Wanajamii huwa wanakataa ile kitu inaitwa "kupendana" na wanafocus katika vitu kama kazi, kipato, uwezo wa kujenga nyumba na kumiliki mali. Ila wanasahau kinachocomtroll mtu na maamuzi yake ni akili yake.
Akili ikishapata kile imetaka huwa inarejea moyo na kutaka kile nafsi inahitaji.
Huwezi fanya mahaba na mtu ambaye ulimtaka tu kwaajiri ya kujenga nyumba nzuri, kupata kazi, kupata watoto, kukusapoti biashara, yaani sio kwa yale mapenzi ya msisiko.
Kuna watu waliachana watu waliowapenda kwa dhati ile tokea moyoni kupita maelezo na walikuwa tayari kwa lolote ingawa ni dini tofauti, hali ya kiuchumi hawalingani, hawana malengo, etc sababu ambazo kimsingi ukizipa muda huwa zinapungua nguvu na kutokuwa na uzito tena na ndipo moyo unaanza kuhoji, umepata nyumba, gari, watoto, kazi /biashara, upo wapi upendo? Fulani alikupa msisimko na hata sasa ukimkumbuka unapata hisia nzito juu yake, kwann uliamua kuachana nae na unampenda sana?
Ndoa tunafunga kufurahisha wazazi na ndugu zetu, nyumba ya kuishi hata tukiikosa leo tunaweza jenga muda mwingine sio lazima iwe leo hii tunapotaka sisi, magari, biashara, pesa na mali vinatafutwa, tukiwa na subira tutavipata. Ila upendo wa hisia nzito ule wa "it might be you" huwa unakuja mara moja tu, huwezi tena pata popote, ukishaondoka unaishi na gepu la upweke maisha yako yote hadi uzee na majuto yake ni mazito kuliko chochote.
Usione hadi watu wanauwana na kufanyiana ukatili zile ni hasira za upweke na kukosa mrejesho wa ule upendo ule waliotegemea. Ukimpata ambaye mtaclick komaa nae hadi kieleweke, maisha huwa yanatupa mitihani ya muda tu sio milele, ukisema unataka penzi la kweli, MUNGU anakupa mtu asiyeeleweka ukiprove unaweza mpenda na ukawa imara utashangaa reward yake anakuja kaa sawa baadae na anabadilika na kuwa vile ulitamani awe, trust me mradi asikusaliti tu na kupenda mwingine.
Ukipata mali, nyumba, magari, pesa, na vingine, then what's new coming from them? [emoji23]
But ukipendana na unayempenda ni hadi uzeeni you only exchange vibes, loneliness inakuwa the myth.