Muwe mnafuatilia taarifa vizuri.
Hakuna mahali popote ambapo imeripotiwa kuwa Israel iliomba ceasefire. Kama unayo weka hapa.
Nchi ya kwanza kuongelea ceasefire ilikuwa Iran kwenye kikao chake na ujumbe wa Ulaya. Iran ilisema kuwa yenyewe ingesimamisha urushaji wa makombora mara moja, kama Israel nayo ingeacha kushambulia. Siku 2 baadaye Trump akaja na mpango wa ceasefire akisema kuwa amewasiliana na Iran na Israel, na kwamva pande zote zimeridhia. Na kuwa ndege za Israel zilizokuwa njiani kwenda kushambulia Iran, Israel imezirudisha.
Sisi kuandika hapa habari zisizo sahihi wala haibadilishi kwa vyovyote uhalisia wa vita. Kama wairan wengi wameuawa na majeshi ya Israel, hata tuandike vipi, haitabadilika wawe wachache. Kama majengo mengi ya Israel yamebomolewa kwa makombora ya Iran, hata tuandike vipi, majengo hayo hayatasimama.
Hata kwenye taarifa hii, ukifungua hiyo link, wanaeleza kuwa precision ya ulinzi wa anga ya Israel ilidungua 84% ya makombora ya Iran, huku Israel yenyewe ikisema ilidungua 87% ya makombora. Kwenye vifo, hata kwenye hii taarifa, wanasema kuwa Israel ilisaidiwa sana na mifumo yake ya usalama ambapo ni watu 28 tu ndio waliouawa, huku Iran ikiripoti kuwa watu 600 walipoteza uhai.
Kwenye hii taarifa bado inaonesha kuwa wakati Iran ilipoteza sehemu kubwa ya miundombinu yake ya kivita na wanavita, Israel iipoteza zaidi majengo, huku miundombinu yake ya kivita na wanavita wakikosa kuguswa.