Tegemea hili kutokea juu ya Tundu Lissu hivi punde

Tegemea hili kutokea juu ya Tundu Lissu hivi punde

Katika vitu ambavyo mama nampenda ni kuwa ana Imani sana na Mungu na pia ni muumini sana na dini yake. Kwa hapo Mungu azidi kumpigania Rais wetu azidi kumpa afya njema na busala iliyotukuka.Pili Rais wetu ana nia njema na nchi yetu, sema Kuna uharaka sana wa kibadirisha hizo Sheria. Lakini tumpe muda Rais wetu ninaamini hili swala Mama yetu atalifanya kwa sababu ni muumini sana wa dini.Kwa sasa muda wa No reform no election ni mdogo sana. Tukisema tupambane sana hamna Rais mwingine atakaye fanikisha hili jambo. Tumuache Mama uchakuzi uishe. Mama atarekebisha kila kitu. Pia tukumbuke kuwa harakq harakq Haina baraka.
Pambana na kata yako kwanza we mzee... Mwaka huu wanakutoa
 
Serikali haiwezi kumdhuru lissu pamoja na madhaifu yake ya kidemokrasia ila LISU atakuwa salama ila kama kutatokea wajinga watakaotaka kuichomea serikali petrol basi akidhuriwa LISU serikali itashuhudia umwagaji mkubwa sana wa damu Toka tupate uhuru hivyo ushauri wangu serikali imlinde LISU kama bank kuu basi.
 
LISU Yuko salama mikononi mwa assets zenye heshima za serikali mfano Ile Tiss ya juu sio Hawa chawa wa uvccm -tiss
 
Ngoja kwanza, sisi tunasubiri jamaa apigwe kitanzi imekuwaje?

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni Mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele.
Israel naye na aseme sasa

Mlango warumi na waseme fadhili za BWANA ni za milele
 
Hao wako mbali sana mmoja tabora mwingine bukoba
Kwamba inashindikana kuwatumia ndege za dharura za serikali in a flash of an eye acha ushamba dogo. Serikali Ina ndege zisizopungua kumi ambazo ziko full alert kwa dharura yeyote ya kitaifa.
 
Congratulations gentleman,
upotoshaji at it's best wakati mahabusu akiinjoy mandhari nyingine mpya ya korokoroni katika gereza la ukonga kulingana na mahitaji ya physical condition ya mshukiwa 🐒
Physical condition kwa kiswahili ndio "vyuma vimekaza"?
 
Juzi nilipost mambo Saba yatakayotokea kueleka UCHAGUZI MKUU 2025 na jambo la kwanza nilisema Mh. Tundu A. Lissu ataachiwa kabla ya mwezi Juni kuisha.

Leo zimezuka taarifa kuwa Mh. Tundu Lissu ametolewa gerezani Keko na kupelekwa kusikojulikana. Nilikuwa nasubiria kujilizisha kutoka Deep source zangu Kuanzia tukio la Mh. Freeman Mbowe kumtembelea Hadi tukio la leo hii kutolewa Keko Kwa msafara maalumu.

Ukweli kutoka chanzo chá ndani kabisa ni kwamba Mh. Tundu Lissu ni Kweli alitolewa Keko majira kati ya saa 5:38 aSbh Hadi saa 6:10 kwa order toka Juu na kupelekwa sehemu kwajili ya negotiation na viongozi kadhaa wakuu katika nchi juu ya REFORMS NA UCHAGUZI MKUU KUIRUDISHA CHADEMA ULINGONI. Mazungumzo ya leo yamekuja baada ya mazungumzo ya awali na mwenyekiti aliyepita ambaye alikuwa Messenger wa Kile ambacho kilitarajiwa kuzungumzwa leo na MSIMAMO WA TUNDU LISSU umebaki Ule Ule kuwa NO REFORMS NO ELECTION AND BETTER TO DIE.... OVER MY DEAD BODY I WON'T COMPROMISE MY STATUS.

Taarifa toka ndani zinaeleza kuwa kikao cha leo kilihuzuliwa na viongozi kadhaa wa kidini wenye nguvu ya ushawishi Lakini Bado msimamo wa Lissu ni Ule Ule.

Kuna pressure kubwa sana kutoka upande wa gavoo na tutarajie Kuona kauli za mawaziri na viongozi wa CHAMA kuendelea kuitetea serikali Kwa kisingizio cha MUDA WA REFORMS HAUPO ILA TUNA AHIDI UCHAGUZI HURU KWELI KWELI

Mh. Tundu Lissu Yupo sehemu salama na atarudishwa Keko Kwajili ya kupanda kizimbani Tarehe 24. Japo Pia Kuna uwezekano wa kuhamishiwa Ukonga. Kitu pekee chakumfanya ni watanzania waendelee kuomba Wale chawa wasije Fanya Sifa kinyume na maagizo ya Mh. Rais na wakamdhuru. MWENYE NCHI HANA AJENDA YA KUMTENDEA UBAYA TUNDU LISSU JAPO VIBARAKA NDIO WANAOSHINIKIZA SANA ILA KAULI YA MWENYE NCHI NI HAPANA.
View attachment 3308605
Mkuu upo sawa. Hapo alipo kama asipotoka ni kifo na akitoka ndani anatoka na no reform no election
 
Back
Top Bottom