Tegeta, Dar: Maafisa wa TRA washambuliwa na wananchi kwa mawe

Tegeta, Dar: Maafisa wa TRA washambuliwa na wananchi kwa mawe

View attachment 3170006View attachment 3170007

Maeneo ya Tegeta kwa Ndevu jijini Dar, Watu waliojitambulisha kuwa ni maafisa wa TRA wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Landcruizer, wameblock gari binafsi aina ya BMW X6 yenye namba za usajili T 229 DHZ na kumtaka dereva ashuke wanamhitaji.

Dereva wa BMW amegoma kushuka na kuamua kufunga vioo na milango yote. Kwa kuwa gari lililodaiwa ni la TRA lilikua limemblock ulitokea msongamano mkubwa eneo hilo. Dereva wa BMW alipiga kelele kuwa watu hao wanataka kumteka, ndipo wananchi walipoanza kuishambilia kwa mawe gari hiyo iliyodaiwa kuwa ni ya TRA.

Walipoona mawe yamezidi wakaamua kunusuru roho zao kwa kukimbia lakini inasemekana wamegonga mtoto mdogo. Hali hiyo imezidisha hasira kwa wananchi ambao wameendelea kuishambulia gari hiyo kwa mawe na kujeruhi waliomo ndani hadi Polisi walipofiia kuwanusuru.

Inadaiwa kumetoka vifo katika tukio hilo, japo bado haijathibitishwa.!
Wangeitia moto hiyo gari blood mazaf@kaz
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeeleza masikitiko yake na kuutarifu umma kuhusiana na gari yake yenye namba za usajili STL 9923 ikiwa na watumishi watatu (3) ndani yake waliokuwa kwenye doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo ya magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za forodha na kutolipiwa ushuru imeshambuliwa imeshambuliwa na watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam usiku wa Desemba 05.2024

Taarifa ya TRA iliyotolewa kupitia Idara ya Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano imebainisha kuwa kadhia hiyo imekuja baada ya watumishi wa mamlaka hiyo kubaini kwamba gari yenye namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ambayo inadaiwa kuingizwa nchini kinyemela bila kulipiwa kodi za serikali stahiki na kwa mujibu wa sheria, hivyo kuifuatilia kwa lengo la kuikamata na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa, wakati watumishi hao wa TRA wanaendelea kutimiza wajibu wao walihusishwa na vitendo vya utekaji, hatua iliyopelekea wao na gari walilokuwa wanatumia kushambuliwa

"Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatoa pole kwa watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao, pamoja na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii, na kuwaombea wapone haraka" -TRA

Katika hatua nyingine, mamlaka hiyo imeuhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.
1733461593619.png
 
Najaribu kuwaza kama hao jamaa wa the so called TRA walikuwa kwenye magumashi yao binafsi, kesho wanaeleza nn ofisi gari kuvunjwa vioo na wao kujeruhiwa 😂😂.
Bila police escort ni kwamba ilikuwa mishe yao binafsi ya upigaji, ofisini lazima kinuke japo huwa wanayamaliza kiaina kwani hakuna msafi among them all.
Possibility nyingine inaweza kuwa ni 'wasiojulikana' sasa baada ya mission kuzuiwa na raia wema wamekuwa spin-crafters hivyo basi kwa kuwa walimlenga mmiliki wa X6 ndiyo twist yao wanahadaa umma kuwa ilikuwa ni operation ya TRA.
My thinking ni kati ya hayo mawili.
 
Gari ya serikali namba STL 9923, Usiku huu imeshambuliwa kwa mawe na wananchi wenye hasira butu, na watumishi waliokuwemo ndani wameumizwa.

Chanzo cha kizaa zaa hicho inasemekana hilo gari la serikali lilikua linaifuatilia gari nyingine ndogo aina ya BMW.

Baada ya kufika maeneo ya tegeta kwa ndevu, ile gari ya serikali ika buloku ile BMW.

Wananchi walipotaka kujua kulikoni, maana stori za utekaji zimekua nyingi, jamaa wakajitetea wao ni watumishi wa serikali kitengo cha T.R.A na wapo kazini wakitekeleza majukumu yao.

Basi bwana, katika vita nikuvute, Wananchi wakahoji, kama mpo kazini mbona usiku? Na tena bila escort ya polisi mwenye gwanda?

Jamaa walipoona Wananchi wamekaza na wanazidi kuongezeka(bodaboda walipaki kwa mbele na nyuma ya cluza hilo la serekali) ikabidi waliondoe gari kwa nguvu na hivyo kuishia kugonga bodaboda zilizokua zimewabuloku.

Wananchi kuona hivyo nao wakaanza kutimiza wajibu wao.

BADO HAIJADHIBITIKA KAMA NI KWELI WATEKAJI AU NI WATUMISHI

Hii stori mwenyewe nimekuta imeshatokea msije kunitafuta mimi ni raia mwema na ninampenda rais Samia.

Pia Soma: Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam
View attachment 3169961View attachment 3169963View attachment 3169967
Kumbe T.R.A wanafanya kazi usiku !! tena bila hata vitambulisho ??
 
Kuna siku niliwaza hizo Tabia za kutekana, Ipo siku tutapoteza Raia Wengi na Askari kwa Pamoja.
uzaifu upo ktk mfumo.
Mfumo wa Ulizi na Usalama uko Mixed na siasa ndio maana yanatokea haya tunayoyaona.
Kweli kabisa kwa sasa itakuwa ngumu kwa baadhi ya watu kutekeleza majukumu yao ya kazi kwa hili ambalo wamelilea.
 
Gari ya serikali namba STL 9923, Usiku huu imeshambuliwa kwa mawe na wananchi wenye hasira butu, na watumishi waliokuwemo ndani wameumizwa.

Chanzo cha kizaa zaa hicho inasemekana hilo gari la serikali lilikua linaifuatilia gari nyingine ndogo aina ya BMW.

Baada ya kufika maeneo ya tegeta kwa ndevu, ile gari ya serikali ika buloku ile BMW.

Wananchi walipotaka kujua kulikoni, maana stori za utekaji zimekua nyingi, jamaa wakajitetea wao ni watumishi wa serikali kitengo cha T.R.A na wapo kazini wakitekeleza majukumu yao.

Basi bwana, katika vita nikuvute, Wananchi wakahoji, kama mpo kazini mbona usiku? Na tena bila escort ya polisi mwenye gwanda?

Jamaa walipoona Wananchi wamekaza na wanazidi kuongezeka(bodaboda walipaki kwa mbele na nyuma ya cluza hilo la serekali) ikabidi waliondoe gari kwa nguvu na hivyo kuishia kugonga bodaboda zilizokua zimewabuloku.

Wananchi kuona hivyo nao wakaanza kutimiza wajibu wao.

BADO HAIJADHIBITIKA KAMA NI KWELI WATEKAJI AU NI WATUMISHI

Hii stori mwenyewe nimekuta imeshatokea msije kunitafuta mimi ni raia mwema na ninampenda rais Samia.

Pia Soma: Ufafanuzi kuhusu shambulio la gari la watumishi wa TRA eneo la Tegeta, Dar es Salaam
View attachment 3169961View attachment 3169963View attachment 3169967
Kama Taifa tunaelekea wapi? Hii siyo afya kwa ustawi wetu
 
Idara ya forodha inafanya kazi masaa 24 na ina majukumu ya kipolisi ya kukamata wahalifu wanaovunja sheria za kiforodha. Kazi ya kukamata magendo au mizigo iliyoingia nchini kinyume cha sheria ya forodha inafanywa na watumishi wa TRA wa idara ya forodha. TRA ina doria za usiku za kudhibiti na kukamata magendo. Jamii inapaswa kuelimishwa kuhusu hili.
 
Sheria ipi inayompa mamlaka Afisa wa TRA kufanya arrest
 
Back
Top Bottom