

Kwa mujibu wa ratiba ilyotangazwa, Jumuiya zote za Kitume ndani ya Kanisa katoliki zinatakiwa kushiriki kikamilifu. Kuna Kwaya, Viwawa, Uwaka, Wawata na Jumuiya Ndogo Ndogo. Mgawanyo wa majukumu ni kama ifuatavyo:

SAA 2:00—03:00 Asubuhi: Kutakuwepo na matukio mawili.

  • Kwanza ni Misa Takatifu ya ufunguzi “kwa ajili ya kudumisha amani na haki.”
  • Misa hii inapaswa kufanyika kwa kuzingatia utaratibu wa “Misa namba 30,” unaopatikana kwenye kitabu cha Misale ya Kiroma, ukurasa wa 931-932.
  • Kisha litakuwepo tukio la “Kuabudu Ekaristi Takatifu” lengo lake likiwa ni “kuabudu, kuikabidhi nchi yetu ya Tanzania Kwa Mungu.”
SAA 3:00—5:00 Asubuhi: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani:
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu”; na
  • “Maungamo”; na “Mafundisho ya Biblia.”
  • Matukio haya yatakayoongozwa na “Makatekista na Watumikizi.”
SAA 5:00—7:00 Mchana: Kutakuwepo na matukio manne, yaani:
  • “Kuabudu kwa Watoto,” somo kuu likiwa ni “Yesu rafiki wa watoto”;
  • “Sala ya Kuombea haki na amani nchi yetu na nyimbo”; na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu”; na “Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Utoto Mtakatifu na Walezi Wao.”
SAA 7:00—9:00 Mchana: Kutakuwepo na matukio manne, yaani
  • “Sala ya Malaika wa Bwana na Rozari Ya Huruma ya Mungu,”
  • “Nyimbo za kusifu na kuabudu Ekaristi Takatifu,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu;” na
  • “Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “KWAYA.”
SAA 9:00 Alasiri—11:00 Jioni: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani
  • “Neno la Mungu na Litania ya Bikira Maria”;
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu” na
  • “Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Vijana Wafanyakazi Wakatoliki-VIWAWA.”
SAA 11:00 — 12:00 Jioni: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
  • “Tafakari ya Neno la Mungu”;
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu,”
  • “Maungamo”; na
  • “Litania ya Moyo Mt. wa Yesu.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Umoja wa Wanaume Katoliki -UWAKA.”
SAA 12:00 — 2:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Rozari Takatifu,”
  • “Litania ya Bikira Maria”; na
  • “Ukimya na Maungamo.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Wanawake Wakatoliki Tanzania-WAWATA.”
SAA 2:00 — 4:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
  • “Mafundisho juu ya Huruma ya Mungu,”
  • “Litania ya huruma ya Mungu,”
  • “Tafakari ya mateso ya Kristo,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.
  • Matukio haya yataongozwa na “Watawa, Waseminari na Mapadre.”
SAA 4:00 — 6:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Ukimya na Sala za Kibinafsi,”
  • “Nyimbo za Kusifu na kuabudu Ekaristi Takatifu,” na
  • “Maombi binafsi.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Kwanza.
SAA 6:00 — 8:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Neno la Mungu na Litania ya Bikira Maria,”
  • “Litania ya Jina Takatifu la Yesu,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Pili.
SAA 8:00 — 10:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
  • “Ukimya na Kuimba Nyimbo za Ekaristi Takatifu,”
  • “Neno la Mungu na Litania ya Huruma ya Mungu,” na
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.”
  • Matukio haya yataongozwa na Jumuiya za “Moyo Mtakatifu Wa Yesu Na Karismatiki Katoliki.”
SAA 10:00 — 12:00 Asubuhi: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
  • “Neno la Mungu,”
  • “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu,”
  • “Rozari Takatifu na Litania ya Bikira Maria,” na
  • “Sala ya asubuhi na Maandalizi ya Misa.”
  • Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Tatu.
SAA 1:30 — 3:30 Asubuhi: Kutakuwepo na tukio moja pekee, yaani,
  • “Misa Takatifu ya Kufunga.”
  • Kwa mujibu wa mwongozo, “siku ya kuhitimisha itaadhimishwa Misa ya Dominika” lakini lazima iwekwe nia ya “kumshukuru Mungu kwa siku hii ya Mfungo na Sala.”

Kwa sababu ya ubora wa ratiba hii, ni wazi kwamba, mafungo haya yanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kugeuza nyoyo za waumini katika msimu huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Na hapa tusisahau kwamba, sala ni wajibu wa kila Mkristo. Maana tunasoma kwamba, "Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtakaribishwa" (Luka 11:9)
Hivyo, sasa ni wazi kwamba Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limeamua kufuata nyayo za Mtakatifu Fransis wa Assiz, Mwalimi Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania, pamoja na Papa Yohane Paulo II, kuhusu ajenda ya kudumu ya kupigania haki na amani.

Katika sala yake ya kuombea haki na amani, Mtakatifu Fransis (1182–1226), mzaliwa wa Italia, anamwomba Mungu amfanye “chombo cha amani” ili aweze kugeuza chuki kuwa upendo, majeraha kuwa msamaha, mashaka kuwa imani, kukata tamaa kuwa matumaini, giza kuwa nuru, na huzuni kuwa furaha.

Mwalimu Nyerere, mwaka 1961, alizindua Mwenge wa uhuru ili autumie kama alama inayoonekana kuwakilisha ndoto yake ya “kugeuza giza la dhuluma kuwa nuru ya haki” katika Taifa jipya.

Naye Papa Yohane Paulo II, wakati wa ziara zake nchini Poland za mwaka 1979 hadi 1989, alitumia kaulimbiua iliyobeba maneno ya Mzaburi kufanikisha ajenda ya “kuufanya upya uso wa nchi” kwa kuhubiri haki na amani nchini humo.

Mkakati wake ulianzia kwenye maneno ya Zaburi yasemayo kwamba, “
Waipeleka Roho yako Ee Mungu, nawe waufanya upya uso wa nchi.” (Zaburi 104:30).

Huu ndio ujumbe unaosindikiza Mafungo ya Kanisa katoliki kwa ajili ya “Kuomba Haki na Amani” nchini Tanzania utakaohitimishwa tarehe 23 Agosti 2025.

Kwa ufupi, tunaweza kusema kwamba, TEC wanatembea katika nyayo zote hizi.


View attachment 3438173
Padre Makubi (kushoto) ​
Labda kama huyo Mungu ni wao pekeyao.

Hata hivyo alama ya ulawiti wa watoto wadogo, dhuluma za kingono na kutekeleza watoto mitaani baada ya kupiga mimba na kutekeleza wasichana wa watu inabaki kua alama na sura pekee ya kanisa katoliki duniani, hayo mengine ya tec na Askofu pisa ni unafiki mtupu 🐒
 
Back
Top Bottom