Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hii ndio Kashfa mpya inayozunguka kwenye Manispaa hiyo kwa sasa , ikiwa ni siku chache tangu kashfa ya Mwenyekiti wa ccm wa wilaya hiyo kutafuna zaidi ya sh. mil 300 za vikundi kuibuliwa.
Mstahiki Meya Abdallah Ntinika anatajwa kuwashawishi kwa nguvu kubwa viongozi wa Manispaa hiyo ili Waiuze Shule hiyo ya umma, ambayo tayari imekwishapelekewa pesa za serikali , zinazoitwa hela za COVID 19, na tayari madarasa saba mapya yakiwa yamekwisha jengwa.
Sababu hasa ya Meya huyo kufanya jambo hilo la Uhujumu Uchumi bado hazijafahamika, ingawa dalili za awali zinaonyesha kwamba kuna ushawishi wa 10%.
Kama kawaida yetu tutaendelea kukuletea kila kinachojiri kwenye manispaa hiyo baada ya Nzi wetu kuahidi kubaki ndani ya manispaa hiyo kutudokolea kila uhondo