Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

Imeripotiwa kuwa ngoma za vigodoro, jando na unyago sasa zitaanza kutozwa kodi ya shilingi 50,000. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke Lusubilo Mwakabibi amesema tozo hiyo ni lazima na atakayekaidi kufanya shughuli bila kibali atalipa faini ya shilingi 200,000
 
Kwani chadema ishika madaraka itaendesha serikali bila kutoza kodi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku mtaani tumeambiwa sisi WANACCM hatutalipa kodi hiyo bali itawahusu wapinzani tu....

Asante sana magufuli kwa kutujali
Ccm oyeeeeee!!!
 
Imeripotiwa kuwa ngoma za vigodoro, jando na unyago sasa zitaanza kutozwa kodi ya shilingi 50,000. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke Lusubilo Mwakabibi amesema tozo hiyo ni lazima na atakayekaidi kufanya shughuli bila kibali atalipa faini ya shilingi 200,000
Baada ya kufanikisha wizi wa kura Kakonko , haya ndio mapya aliyokuja nayo mjini
 
Ni jambo jema. Ifike wakati hizi ngoma ziachwe zifanyike huko vijijini. Sherehe kama hizi zilipaswa zifanyike nyumbani kama private parties au zifanyike kwenye kumbi. Na wenye kumbi za sherehe wazisajili na wawe wanaomba vibali vya sherehe na kulipia kabla ya sherehe husika.

Majiji tunayojaribu kuyaweka kwenye hadhi ya kimataifa hayapaswi kuwa na sherehe za kufunga mitaa.
 
Mitano tena!
9087654098.jpg
 
Kimya kimya,unatakiwa ule pilau bila kelele,kuingia mmoja mmoja,kutoka mmoja mmoja,hapo hakuna kupendeza,unakuja ukiwa ovyo ovyo nguo unaweka kwenye begi,ukiingia ndani ndio unavaa ili userebuke,kinyume cha hapo lipa kodi ili ujiachie...
 
Amefafanua kwamba katika "shughuli" yoyote watakaotakiwa kulipa kodi ni ma-MCs 50,000/= DJ 30,000/=, mpishi 50,000/=, ukumbi 50,000/= nk. Malipo haya haijalishi ukubwa wa shughuli hata kama ni birthday ya mtoto wa mwaka mmoja.
This is hogwash to say the least......

Kwahio kama DJ/MC kapata shughuli ya kulipwa elfu 25 au 10 kwa siku, itabidi atoe kwenye mfuko wake kulipa hio difference..., Au wanataka kusema profit kwa kila kazi kwa hawa watu zinazidi hizo kodi, in short kwa shughuli yoyote mtu inabidi aweke kando 180,000/ kwa ajili ya kodi no matter kama ametumia cost ya laki mbili au bilioni mbili ?
 
You knew Sengerema was going to set the precedent.

Sometimes wacha yawakute tu aiwezekani watu wajiamulie mambo na sheria ipo; halafu wahusika kwao iwe hewala tu.

Kesho watasema mechi za ndondo cup kuchezwa lazima walipie tozo ya laki moja ili kuwe na kiingilio.

Kikubwa kwao chochote kinachompa mtanzania starehe nchi ambayo wananchi wake wanatakiwa wawe na manung’uniko according global happiness index lazima kiangaliwe upya na kuitoa hiyo furaha maana ilo jambo ni anasa.

Haya ndio madhara ya kuwa na waziri wa fedha asie mwanasiasa na kura za ushindi aziitaji ushawishi; vinginevyo waziri mwingine yeyote asingekubali huu upuuzi.

Mwisho wa siku anaelipa ni wenye sherehe sio mpishi, MC, mwenye ukumbi wala photographer; just pathetic watu wakikubali huu upuuzi.

Mtu mwanawe kafaulu shule, mzazi amefurahi anataka kumfanyia ka part inabidi aachane na hilo wazo maana kuna tozo za halmashauri zinamsubiri; aisee na wananchi wanadhani this is OK ili swala likipita bila makash kash sasa ndio ntaamini watanzania ni kama kondoo.
 
Back
Top Bottom