Japo jamaa anaongea kimuzaha lakini bado anayo point. Hivi hili janga lingeikuta nchi ya Sweden ambayo majuzi Walichoma Qur'an hivi Waislam WA Duniani kote hasa humu JF wangeliacha kuwakashifu kweli kwa kulihusisha na kuchoma kwao Qur'an? Hakika Mungu hapangiwi hizi dini ni usaniii tu, hazina nafasi mbele ya Mungu Bali roho ya binadamu. Mtenda mema anaweza kufa huku jambazi akifikisha umri WA miaka 100 licha ya ushenzi wake.
Nikusaidie kukujibu! Na nadhani bila shaka kwa asilimia kubwa pengine tunaweza tukalielewa hili. Na nitalijibu kwa munasaba wa mazingira ya hoja kwa maana fikra tofauti mlizobadilishana. Kwa msingi huo, hali ipo hivi:
Kupata mali au kuwa na maisha fulani ya hali ya juu haimaanishwi ndiyo kupendwa na Mungu. Au kutopatwa na majanga ya asili kama yanavyoitwa haimaanishi ndiyo kupendwa na Mungu. Mungu huwa anaadhibu kwa namna tofauti tofauti.
Unaweza ukawa na pesa nyingi na hali yako ya maisha ni nzuri tu. Kwa kuwa ukaenda tofauti na namna ambayo Mungu ameiridhia, Mungu anaweza akakukasirikia na adhabu yake wewe unaweza ukawa bakhili tu! Ubakhili kwa Mungu haufai. Yaani; una mali na Mungu kaamrisha tusaidiane na mtu huyu akajifanya ni mjanja zaidi Mungu anaweza akamtia adhabu ya ubakhili. Utajiona unaweza lakini kumbe ndiyo unapotea.
Firauni aliwatesa wana wa Yaaqub (Waisrael) mateso makubwa! Mungu akamtuma Nabii Musa amani ya Mungu iwe juu yake lakini bado firauni akaleta ukaidi. Lakini ukitizama maisha ya firauni yalikuwaje? Yalikuwa ni mazuri yasiyo na chembe za dhiki.
Pengine unaweza ukajiuliza kwa nini Mungu muda wote aliamua kumuacha awe na maisha hayo mazuri licha ya kuwatesa wana wa israel, kumletea ukaidi Mtume wake na akamletea ukaidi Mungu mwenyewe? Mungu ana namna zake za kuadhibu.
Wengine wanaweza wakawa na kila kitu, kwa kuwa wakaenda tofauti na Mungu, yeye Mungu anaweza akawakasirikia. Akawapa adhabu ya hofu tu! Maisha yao yote wanaishi kwa hofu! Uchumi wa nchi ni mzuri, maisha ya raia ni mazuri lakini taifa lenu likaishi kwa hofu kubwa mnoo!
Mtenda mema anaweza kufa huku jambazi akifikisha umri WA miaka 100 licha ya ushenzi wake.
Kwa namna nyengine kifo kinakuwa ni adhabu kutoka kwa Mungu. Kwa namna nyengine kifo si adhabu kutoka kwa Mungu. Nabii Ibrahim amani ya Mungu iwe juu yake alipoambiwa umri wake wa kuishi kwenye hii dunia umefikia kikomo. Akamwambia Mungu inakuwaje rafiki anamuuwa rafiki yake? Mungu akamjibu; inakuwaje rafiki hataki kukutana na rafiki yake?! Kwa kuwa Nabii Ibrahim ni muelewa akachagua kifo!
Again; kuna namna tofauti ya haya masuala! Muda mwengine uovu unapozidi na ufisadi ukaenea, Mungu kwa mapenzi yake huwachukua watendao mema ili wafanyao ufisadi wapoteee zaidi ili awaadabishe zaidi kwa namna tofauti tofauti atakayoiamua yeye mwenyewe.
Huu ni upande wa pili wa shilingi niliyokupa! Hayo mambo yapo dhahiri kama unavyoyaona. Muda mwengine mambo yapo baatwiin.
Na haiwezekani Mungu akawaleta duniani na kuwaacha tu mzagae! Binadamu ndani ya mwili wake amewekewa kisembuzi kutoka kwa Mungu. Hivyo, binadamu anafahamu zuri na anafahamu baya! Lakini Mungu hakukuacha hivyo tu bali amekupatia na msaada wa elimu. Elimu hii ni kutoka kwa Mitume yake kuwa binadamu aishi kwa kanuni na njia hizi. Huo mfumo wa elimu aliyotupatia ndiyo unaoitwa dini.
Mungu ana utaratibu wake aliyouweka kwa binadamu. Kama ilivyo serikali kwa raia au kitu chochote kilivyowekewa utaratibu wa kuendesha shughuli zake. Huu ni mfano mdogo tu.
Naam, Mungu ametuchagulia mfumo wa maisha kwa jinsi gani binadamu yamfaa aishi kwa kupitia elimu kutoka kwa Mitume yake. Huo mfumo aliyotuchagulia ndiyo unaoitwa dini. Na ni nini maana ya dini? Ni mfumo kamili wa maisha ya binadamu.