The Daily Telegraph: Iran ilipiga kambi 5 za kijeshi za Israel

Mtamba wa Panya

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2017
Posts
790
Reaction score
1,962
IMG-20250712-WA0003.jpg

Exclusive: Iran ilishambulia kambi tano za kijeshi za Israeli katika vita yao ya siku 12.

Uchambuzi wa data za rada uliofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Oregon(Oregon State University ) na kusambazwa na gazeti maarufu la Uingereza The Daily Telegraph, unaonyesha kwamba Iran ilipiga jumla ya makombora sita kwenye kambi tano tofauti za kijeshi za Israeli katika maeneo ya kaskazini, katikati, na kusini mwa nchi hiyo .

Kambi zilizoripotiwa kuwa zimepata mashambulizi ni:

1. Camp Zipporit

2. Irtah

3. Camp Glilot

4. Beit Nehemia

5. Tel Nof

IMG-20250712-WA0001.jpg

Data hizi hazijawahi kuripotiwa na mamlaka za Israeli kutokana na usiri/udhibiti mkali wa taarifa ndani ya taifa hilo.

Makombora ya Iran kwenye kambi hizo yalisababisha uharibifu mkubwa.

Mfumo wa ulinzi wa Israel unajumuisha Iron Dome, David’s Sling, Arrow, na msaada wa mfumo wa Marekani wa THAAD kutoka eneo la Baharini yaani Red Sea .

IDF imekataa kusema chochote kuhusu habari za kushambuliwa kambi zake hizo

Source: Iran struck five Israeli military bases during 12-day war
 
Hivi kwanini Israel na U.S waliomba ceasefire haraka baada siku chache tu please kwa anayejua sababu ?
Iran ameharibu vibaya sana maeneo mengi Tel Aviv na Haifa japo mamlaka za Israel zimeficha
Ikumbukwe mji wa Haifa umekumbwa na gesi ya Benzene iliyovuja baada ya Iran kupiga zile oil refineries na wakazi wako mbioni kuhamishwa

Benjamin kaona hali tete, kaomba ceasefire kupitia Marekani
Ayatollah hacheki na kima, alisema naigeuza Israel kuwa kifusi
 
View attachment 3402792

View attachment 3402793

Kwa kifupi walipigika hiyo cease fire ni kujipanga
Walipigwa kipigo kitakatifu hata Trump mwenyewe hakuamini kilicho kuwa kinawapata Wayahundi ndio maana aliwasihi Wairan na Israel wasitishe mapigano baada ya kuona Israel inalemewa. Tangu vita hivyo visitishwe hata USA haimchukulii Iran poa hata kidogo!!
 
Kazi ipo.

Hivi kwanini Israel na U.S waliomba ceasefire haraka baada siku chache tu please kwa anayejua sababu ?

Na kwa nini Israel imekuwa mgumu kukubali ceasefire hapo Gaza pamoja hata akiwa ana bembelezwa ?

Muwe mnafuatilia taarifa vizuri.

Hakuna mahali popote ambapo imeripotiwa kuwa Israel iliomba ceasefire. Kama unayo weka hapa.

Nchi ya kwanza kuongelea ceasefire ilikuwa Iran kwenye kikao chake na ujumbe wa Ulaya. Iran ilisema kuwa yenyewe ingesimamisha urushaji wa makombora mara moja, kama Israel nayo ingeacha kushambulia. Siku 2 baadaye Trump akaja na mpango wa ceasefire akisema kuwa amewasiliana na Iran na Israel, na kwamva pande zote zimeridhia. Na kuwa ndege za Israel zilizokuwa njiani kwenda kushambulia Iran, Israel imezirudisha.
Sisi kuandika hapa habari zisizo sahihi wala haibadilishi kwa vyovyote uhalisia wa vita. Kama wairan wengi wameuawa na majeshi ya Israel, hata tuandike vipi, haitabadilika wawe wachache. Kama majengo mengi ya Israel yamebomolewa kwa makombora ya Iran, hata tuandike vipi, majengo hayo hayatasimama.

Hata kwenye taarifa hii, ukifungua hiyo link, wanaeleza kuwa precision ya ulinzi wa anga ya Israel ilidungua 84% ya makombora ya Iran, huku Israel yenyewe ikisema ilidungua 87% ya makombora. Kwenye vifo, hata kwenye hii taarifa, wanasema kuwa Israel ilisaidiwa sana na mifumo yake ya usalama ambapo ni watu 28 tu ndio waliouawa, huku Iran ikiripoti kuwa watu 600 walipoteza uhai.

Kwenye hii taarifa bado inaonesha kuwa wakati Iran ilipoteza sehemu kubwa ya miundombinu yake ya kivita na wanavita, Israel iipoteza zaidi majengo, huku miundombinu yake ya kivita na wanavita wakikosa kuguswa.
 
Iran ameharibu vibaya sana maeneo mengi Tel Aviv na Haifa japo mamlaka za Israel zimeficha
Ikumbukwe mji wa Haifa umekumbwa na gesi ya Benzene iliyovuja baada ya Iran kupiga zile oil refineries na wakazi wako mbioni kuhamishwa

Benjamin kaona hali tete, kaomba ceasefire kupitia Marekani
Ayatollah hacheki na kima, alisema naigeuza Israel kuwa kifusi
Na kweli Ayatolla lifanya hivyo bila ya kusita.

Nilipo angalia photo vile vile na video clip ndiyo nikajiridhisha kwamba kumbe Israel ni paper tiger lilikuwa ni suala la muda tu kabla hawajapata kiboko yao - wamepata fundisho LA mwaka kutoka Iran hawatarudia tena kuichoza Iran.
 
Muwe mnafuatilia taarifa vizuri.

Hakuna mahali popote ambapo imeripotiwa kuwa Israel iliomba ceasefire. Kama unayo weka hapa.

Nchi ya kwanza kuongelea ceasefire ilikuwa Iran kwenye kikao chake na ujumbe wa Ulaya. Iran ilisema kuwa yenyewe ingesimamisha urushaji wa makombora mara moja, kama Israel nayo ingeacha kushambulia. Siku 2 baadaye Trump akaja na mpango wa ceasefire akisema kuwa amewasiliana na Iran na Israel, na kwamva pande zote zimeridhia. Na kuwa ndege za Israel zilizokuwa njiani kwenda kushambulia Iran, Israel imezirudisha.
Sisi kuandika hapa habari zisizo sahihi wala haibadilishi kwa vyovyote uhalisia wa vita. Kama wairan wengi wameuawa na majeshi ya Israel, hata tuandike vipi, haitabadilika wawe wachache. Kama majengo mengi ya Israel yamebomolewa kwa makombora ya Iran, hata tuandike vipi, majengo hayo hayatasimama.

Hata kwenye taarifa hii, ukifungua hiyo link, wanaeleza kuwa precision ya ulinzi wa anga ya Israel ilidungua 84% ya makombora ya Iran, huku Israel yenyewe ikisema ilidungua 87% ya makombora. Kwenye vifo, hata kwenye hii taarifa, wanasema kuwa Israel ilisaidiwa sana na mifumo yake ya usalama ambapo ni watu 28 tu ndio waliouawa, huku Iran ikiripoti kuwa watu 600 walipoteza uhai.

Kwenye hii taarifa bado inaonesha kuwa wakati Iran ilipoteza sehemu kubwa ya miundombinu yake ya kivita na wanavita, Israel iipoteza zaidi majengo, huku miundombinu yake ya kivita na wanavita wakikosa kuguswa.
Uongo...wewe ndo hujui
 
Iran hanaga maneno na porojo, missiles ndo lugha pekee anayoongea kwa ufasaha
 
Usiku wa ceasefire masaa 12 pamepigwa Iran vibaya mno.
Nyie mbiga hizi report sijui hata mnaongea upuuzi gani
 
Muwe mnafuatilia taarifa vizuri.

Hakuna mahali popote ambapo imeripotiwa kuwa Israel iliomba ceasefire. Kama unayo weka hapa.

Nchi ya kwanza kuongelea ceasefire ilikuwa Iran kwenye kikao chake na ujumbe wa Ulaya. Iran ilisema kuwa yenyewe ingesimamisha urushaji wa makombora mara moja, kama Israel nayo ingeacha kushambulia. Siku 2 baadaye Trump akaja na mpango wa ceasefire akisema kuwa amewasiliana na Iran na Israel, na kwamva pande zote zimeridhia. Na kuwa ndege za Israel zilizokuwa njiani kwenda kushambulia Iran, Israel imezirudisha.
Sisi kuandika hapa habari zisizo sahihi wala haibadilishi kwa vyovyote uhalisia wa vita. Kama wairan wengi wameuawa na majeshi ya Israel, hata tuandike vipi, haitabadilika wawe wachache. Kama majengo mengi ya Israel yamebomolewa kwa makombora ya Iran, hata tuandike vipi, majengo hayo hayatasimama.

Hata kwenye taarifa hii, ukifungua hiyo link, wanaeleza kuwa precision ya ulinzi wa anga ya Israel ilidungua 84% ya makombora ya Iran, huku Israel yenyewe ikisema ilidungua 87% ya makombora. Kwenye vifo, hata kwenye hii taarifa, wanasema kuwa Israel ilisaidiwa sana na mifumo yake ya usalama ambapo ni watu 28 tu ndio waliouawa, huku Iran ikiripoti kuwa watu 600 walipoteza uhai.

Kwenye hii taarifa bado inaonesha kuwa wakati Iran ilipoteza sehemu kubwa ya miundombinu yake ya kivita na wanavita, Israel iipoteza zaidi majengo, huku miundombinu yake ya kivita na wanavita wakikosa kuguswa.
..bado hamjasema mtasema tu! waisrael wenyewe wameukubari muziki wa Iran na vyombo vya habari vya kimataifa vinasema Israel inaficha ila ilishenyentwa hasa na yenyewe ndo iliomba po! sasa tukuamini wewe upo mchambawima huko?
 
Back
Top Bottom