TFF imetoa taarifa ya mapato ya Mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga ambao ulifanyika jumapili iliyopita tarehe 16/4/2023

Headcorner

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2020
Posts
205
Reaction score
292
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limetoa taarifa ya mapato ya Mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga ambao ulifanyika jumapili iliyopita tarehe 16/4/2023, wadau mbalimbali wametoa maoni yao kufuatia timu mwenyeji (Simba)kuambulia sh 188,987,181.10 tu katika mapato yote yaliyopatikana, kuna haja ya timu hizi kuwa na Viwanja vyao kukwepa Unyonyaji huu.

Simba na Yanga jengeni viwanja vyenu

img-20230420-wa0026-jpg.2593943

Taarifa hii hapa
BMT (Baraza la michezo Tanzania) wanachukua mgao kwa kipi wakati tayari kuna VAT?
TFF na TPLB zote ni taasisi inayofanya kazi pamoja, kwanini ela zigawanyike kwa taasisi zote mbili badala ya kuingia upande wa TPLB peke yake?
Kama kulikuwa na gharama ya uwanja na gharama ya mchezo, FA mkoa wanapewa ela kwaajili ya lipi?

Gharama ya kutengeneza tiketi ni mil 22+ mh haya watu wenye fani zao wanaweza kujua kama ni sahihi au sio sahihi.
 
Ipo siku itajua kwmba bossi wako anachangia kukukwamisha ili uwendelee kumtumikia, unaweza akapnga mipango yako safiii ,akatokea mtu akawashauli wengine wakaaribu mipango yooote, waza cmba na yanga wakawa na viwanja selikali itapata nn kupitia hizo timu?
 
BMT ni taasisi ya serikali kama serikali inachukua Vat kwanini BMT wapewe mgao, hili jambo alilipigia kelele sana Ndolanga ila alionekana hajali pia gharama za tiketi zinafikaje milioni 22 wakati tiketi ni electronics kwa kifupi hii hali imechangiwa na viongozi wa vilabu wengi upeo wao ni mdogo.
 
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limetoa taarifa ya mapato ya Mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga ambao ulifanyika jumapili iliyopita tarehe 16/4/2023,wadau mbalimbali wametoa maoni yao kufuatia timu mwenyeji (Simba)kuambulia sh 188,987,181.10 tu katika mapato yote yaliyopatikana,kuna haja ya timu hizi kuwa na Viwanja vyao kukwepa Unyonyaji huu
Simba si wanajenga kule GOBA sijui BUNJU
 
Inyeshe tena kidogo tuone matundu yanayovuja inyeshe inyeshe tafadhali
 
Hili swala serikali iliingilie kati.
Je Simba na Yanga wakiamua cheza bila mashabiki watapata wapi hizo fedha?
Bora timu ipewe asilimia 70 ya mapato
 
BMT ni taasisi ya serikali kama serikali inachukua Vat kwanini BMT wapewe mgao, hili jambo alilipigia kelele sana Ndolanga ila alionekana hajali pia gharama za tiketi zinafikaje milioni 22 wakati tiketi ni electronics kwa kifupi hii hali imechangiwa na viongozi wa vilabu wengi upeo wao ni mdogo.
Sio upeo wao mdogo, huko kwenye tiketi wana ganji zao
 
Halafu mbona kwenye huu mchanganuo hakuna ticket za platinum ( 150,000/=) na executive ambayo ni sh 40,000/=
Inamaana Simba walizitangaza lakini hazikupata mteja hata mmoja au inakuaje. Hapa upigaji ni kupita kiwango aisee
 
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limetoa taarifa ya mapato ya Mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga ambao ulifanyika jumapili iliyopita tarehe 16/4/2023, wadau mbalimbali wametoa maoni yao kufuatia timu mwenyeji (Simba)kuambulia sh 188,987,181.10 tu katika mapato yote yaliyopatikana, kuna haja ya timu hizi kuwa na Viwanja vyao kukwepa Unyonyaji huu.

img-20230420-wa0026-jpg.2593943

inakuaje timu mwenyeji anapata 46% ya mapato?
hio 54 inaenda wapi yote!?

mbona zamani timu zilipokuwa zinagawana mapato kila timu ilikua inapata 33% ya mapato yote?
 
Hili swala serikali iliingilie kati.
Je Simba na Yanga wakiamua cheza bila mashabiki watapata wapi hizo fedha?
Bora timu ipewe asilimia 70 ya mapato
Hiyo serikali ya kuingilia kati ndo mnufaika mkubwa wa hizo pesa .
 
haya mambo inatakiwa yaende kwa percent (%).....
lakini pia inatakiwa hawa simba na yanga wakodishe viwanja vya ccm......

ufike wakati tff ibaki kuwa regulator, bodi ya ligi iachiwe majukumu yake ya kuendesha ligi, vilabu viachiwe jukumu la kuandaa mechi
 
Ukweli ni kwamba hata kama Simba au Yanga angekua na uwanja wake hapa angeokoa milioni 47 tu.

Vat ingelipwa hiyo hiyo, BMT wangechukua kiasi hiko hiko, Hapo kwenye gharama za ticket kungebaki hivyo hivyo, gharama za mchezo na mambo mengine yote.

Ni wakati wa kuuliza maswali sahihi

1 ) BMT wanachukua hela za nini wakati wao ni serikali na serikali imeshachukua pesa pale kwenye VAT

2) Gharama za ticket zinafikaje milion 22 wakati ticket ni za electronic

3) Gharama za mchezo mchanganuo wake upoje? Wanalipwa wakina nani? Kwa nini?

4) TFF, TPLB, FA tofauti yake ni nini maana viongozi ni wale wale wanabadili kofia tu kubeba maokoto

5) Gharama za kukodi uwanja zinakaribiaje milioni hamsini na unakwenda unakuta uwanja mchafu, viti vichafu, vyoo vichafu na hakuna huduma yoyote zaidi ya kukaa tu?

Imefikia pahala limeshakuwa chaka la maokoto na hatuwezi kusogea kwa style hiyo.
 
Hilo la uwanja ni mfano Mdogo tu Wa uozo Mkubwa uliopo huko serikalini. Tofauti ni kwamba, huku kwenye mpira kuna Transparency Kwa kiwango kikubwa zaidi ikilinganishwa na sekta nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye Million 410, Simba ambaye ni Mwenyeji wa mchezo amepata Million 188 na point, huku Yanga hajapata kitu kwakuwa ni Mgeni.

9F6C9C30-69B9-41F9-AAF7-B2BF5D53B533.jpeg
 
Ukweli ni kwamba hata kama Simba au Yanga angekua na uwanja wake hapa angeokoa milioni 47 tu.

Vat ingelipwa hiyo hiyo, BMT wangechukua kiasi hiko hiko, Hapo kwenye gharama za ticket kungebaki hivyo hivyo, gharama za mchezo na mambo mengine yote.

Ni wakati wa kuuliza maswali sahihi

1 ) BMT wanachukua hela za nini wakati wao ni serikali na serikali imeshachukua pesa pale kwenye VAT

2) Gharama za ticket zinafikaje milion 22 wakati ticket ni za electronic

3) Gharama za mchezo mchanganuo wake upoje? Wanalipwa wakina nani? Kwa nini?

4) TFF, TPLB, FA tofauti yake ni nini maana viongozi ni wale wale wanabadili kofia tu kubeba maokoto

5) Gharama za kukodi uwanja zinakaribiaje milioni hamsini na unakwenda unakuta uwanja mchafu, viti vichafu, vyoo vichafu na hakuna huduma yoyote zaidi ya kukaa tu?

Imefikia pahala limeshakuwa chaka la maokoto na hatuwezi kusogea kwa style hiyo.

Hili la BMT nadhani vilabu vifikie hatua hata kwa kwenda ngazi ya juu, FIFA wamekataza serikali kuingilia maswala ya michezo. Hivyo BMT haitambuliki na FIFA na haipaswi kupokea mgao wakati hakuna kazi wanayoifanya katika mechi
 
Back
Top Bottom