TEUZI: Rais Samia ateua Wakuu wa Wilaya. Nassari, Dkt. Mashinji, Lijualikali, Msando, Nikki wa Pili ndani

TEUZI: Rais Samia ateua Wakuu wa Wilaya. Nassari, Dkt. Mashinji, Lijualikali, Msando, Nikki wa Pili ndani

Pongezi kwa wateule wote.
Wote mnafaa na mnastahili kupewa dhamana hiyo, Mhe. Rais amewaamini na sisi wananchi tunawaamini kuwa mtachapa kazi kwa nguvu na maarifa.
usisherehekee kupata cheo bali sherehekea pindi utakapo tatua kero za wananchi na kuleta maendeleo kwenye kipande chako ulicho kabidhiwa.
Mungu awatangulie.
 
Rais Samia Suluhu Hassan leo ameachia mkeka wa Wakuu wa Wilaya mbalimbali uliosheheni vijana. Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wapya ni pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji, pia yupo Joshua Nassari na Wakili Albert Msando. Wengine ni Mwenyekiti wa UVCCM Kherry James, mtangazaji Hassan Ngoma kutaja kwa uchache.
Yetu macho. UDC sasa hauheshimiki tena!
 
Pongezi kwa wateule wote.
Wote mnafaa na mnastahili kupewa dhamana hiyo, Mhe. Rais amewaamini na sisi wananchi tunawaamini kuwa mtachapa kazi kwa nguvu na maarifa.
usisherehekee kupata cheo bali sherehekea pindi utakapo tatua kero za wananchi na kuleta maendeleo kwenye kipande chako ulicho kabidhiwa.
Mungu awatangulie.
 
Nashtuka kutoka kupumzika naona simu yangu sms kibao kila mahali hadi nikashtuka kuna nini?
Kumbe kuna kacheo uchwara nimeshatupiwa humu. Mama mimi na udisii wapi na wapi? Hiyo nafasi yangu mpe mtu mwingine maana wala hata sitajisumbua kwenda huko. Yani wala hata siwazi achilia mbali kupeleka kwato zangu huko.
Acha mkwara mkuu..thibitisha!
 
Unadhani wanalipwa 2M mshahara wa Headmaster wa sekondari?
6M plus allowances+ulinzi+nyumba kali+V8+Dereva.
Haahaa ukuu wa wilaya Ni sehemu ya kuifilisi hazina ya nchi bila jasho...
Siasa ndio ajira pekee zilizobakia .

Yaani serikali imeshindwa kutengeneza ajira imebakia kuteua watu nafasi za kisiasa.

Shame.
Haahaa, siasa ndo eneo pesa ya nchi inapotafunwa, mama anatoa ajira kwa makada vijana...
 
Hongera kwako, Dada yetu Jokate, Mama amekuamini tafadhali onyesha uwezo wako kama ulivyowaonesha Kisarawe. Wana TMK tunakusaport.
 
hongera nyingi sana kwa kaka yangu kherey Jemsi, naamini sasa wilaya mpya ya Ubungo haswa Jimbo la kimbamba itachangamka, angalau sasa miradi ya DMDP itafanyika ktk kata ya Kibamba.
 
Back
Top Bottom