Headcorner
JF-Expert Member
- Nov 26, 2020
- 205
- 292
BMT (Baraza la michezo Tanzania) wanachukua mgao kwa kipi wakati tayari kuna VAT?Taarifa hii hapa
Simba si wanajenga kule GOBA sijui BUNJUShirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limetoa taarifa ya mapato ya Mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga ambao ulifanyika jumapili iliyopita tarehe 16/4/2023,wadau mbalimbali wametoa maoni yao kufuatia timu mwenyeji (Simba)kuambulia sh 188,987,181.10 tu katika mapato yote yaliyopatikana,kuna haja ya timu hizi kuwa na Viwanja vyao kukwepa Unyonyaji huu
Sio upeo wao mdogo, huko kwenye tiketi wana ganji zaoBMT ni taasisi ya serikali kama serikali inachukua Vat kwanini BMT wapewe mgao, hili jambo alilipigia kelele sana Ndolanga ila alionekana hajali pia gharama za tiketi zinafikaje milioni 22 wakati tiketi ni electronics kwa kifupi hii hali imechangiwa na viongozi wa vilabu wengi upeo wao ni mdogo.
inakuaje timu mwenyeji anapata 46% ya mapato?Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limetoa taarifa ya mapato ya Mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga ambao ulifanyika jumapili iliyopita tarehe 16/4/2023, wadau mbalimbali wametoa maoni yao kufuatia timu mwenyeji (Simba)kuambulia sh 188,987,181.10 tu katika mapato yote yaliyopatikana, kuna haja ya timu hizi kuwa na Viwanja vyao kukwepa Unyonyaji huu.
Hiyo serikali ya kuingilia kati ndo mnufaika mkubwa wa hizo pesa .Hili swala serikali iliingilie kati.
Je Simba na Yanga wakiamua cheza bila mashabiki watapata wapi hizo fedha?
Bora timu ipewe asilimia 70 ya mapato
Ukweli ni kwamba hata kama Simba au Yanga angekua na uwanja wake hapa angeokoa milioni 47 tu.
Vat ingelipwa hiyo hiyo, BMT wangechukua kiasi hiko hiko, Hapo kwenye gharama za ticket kungebaki hivyo hivyo, gharama za mchezo na mambo mengine yote.
Ni wakati wa kuuliza maswali sahihi
1 ) BMT wanachukua hela za nini wakati wao ni serikali na serikali imeshachukua pesa pale kwenye VAT
2) Gharama za ticket zinafikaje milion 22 wakati ticket ni za electronic
3) Gharama za mchezo mchanganuo wake upoje? Wanalipwa wakina nani? Kwa nini?
4) TFF, TPLB, FA tofauti yake ni nini maana viongozi ni wale wale wanabadili kofia tu kubeba maokoto
5) Gharama za kukodi uwanja zinakaribiaje milioni hamsini na unakwenda unakuta uwanja mchafu, viti vichafu, vyoo vichafu na hakuna huduma yoyote zaidi ya kukaa tu?
Imefikia pahala limeshakuwa chaka la maokoto na hatuwezi kusogea kwa style hiyo.