Ujumbe wa TEC Siku ya tarehe 23 Agosti 2025: “Ewe Mungu Wetu, Tuma Roho wako, Afanye Upya Uso wa Nchi Kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025” (Zaburi 104:30)
- Wameandaa Sala na Mafungo ya kuombea haki na amani nchini
- Watataka “chuki ishindwe na upendo”
- Watashawishi “kisasi kiuachie nafasi msamaha”
- Watahimiza “ugomvi ugeuzwe kuwa urafiki.”
- Watahamasisha "maadui warejee kwenye mazungumzano"
- Watahanukiza "wapiganao wapeane mikono"
Sasa ni wazi kwamba Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania limeamua kufuata nyayo za Mtakatifu Fransis wa Assiz, Mwalimi Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa la Tanzania, pamoja na Papa Yohane Paulo II, kuhusu ajenda ya kudumu ya kupigania haki na amani.
Katika sala yake ya kuombea haki na amani, Mtakatifu Fransis (1182–1226), mzaliwa wa Italia, anamwomba Mungu amfanye “chombo cha amani” ili aweze kugeuza chuki kuwa upendo, majeraha kuwa msamaha, mashaka kuwa imani, kukata tamaa kuwa matumaini, giza kuwa nuru, na huzuni kuwa furaha.
Mwalimu Nyerere, mwaka 1961, alizindua Mwenye wa uhuru ili alama inayoonekana kuhusu ndoto yake ya “kugeuza giza la dhuluma kuwa nuru ya haki” katika Tanzania mpya.
Huu ndio ujumbe unaosindikiza Mafungo ya Kanisa katoliki kwa ajili ya “Kuomba Haki na Amani” nchini Tanzania utakaohitimishwa tarehe 23 Agosti 2025.
Naye Papa Yohane Paulo II, wakati wa ziara zake nchini Poland za mwaka 1979 hadi 1989, alitumia kaulimbiua iliyobeba maneno ya Mzaburi kufanikisha ajenda ya “kuufanya upya uso wa nchi” kwa kuhubiri haki na amani nchini humo. Mkakati wake ulianzia kwenye maneno ya Zaburi yasemayo kwamba, “Waipeleka Roho yako Ee Mungu, nawe waufanya upya uso wa nchi.” (Zaburi 104:30).
Tunaweza kusema kwamba, TEC wanatembea katika nyayo hizi. Tarehe 08 Agosti 2025, Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, yenye Makao yake Makuu Jijini Dar es Salaam, imetoa mwongozo wa kitaifa, wenye rejea namba TEC/P/05/08/25 05/08/2025, kuhusu utaratibu wa kutekeleza ratiba ya “Ratiba ya Mfungo Kuomba Haki na Amani Nchini Tarehe 23 Agosti 2025.”
Mwogozo huo unatokana na Barua ya Maaskofu Katoliki ya tarehe 19 Juni 2025 iliyotoa wito wa kuandaliwa kwa siku maalum ya “sala na mfungo” kwa ajili ya kuombea “amani” ambayo ni “tunda” la “haki, usawa, ukweli, mshikamano na ustawi wa wote.”
Pamoja na utaratibu ambao kila Jimbo litajipangia katika kutekeleza wito huo, mwongozo wa sasa unatoa mapendekezo ya kitaifa yatakayotumika kama utaratibu wa kuiadhimisha siku hii maalum kwa sala na mfungo.
Mwongozo huo kutoka Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, umesainiwa na Padre Alister Makubi, Mkurugenzi Wa Uchungaji wa TEC.
Padre Makubi amewaagiza viongozi wa Kanisa Katyoliki nchi nzima kutekeleza mkakati wa Kanisa Katoliki wa kuombea Haki na Amani kwa kutumia mwongozo wa “Misa Namba 30.”
Misa hii inapatikana kwenye kitabu kinachoitwa “Misale ya Waumini,” zu tusema “Misale ya Kiroma,” ukurasa wa 931-932.
Kurasa hizi ndizo zinabeba ujumbe rasmi wa Kanisa Katoliki kwa Waumini wote na Taifa kwa Ujumla. Ujumbe hii umetapaa kwenye salama kadhaa zikiwemo cifuatazo:
- Sala ya kuanza ibada,
- Sala ya kuombea dhabihu,
- Sala ya Ekaristi ya Upatanisho,
- Wimbo wa Komunyo na
- Sala baada ya Komunyo.
Sala ya kuanza ibada inabeba maneno yanayomwomba Mungu, awape “amani” wamngojao na ukatuongoze “kwenye nijia ya haki”; kwamba, kwa vile amefunua kwamba “wapatanishi wataitwa wana wa Mungu,” basi asiache mwaka huu upite bila ahadi hii kutumia.
Aidha, Sala ya kuanza ibada inabeba maneno yanayomwomba Mungu atujalie uwezo wa kuimarisha “bila kukoma haki ile ambayo peke yake inaleta kwa uhakika amani ya kudumu na ya kweli”; kwamba, kwa vile anawashughulikia “watu wote kwa wema,” basi awe “radhi kuwajalia wanadamu” aliowapa “chimbuko moja wawe familia moja yenye amani’; na kwamba watu wote “waunganishwe daima kwa roho ya udugu.”
Sala ya kuombea dhabihu inabeba maneno yanayosema kwamba, sadaka ya Misa Takatifu “ambayo inatolewa kwa ishara hizi za sakramenti zinazoonyesha amani na umoja, ifae kwa kazi ya kuimarisha uelewano kati ya wana” wake wote.
Sala ya Ekaristi ya Upatanisho inabeba maneno yanayosema kwamba, “japo familia ya wanadamu imefarakana na kutengana kwa fitina, tumefahamu na kutambua kwamba wewe unaweza kulegeza mioyo, ili watu wawe tayari kupatanishwa”.
Aidha, Sala ya Ekaristi ya Upatanisho inabeba maneno yanayosema kwamba, Mungu ana uwezo wa kuishawishi “mioyo ya watu, ili maadui warejee kwenye mazungumzano, wapiganao wapeane mikono, na mataifa watafute njia ya kukutana kwa amani”; na kwamba, kwa sababu hii, basi, “chuki ishindwe na upendo, kisasi kiuachie nafasi msamaha, na ugomvi ugeuzwe kuwa urafiki.”
Wimbo wa Komunyo unabeba maneno yenye ujumbe kwamba “Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu (Mt 5:9)” na kwamba “Amani nawaachieni, amani yangu nawapa, asema Bwana (Yn 14:27).”
Na sala baada ya komunyo inabeba maneno yasemayo kwamba, “tunakuomba utujalie roho ya mapendo,” ili kwa sababhu hiyo “tustawishe kwa ufanisi kati ya wote ile amani ambayo wewe mwenyewe umetuachia.”
Ratiba ya Sala na Mfungo
SAA 2:00—03:00 Asubuhi: Kutakuwepo na matukio mawili.
- Kwanza ni Misa Takatifu ya ufunguzi “kwa ajili ya kudumisha amani na haki.”
- Misa hii inapaswa kufanyika kwa kuzingatia utaratibu wa “Misa namba 30,” unaopatikana kwenye kitabu cha Misale ya Kiroma, ukurasa wa 931-932.
- Kisha litakuwepo tukio la “Kuabudu Ekaristi Takatifu” lengo lake likiwa ni “kuabudu, kuikabidhi nchi yetu ya Tanzania Kwa Mungu.”
SAA 3:00—5:00 Asubuhi: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani:
- “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu”; na
- “Maungamo”; na “Mafundisho ya Biblia.”
- Matukio haya yatakayoongozwa na “Makatekista na Watumikizi.”
SAA 5:00—7:00 Mchana: Kutakuwepo na matukio manne, yaani:
- “Kuabudu kwa Watoto,” somo kuu likiwa ni “Yesu rafiki wa watoto”;
- “Sala ya Kuombea haki na amani nchi yetu na nyimbo”; na
- “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu”; na “Maungamo.”
- Matukio haya yataongozwa na “Utoto Mtakatifu na Walezi Wao.”
SAA 7:00—9:00 Mchana: Kutakuwepo na matukio manne, yaani
- “Sala ya Malaika wa Bwana na Rozari Ya Huruma ya Mungu,”
- “Nyimbo za kusifu na kuabudu Ekaristi Takatifu,” na
- “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu;” na
- “Maungamo.”
- Matukio haya yataongozwa na “KWAYA.”
SAA 9:00 Alasiri—11:00 Jioni: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani
- “Neno la Mungu na Litania ya Bikira Maria”;
- “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu” na
- “Maungamo.”
- Matukio haya yataongozwa na “Vijana Wafanyakazi Wakatoliki-VIWAWA.”
SAA 11:00 — 12:00 Jioni: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
- “Tafakari ya Neno la Mungu”;
- “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu,”
- “Maungamo”; na
- “Litania ya Moyo Mt. wa Yesu.”
- Matukio haya yataongozwa na “Umoja wa Wanaume Katoliki -UWAKA.”
SAA 12:00 — 2:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
- “Rozari Takatifu,”
- “Litania ya Bikira Maria”; na
- “Ukimya na Maungamo.”
- Matukio haya yataongozwa na “Wanawake Wakatoliki Tanzania-WAWATA.”
SAA 2:00 — 4:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
- “Mafundisho juu ya Huruma ya Mungu,”
- “Litania ya huruma ya Mungu,”
- “Tafakari ya mateso ya Kristo,” na
- “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.
- Matukio haya yataongozwa na “Watawa, Waseminari na Mapadre.”
SAA 4:00 — 6:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
- “Ukimya na Sala za Kibinafsi,”
- “Nyimbo za Kusifu na kuabudu Ekaristi Takatifu,” na
- “Maombi binafsi.”
- Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Kwanza.
SAA 6:00 — 8:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
- “Neno la Mungu na Litania ya Bikira Maria,”
- “Litania ya Jina Takatifu la Yesu,” na
- “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.”
- Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Pili.
SAA 8:00 — 10:00 Usiku: Kutakuwepo na matukio matatu, yaani,
- “Ukimya na Kuimba Nyimbo za Ekaristi Takatifu,”
- “Neno la Mungu na Litania ya Huruma ya Mungu,” na
- “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu.”
- Matukio haya yataongozwa na Jumuiya za “Moyo Mtakatifu Wa Yesu Na Karismatiki Katoliki.”
SAA 10:00 — 12:00 Asubuhi: Kutakuwepo na matukio manne, yaani,
- “Neno la Mungu,”
- “Kipindi cha kimya binafsi mbele ya Ekaristi Takatifu,”
- “Rozari Takatifu na Litania ya Bikira Maria,” na
- “Sala ya asubuhi na Maandalizi ya Misa.”
- Matukio haya yataongozwa na “Jumuiya Ndogo Ndogo –JNNK,” Kundi la Tatu.
SAA 1:30 — 3:30 Asubuhi: Kutakuwepo na tukio moja pekee, yaani,
- “Misa Takatifu ya Kufunga.”
- Kwa mujibu wa mwongozo, “siku ya kuhitimisha itaadhimishwa Misa ya Dominika” lakini lazima iwekwe nia ya “kumshukuru Mungu kwa siku hii ya Mfungo na Sala.”
Jumuiya zote za Kitume ndani ya Kanisa katoliki zinatakiwa kushiriki kikamilifu. Kuna Kwaya, Viwawa, Uwaka, Wawata na Jumuiya Ndogo Ndogo.
Kwa sababu hii, ni wazi kwamba, mafungo haya yanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kugeuza nyoyo za waumini katika msimu huu wa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Na hapa tusisahau kwamba, sala ni wajibu wa kila Mkristo. Maana tunasoma kwamba, "Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtakaribishwa" (Luka 11:9)
Huyo Mungu wanayemuamini Wakristo na wengi wengine, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, angekuwapo kweli, kusingekuwa na haja ya kumuomba kitu.
Angewapa viumbe wake mazuri yote wanayohitaji bila kuombwa, kungekuwa hakuna haja ya kuomba chochote. Na mengine yasiyofaa kuombwa watu wasingejua hata kuwa na tamaa ya kuyaomba.
Ukiona mtu anaomba Mungu tu, huo ni ushahidi Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Kama kuna kazi ya kuifanya kuondoa watawala dhalimu, au kubadilisha mifumo, ifanyieni kazi nyie wenyewe msimtegee Mungu ambaye hayupo awafanyie kazi mnayotakiwa kuifanya nyie wenyewe.
Watawala dhalimu wakisikia mnaishia kuomba Mungu wanafurahi sana kwa sababu wanajua habari ya Mungu ni silaha ya kuwapumbaza watu wasipiganie chao wamuachie Mungu awasaidie.
Kuomba Mungu badala ya kufanya kazi unayotakiwa kufanya wewe mwenyewe ni ku abdicate responsibilities.