Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #121
Kahollya,So what why debate the past...elimu dunia umeikataa na kuwashauri wengi wenu kuipinga lakini ndo inayokufanya u survive na kuitumia kueneza ujinga wako. Said bora ukalime maana unatumia ushawishi usiyo kuwa na tija...ajenda yako ni kuiaminisha dunia kuwa waislamu wamekuwa wahanga wa utawala wa Nyerere...kitu hiki siyo kweli...mpaka leo performance yenu waislamu mliowengi ni doubtful kila nyanja...mfao kikwete na magufuli ni nani amekuwa rais bora? utamduni wenu na uislamu wenu ndo kikwazo wala msisingizie watu wengine kama Baba wa taifa. ...soma kwa makini vitu unavyoviandika na kwa watu wenye akili ndogo kama waislamu ndi wanaweza kuviamini..rhetoric only understood by iliterate people.. utaeleweka zaidi kwa waislamu wenzio tena waliyokataa ellimu dunia na leo wanaishi kulaumu wengine...elimu ya madrasa ni upuuzi ikiwa haitalenga wakomboa kifikra...unahitaji ukombozi ndugu...
Huna sababu ya kunitukana kwani mimi sijakutusi.
Nilichofanya nimenyambua kurasa kwenye kitabu cha Prof. Malima ninachoandika.
na kukiweka hapa.
Why debate the past?
Why not?
Elimu dunia tumeikataa?
Umepata wapi hiyo?
Au hujui kuwa Waislam walitaka kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968 chini ya EAMWS
na jiwe la msingi likawekwa lakini mradi ukahujumiwa kwa Nyerere kuipiga marufuku
EAMWS?
Ukipenda kujijua historia hii nifahamishe.
Mimi naeneza ujinga!
Mimi nimechapwa na Oxford University Press mara kadhaa na vitabu vyangu vinasomwa
kote.
Au hujui hili?
Nalo ungependa nikuwekee hapa nimeandika nini?
Sasa jikague mimi na wewe mjinga ni nani?
Wewe umejaa matusi matupu na ushahidi ni hii post yako ninayojibu.
Elimu ya madrasa ni upuuzi...
Hii umepata wapi?
Mimi ni zao la elimu hiyo na wala si mpuuzi.
Wewe mwenye hiyo elimu isiyo ya madrasa uko humu unatoa matusi na lugha zisizo pendeza.
Hebu jipekue tena ujitazame hiyo elimu unayoisifia imekufaa nini.
Je ungependa nikupe historia ya waliosoma elimu ya madras akina Sheikh Hassan bin Amir,
Iddi Faizi Mafongo, Sheikh Sulieman Takadir, Sheikh Mohamed Ramia na wengine
wengi unajua hawa ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika bega kwa bega na Nyerere
na ndiyo walioijenga TANU?
Usiwe mtu wa kuropoka ovyo.
Tuliza kichwa chako soma na jifunze adabu.