The Inner voice: Sauti ndogo iliyo ndani mwetu ikitueleza kusudi la maisha yetu

Pole sana ndugu. Hujachelewa kabisa kuishi ndani ya kusudi lako. Hujui unatakiwa kuishi muda upi na Kwa Mungu muda haupo so hakuna kuwahi wala kuchelewa.

Yule bwana mdogo kutoka nazareth aliishi kusudi lake kwa muda wa miaka miatatu tu. Ila kafanya pakubwa mno mpaka leo tunamkumbuka.

Unajua nguvu ya wazo.?kwakua unataka kujua kusudi lako weka dhamira kisha omba Mungu utafunuliwa kadri ipasavyo
 
Uzi mzuri,ngoja nikale kwanza,nikirudi ntaupitia...
 
Excellent here[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Nimekuelewa mate.hope Yatakaa sawa.
Hua ni muumini wa kuwaambia watu utajiri wa ya kweli ni wewe kua wa kweli yaani nikua na amani ya moyo inatosha.
Japo ni ngumu ila huu ndio ukweli.
Ndio ukweli huo. Ilimradi unapata furaha yatosha.
Unavyojishikiza kwenye material things unaijinasua kwenye spiritual things..
Any Question so far.?
 
"Ukijitambua utajua kusudi la maisha yako na maisha yako utayaona yana maana kubwa. Hivyo basi tusikilize sauti ndogo iliyo rohoni mwetu inayotoka kwa Mungu inatuambia kusudi jema la maisha yetu, tukishajua kusudi letu tutajitambua na maisha yetu yatakua yenye maana kubwa hapa duniani"Hapa pamebeba kila kitu,huwa nafurahi sana unapotumia terminology za computer,kama "Shetani kashafunga Firewall na Virus kibao kwenye mwili, mwili unakataa request za kutekeleza yale mema roho inayotaka unakua unaprocess request za kwenda kufanya yale mwili upendayo kama starehe. Cha kufanya ni kuinstall Antivirus za maombi na matumaini kwa muumba wako"Umeniongezea kitu kingine kwenye maombi yangu ya kila siku,kuomba Mungu anijalie nijue kusudi langu hapa duniani,Ubarikiwe sana mkuu Da'Vinci ...
 
Ahsante sana mkuu. Stephot hope ww u mtaalamu kwenye masuala haya ya Computer
 
Mimi huwa kuna nyakati huwa inatokea nataka kufanya au kuwaza jambo baya,kunakuwa kama kuna sauti inaniambia acha unafanya jambo baya,sasa unakuta nimelipania kweli nilifanye hilo jambo mpaka unakuta saa nyingine kweli nimelifanya,sasa utakuta kuna hali inaendelea kunisakama sana kuwa unafanya jambo baya ,haitaniachia hata kama ni siku mbili au tatu mpaka napoteza Amani,ila pale nitakapoamua ngoja niache na kutubu na kusema nimeamua kuacha ndio unakuta siisikii tena na pale ndio nakuta ninapata amani kwani muda wote huo inakuwa kama inanizonga kuwa nilichofanya au ninachofanya ni kibaya,nifafanulie hapo mkuu...
 
Uzi umenifanya nipoteze kitu changu nilichokihitaji
Inauma😒😒😒😯
 
Hujanielewa bado namaanisha hivi Kama 1+1=2
Usahihi wa hicho unachokiona hapo Ni mantiki zilizosimama hapo.. moja inasimama kama alama ya kuelezea kitu kimoja,jumlisha imesimama kama nyongeza(kuongeza) na sawasawa imesimama kama kiunganishi cha mantiki ya swali na jibu ambalo ni 2..
So hapo ni sawasawa ni nimekuuliza kwanini 1+1 jawabu liwe 2..?!
So inamaana nahitaji usahihi wa jibu lako ambapo itakupasa ueleze mantiki ya 1+1 kuwa 2!!

So nini usahihi au usahihi unatoka wapi wa kuwa lengo letu la sisi kuishi ni kumuabudu Mungu..?????
Ngoja nikuwekee hivi
Lengo la sisi kuishi + Mungu= kumuabudu Mungu..

Naomba usahihi wa hilo jibu..??
 
Swali lako la kwanza ndio ulilokuwa unatakiwa ulielezee kama njia ya kunijibu Halafu haya yanayofuata yatajibika nitakapo weka mtazamo wangu..
 
Mate
Data bank yako inapenda kuhifadhi clear data...Haitaki kuweka Viruses ndani ya server zake.

Pindi Viruses zikiingia kwenye server yako zinafanya Server yako inakua nzito. Inashindwa kuchakata Information ipasavyo.. HHivyo itakua inastuck stuck katika uchakataji. Kinachotakiwa sasa happ ni Kuformat server zako na kuanza upya ikiwa safi.. na ujitahidi kufungua Strong Anti-Viruses software ili viruses wasiweze kuingia kushambulia sever zako

(Server_Roho)
(Anti virus Maombi na kusali)
(Kuformat ni kutubu)
 
nisiwe na maneno mengi sana ila niwaambie kitu maisha hayana maana yeyote endapo utakosa sehemu ya kuyaweka hilo limekua likiwasumbua wengi sana hivyo kujikuta wapo na matabaka ya imani na vitu vingine life ni meaning less hayana maana wala kusudi kama yana kusudi hebu niambie kuhusu maisha ya wanyama kwa maana hiyo hayo makusudi tunajipa sisi ili tupate tu cha kufanya

msomaji ntaanza kua nachangia maada nimechoka kua msomaji tu
 
Unataka kujilinganisha na wanyama.?
Unajua kama unamshimda hadhi malaika.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…