TEUZI: Rais Samia ateua Wakuu wa Wilaya. Nassari, Dkt. Mashinji, Lijualikali, Msando, Nikki wa Pili ndani

TEUZI: Rais Samia ateua Wakuu wa Wilaya. Nassari, Dkt. Mashinji, Lijualikali, Msando, Nikki wa Pili ndani

wakuu yule jamaa aliyegombeaga ubunge na ndugai kisha akapigwa rungu na ndugai na kuzimia,kisha kumpooza ccm wakampa ukuu wa wilaya ya meatu.

naona kwenye teuzi hayupo,kapewa kitengo gani?

anaitwa dkt chilongani!
😂😂😂😂😂
 
Rais wetu ameshamaliza kazi kwa kupanga safu mpya ya maDC. Huo ndio wajibu wake wa kikatiba, kama kiongozi wa taasisi nyeti ya urais ni lazima ateuwe watu ambao yeye mwenyewe anawaamini kuwa wataweza kumsaidia kutekeleza majukumu yake ya kuiongoza nchi yetu katika ngazi ya wilaya.

MaDC wateule wote nawapa pongezi kwanza kwa kuaminiwa katika nafasi mlizopewa. Pili, ni kazi kwenu kuja na mikakati mipya ili kuweza kufanikisha na kutekeleza kwa kiwango cha juu sana ilani ya chama kuelekea mwaka 2025.
 
Kuna watu ni wanafiki sana Kwahiyo mama kuteua ma-DC imewauma sana?mbona kipindi cha Jpm hamkulalamika?

Kipindi kile watu waliteuliwa hamkulalamika sasa samia anateua mwalalamika kwanini akifanya samia inakua nongwa lakini akifanya magufuli inakua ni sawa?

Au ndo mkuki wa nguruwe

Mbona kipindi cha jpm akiteua hamkunyanyua pua zenu?

Tena wanaolalamika ni vijana wa mataga ambao kipindi cha jpm walifurahia teuzi

Wacheni unafiki acheni mama achape kazi
Hao ni hopelessly , mama pigà kazi
 
Hivi mama anafeli wapi wadau ?yaani ndani ya ccm hakuna vijana wa kupewa uteuzi hadi anawapa ulaji hao wahamiaji wenye tamaa ya madaraka toka chadema, kuna vijana wengi ccm wamekipigania chama toka zamani lakini hawajapata uteuzi,daah yaani anarudia yale yale kama ya hayati magufuli
UVCCM wenye akili.hamna
 
Sio mbaya sana kuwateua vijana wengi kiasi hiki kama wataelewa kitu wanatakiwa kufanya, ubaya unakuja vijana wengi walioteuliwa walionekana kuzingua... Lakini pia unajua kale karoho ka kibongo tena!!!

Nadhani ni mpango mzuri kwa Rais Samia na nadhani matarajio yake ni kuona hawa vijana aliowateua ndio watasaidia na itakuwa rahisi sana kuwainua vijana wenzao ambao ndio kundi kubwa kwa sasa katika jamii yetu na waliopo katika maeneo yao ili kukabiliana na changamoto za kuendesha maisha
 
Huyo kama hii teuzi imempita ndo basi tena atafte shughuli nyingine tu.
Atakuwa anatumia jina lingine
Nadhani labda ni yule wa Temeke maana hili jina ni geni sana huenda ndio yeye
 
Back
Top Bottom