Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

Kimya kimya,unatakiwa ule pilau bila kelele,kuingia mmoja mmoja,kutoka mmoja mmoja,hapo hakuna kupendeza,unakuja ukiwa ovyo ovyo nguo unaweka kwenye begi ukiingia ndani ndio unavaa ili userebuke,kinyume cha hapo lipa kodi ili ujiachie...
Muziki vipi? Mnaingia kama wezi. Nimecheka sana.
 
Hii haiwezi kuwa kweli hata kidogo. Mimi nikifanyia birthday party hapa ghetto nikamuita Mariam awe MC na wapishi ni marafiki zangu nani aje kunikamata. Shughuli hii ni ya kiuchumi kwani?

Haiwezekani serikali iwe na watu mburula kiasi hiki. Labda kwa kumbi za kukodi nitaamini lakini nyumbani, sasa si kutaongezeka na kodi ya kupika chakula au kumiliki TV.
 
hahah hakika hii ndiyo serikali katili ya CCM
 
Wanachomaanisha ni kuwa wamepandisha gharama za hizi shughuli.Yaani kama MC alikuwa analipwa TZS 25,000/= akienda kweye shughuli ya mnyonge kama vile kipaimara sasa itabidi alipwe TZS 75,000/= ili yeye aweke mfukoni 25,000/= na 50,000/= alipie kodi.Tafsiri yake ni kwamba wanyonge hawataweza kuwafanyia wapendwa wao sherehe tena!
 
Wasi wasi wangu ni kwamba ukifanya sherehe hme kwako na hujalipa hiyo kodi ama kupata kibali watakuja migambo kukubeba kibindo/juu juu mbele ya mkeo mpaka kituoni kwa tuhuma za ukwepaji kodi.....!!??
walah tupo pabaya....
 
Wewe ni kinara wakusifia ccm humu, leo unajifanya una uchungu, ndo madhara ya ccm kuongoza hili taifa miaka sitini with nothing new, sikuhizi Hali ya uchumi mbovu, sasa wanatesa wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…