Tegeta, Dar: Maafisa wa TRA washambuliwa na wananchi kwa mawe

Wangeitia moto hiyo gari blood mazaf@kaz
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeeleza masikitiko yake na kuutarifu umma kuhusiana na gari yake yenye namba za usajili STL 9923 ikiwa na watumishi watatu (3) ndani yake waliokuwa kwenye doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo ya magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za forodha na kutolipiwa ushuru imeshambuliwa imeshambuliwa na watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam usiku wa Desemba 05.2024

Taarifa ya TRA iliyotolewa kupitia Idara ya Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano imebainisha kuwa kadhia hiyo imekuja baada ya watumishi wa mamlaka hiyo kubaini kwamba gari yenye namba T229 DHZ aina ya BMW X6 ambayo inadaiwa kuingizwa nchini kinyemela bila kulipiwa kodi za serikali stahiki na kwa mujibu wa sheria, hivyo kuifuatilia kwa lengo la kuikamata na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa, wakati watumishi hao wa TRA wanaendelea kutimiza wajibu wao walihusishwa na vitendo vya utekaji, hatua iliyopelekea wao na gari walilokuwa wanatumia kushambuliwa

"Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatoa pole kwa watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao, pamoja na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii, na kuwaombea wapone haraka" -TRA

Katika hatua nyingine, mamlaka hiyo imeuhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.
 
Najaribu kuwaza kama hao jamaa wa the so called TRA walikuwa kwenye magumashi yao binafsi, kesho wanaeleza nn ofisi gari kuvunjwa vioo na wao kujeruhiwa πŸ˜‚πŸ˜‚.
Bila police escort ni kwamba ilikuwa mishe yao binafsi ya upigaji, ofisini lazima kinuke japo huwa wanayamaliza kiaina kwani hakuna msafi among them all.
Possibility nyingine inaweza kuwa ni 'wasiojulikana' sasa baada ya mission kuzuiwa na raia wema wamekuwa spin-crafters hivyo basi kwa kuwa walimlenga mmiliki wa X6 ndiyo twist yao wanahadaa umma kuwa ilikuwa ni operation ya TRA.
My thinking ni kati ya hayo mawili.
 
Kumbe T.R.A wanafanya kazi usiku !! tena bila hata vitambulisho ??
 
Kuna siku niliwaza hizo Tabia za kutekana, Ipo siku tutapoteza Raia Wengi na Askari kwa Pamoja.
uzaifu upo ktk mfumo.
Mfumo wa Ulizi na Usalama uko Mixed na siasa ndio maana yanatokea haya tunayoyaona.
Kweli kabisa kwa sasa itakuwa ngumu kwa baadhi ya watu kutekeleza majukumu yao ya kazi kwa hili ambalo wamelilea.
 
Kama Taifa tunaelekea wapi? Hii siyo afya kwa ustawi wetu
 
Idara ya forodha inafanya kazi masaa 24 na ina majukumu ya kipolisi ya kukamata wahalifu wanaovunja sheria za kiforodha. Kazi ya kukamata magendo au mizigo iliyoingia nchini kinyume cha sheria ya forodha inafanywa na watumishi wa TRA wa idara ya forodha. TRA ina doria za usiku za kudhibiti na kukamata magendo. Jamii inapaswa kuelimishwa kuhusu hili.
 
Sheria ipi inayompa mamlaka Afisa wa TRA kufanya arrest
 
Sisi wananchi kipande hiki Cha TEGETA, rais Samia aliwahi kutuuliza "mtachanja?" Tukamjibu kwa nguuuuuuvu "HATUCHANJIIIII"

Kwa sasa hv taifa limegubikwa na wingu la utekaji, walichofanya wakazi wenzangu wa TEGETA NI Jambo jema. Na MAENEO mengine muige
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…