GE2025 TEC: Ewe Mungu, Tuma Roho wako, afanye upya uso wa Nchi kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Sina dini lakin ntashiriki maombi
 
Ewe Mungu Wetu, Tuma Roho wako, Afanye Upya Uso wa Nchi Kabla ya Uchaguzi Mkuu 2025” (Zaburi 104:30)

Ewe Mungu futa laana katika taifa lako takatifu katika pembe kuu nane za dunia ,na imekua
 
Uzuri ni kwamba siku hizi Mungu hachelewi kujibu, yuko fasta sana
NEGATIVITY!....(Hekima za kimungu ziwaongoze katika kuitenda haki),nchi yetu ni ya utulivu,haki na usawa,kuna wasiopenda utulivu tulio nao,nao wamejawa na nongwa,mungu wetu ndiye mlinzi wetu,na ndiye amani yetu!.(Some sort, novena like,imekasoro idadi tu ya siku!)
 
🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮
 
OLE WAKE MWANANCHI ATAKAYE ENDA KUPIGA KURA
OLE WAKE MWALIMU ATAKAYE ENDA KUPIGA KURA
OLE WAKE MGAMBO ATAKAYE ENDA KUPIGA KURA

No reforms no election
 
Huyo Mungu wanayemuamini Wakristo na wengi wengine, mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, angekuwapo kweli, kusingekuwa na haja ya kumuomba kitu.

Angewapa viumbe wake mazuri yote wanayohitaji bila kuombwa, kungekuwa hakuna haja ya kuomba chochote. Na mengine yasiyofaa kuombwa watu wasingejua hata kuwa na tamaa ya kuyaomba.

Ukiona mtu anaomba Mungu tu, huo ni ushahidi Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Kama kuna kazi ya kuifanya kuondoa watawala dhalimu, au kubadilisha mifumo, ifanyieni kazi nyie wenyewe msimtegee Mungu ambaye hayupo awafanyie kazi mnayotakiwa kuifanya nyie wenyewe.

Watawala dhalimu wakisikia mnaishia kuomba Mungu wanafurahi sana kwa sababu wanajua habari ya Mungu ni silaha ya kuwapumbaza watu wasipiganie chao wamuachie Mungu awasaidie.

Kuomba Mungu badala ya kufanya kazi unayotakiwa kufanya wewe mwenyewe ni ku abdicate responsibilities.
 
Nyerere mwenyewe wahuni walimla kichwa na aliliwa kichwa sababu waliona misimamo yake inawachelewesha.
Kweli aliliwa kichwa na wahuni eti yeye aliekua nje akiwapigania wakina Mandela ndio kapotea faster ila wahuni sio watu.
 
Kweli aliliwa kichwa na wahuni eti yeye aliekua nje akiwapigania wakina Mandela ndio kapotea faster ila wahuni sio watu.
Yule Mzee alikosea kuwasidia jirani huku analeta deni nyumbani,sababa mjane anasema kaamua kuanika deni lote huenda ni la Nyerere pia likifichwa
 
Yule Mzee alikosea kuwasidia jirani huku analeta deni nyumbani,sababa mjane anasema kaamua kuanika deni lote huenda ni la Nyerere pia likifichwa
Alitumia pesa nyingi kuwasaidia watu wasiokua na fadhila kama SA,Mozambique na Angola hakuna watu huko na hata hawapendi kuzungumzia msaada wetu kwao nakumbuka Mandela nchi yake ya kwanza kwenda kutembelea ilikua Tanzania aliamini ni Nchi iliyoendelea kweli alikutana na vumbi la balaa kwenye Uwanja wa uhuru hapo Mkalimani alikua Mzee Kikwete na alisema akutegetemea kuikuta Tanzania katika hali ile na msaada mkubwa iliyokua inatoa...
 
Mambo mengine hata Mungu kachoka kutusikiliza ..tupige shortcut .asiingie mtu ofisni anayejiita Rais kuanzia 30th October
 
Mambo mengine hata Mungu kachoka kutusikiliza ..tupige shortcut .asiingie mtu ofisni anayejiita Rais kuanzia 30th October
Mungu ni chaka la kutupia mambo ambayo watu wavivu hawataki kuyafanyia kazi, au watu wajinga hawajui wayatatue vipi.

Kiuhalisia Mungu hayupo. Ni hadithi tunajipigia wenyewe kujizuga tu.

Kama kuna kazi ya kufanya, ifanye mwenyewe, usimtegemee Mungu.
 
Huenda hujaelewa madhumuni ya mafungo haya. Ni kuombea haki na amani katika nchi yetu kuelekea uchaguzi wa Oktoba 2025.

Kwani SSH hapendi haki na amani? Haya maombi ni kwa ajili ya nchi, wala si laana kwa mtu. Lakini kama kuna mtu yupo upande wa muovu shetani, ni dhahiri hatapendezwa na jambo hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…