The last days of Prof. Kighoma Ali Malima, July/August 1995

The last days of Prof. Kighoma Ali Malima, July/August 1995

Diranghe,
Si uungwana kumwita mtu ''wewe'' khasa akiwa ni mzee.
Nimeandika mengi na nimechapwa na ''publishers'' kadhaa.

Sijapata hata mmoja kunambia kuna ''negativity'' katika fikra
zangu.

Wengi wamenichapa na nimetoa mada nyingi kwingi kwa
kuwa kila mara nilikuwa nakuja na kitu kipya,

Sijapata kuandika malalamiko.

Mimi nimeandika sana katika historia ya Tanganyika na yale
yaliyotokea.

Ingekuwa mimi nachafua Uislam, Waislam wenyewe wangeniasa.
Uliitaka nikuiteje bila kusema "wewe"? Hiyo hoja yako ya kusema wachapaji hawakukupinga kwa uchapaji wako ni ya kupuuzwa. Jiulize ni magazeti na vitabu vingapi vimeshawahi kufungiwa na mamlaka husika wakati wachapishaji walishafanya kazi yao? pia kusema kwamba hadi waislamu wenzako wakuase ndo uone unachofanya sio sawa ni dalili mbaya ya roho ya ubinafsi na ubaguzi. Badilika wewe mzee.
 
Mtoto aliyelelewa vizuri hawezi kumwita mzee ''wewe.''
Ikiwa hata baada ya kukuasa unashikilia kuwa mtovu
wa adabu basi liko tatizo katika malezi yako.

Vitabu vyangu vyote viko nchini na hakuna hata kimoja
kilichopigwa marufuku.

Narudia kukufahamisha kuwa Waislam wamefarijika na
juhudi zangu za kuiandika historia yao.

Ukitaka tujadili ''roho mbaya'' na ''ubinafsi'' fungua uzi
nije nikupe darsa pampja na rejea zenye uthibitisho ili
uwatambue wenye ''roho mbaya'' na watu ''wabinafsi.''
 
Bora ulivyoweka wazi harakati zako ni kutetea uislamu sio nchi ya Tanzania. Uislamu ni dini safi yenye heshima yake na kuna waalimu wengi wa kiislamu wanaoelezea dini vizuri kwa njia salama na ya kueleweka sio kama wewe hadi umponde Nyerere na kuishia kulalamika. Nakushauri ujifunze kwa waalimu wengine ambao hadi mimi nimetambua uislamu hauna tatizo kwa njia za amani tu. Kuiponda serikali haitakusaidia mzee Mohamed.
 
Kidogo sasa unaanza kuelekea.
Sasa mjadala unaanza.

Naomba unionyeshe mahali katika maandishi yangu ambako ''nimemponda''
Nyerere.

Sijapatapo kulalamika.
Mimi huandika na kueleza kile ninachoamini huu si ulalamishi.

Mimi mwalimu wangu ni Maalim Haruna na sasa ni marehemu.

Yeye ndiye aliyenifundisha mbinu za mnakasha yaani majadiliano na fani
nyingine kama mantik yaani logic.
 
Saidi you are bogasssss....
Kahollya,
Naamini umekusudia neno la Kiingereza ''bogus.''
Maana ya neno hilo kwenye ''dictionary'' ni ''pretending to be real.''

Mimi ndiye huyu Mohamed Said unaemsoma hapa sijajifanya kuwe
siye.

Ikiwa sijakuelewa na ''bogassss,'' tafadhali nifahamishe.
 
Wengi humu mnabishana na mzee Mohammed Said kama mpo kijiweni. Amewazidi maarifa mengi. Lugha pia amewazidi. Iwe ile ya malkia au hii ya mama mzazi. Mnamkosea adabu lakini hachukii. Anawajibu kwa hoja sio vioja kama wengi wenu mfanyavyo. Mkitaka kumuweza huyu mzee sharti nanyi muwe nondo kidogo kwenye mjadala. Vinginevyo nikionacho mna mpa maksi za bure tu. Akitoa hoja nanyi mpingeni kwa hoja, akitoa kioja nanyi mpingeni kwa kioja. Kawashinda huyu. Mwanakijiji mwenye hoja nyingi jukwaani hapa nilishaona alishindwa kukabiliana nae.
 
Hizi historia kila siku ni Nyerere tu na uislamu ,sawa alifanya makosa ,ila Mwinyi alipochukua kiti kama Rais alifanya nini kuondoa Makosa ya Nyerere na uislamu ??
Ni vigumu kwa Mwinyi kuondoa makosa yaliyokomaa kwa miaka 24 ya utawala wa Nyerere (1961-1985) wakati Rais Mwinyi alikuwa madarakani kwa miaka 10 tu! tuwe tunafikira jamani...
 
Ni vigumu kwa Mwinyi kuondoa makosa yaliyokomaa kwa miaka 24 ya utawala wa Nyerere (1961-1985) wakati Rais Mwinyi alikuwa madarakani kwa miaka 10 tu! tuwe tunafikira jamani...
Miaka kumi ni mingi inatosha kurekebisha. Kujenga ndio kazi kubomoa na kurekebisha ni rahis. Huoni Magufuli anarekebisha makosa ya Mkwere.
 
Ni vigumu kwa Mwinyi kuondoa makosa yaliyokomaa kwa miaka 24 ya utawala wa Nyerere (1961-1985) wakati Rais Mwinyi alikuwa madarakani kwa miaka 10 tu! tuwe tunafikira jamani...
Acha siasa hapa ,ugumu wake ni nini ?? Ameshindwa Mwinyi ,Jakaya kafanya nini ??
 
Acha siasa hapa ,ugumu wake ni nini ?? Ameshindwa Mwinyi ,Jakaya kafanya nini ??
Mwinyi hakushindwa yeye ndio mwana mageuzi mkuu,
Mwinyi aligeuza sera mbovu za uchumi na siasa na uhuru wa binaadamu upside dowm...mwinyi kwa aliuangusha na kuobomoa mfumo...
Alitupilia mbali siasa chakavu za ujamaaa
Alifungua uhuru wa habari kwa kuruhusu TV , Radio na Magazeti huru
Aliachana na siasa za fikra za mwenyekiti na kifalme
Akafuta kabisa kujipanga foleni rais akitokea mbeya,,,
Kwa kweli alofanya ni makubwa mnoo tena muda mfupi tu
 
Ila kwa hali tuliyofikia kwenye nchi hii hatutaruhusu tena kumpa urais mtu jamii ya Mwinyi na Kikwete. Hawa wawili tuliwajaribu inatosha. Nimekosea jamani?
 
Ni kweli saidi hakuna anaeweza kumshinda kwa kupandikiza maandiko yanayopelekea chuki miongomoni mwetu...mfano mimi nimejikuta pia nimeingia katika mtego huo,,,nikamchukia..na hata hizo takataka zake nimekoma kuzisoma..sasa nitamshambulia kwa ujinga na ushetani wake.
 
Ila kwa hali tuliyofikia kwenye nchi hii hatutaruhusu tena kumpa urais mtu jamii ya Mwinyi na Kikwete. Hawa wawili tuliwajaribu inatosha. Nimekosea jamani?
Kama unatoa wewe urais sawa....ila tunawahitaji hao sana....ikifika miaka 5 ndo tutajua sasa hivi ni vigelegele
 
Wengi humu mnabishana na mzee Mohammed Said kama mpo kijiweni. Amewazidi maarifa mengi. Lugha pia amewazidi. Iwe ile ya malkia au hii ya mama mzazi. Mnamkosea adabu lakini hachukii. Anawajibu kwa hoja sio vioja kama wengi wenu mfanyavyo. Mkitaka kumuweza huyu mzee sharti nanyi muwe nondo kidogo kwenye mjadala. Vinginevyo nikionacho mna mpa maksi za bure tu. Akitoa hoja nanyi mpingeni kwa hoja, akitoa kioja nanyi mpingeni kwa kioja. Kawashinda huyu. Mwanakijiji mwenye hoja nyingi jukwaani hapa nilishaona alishindwa kukabiliana nae.
Ngalikivembu,
Umri ni kitu muhimu sana katika hulka zetu kwani umri unakuwa
ushakupitisha kwingi.

Huku kwingi ni pamoja na kusoma vitabu vingi na kusoma enzi
walimu wakisomesha.

Huwa najitahidi kuwashajiisha vijana katika adabu kuwa mjadala
usiwe mahali pa matusi.

Mimi nimekuwa wakati wanafunzi tukishindana kusoma vitabu vya
kila aina na shule zikilikuwa na maktaba.

Mimi nimelelewa wakati jamii nzima ni walezi.
Mtoto kukosa adabu ni fedheha kwa wazazi wake.

Na yapo mengi...
Nakushukuru kwa mchango wako.
 
Ni kweli saidi hakuna anaeweza kumshinda kwa kupandikiza maandiko yanayopelekea chuki miongomoni mwetu...mfano mimi nimejikuta pia nimeingia katika mtego huo,,,nikamchukia..na hata hizo takataka zake nimekoma kuzisoma..sasa nitamshambulia kwa ujinga na ushetani wake.
Kahollya,
Sina maandiko ya chuki.
Lete ushahidi wa andiko langu moja lenye chuki Majlis ione.

''Takataka,'' zangu ni hizi hapo chini nakuwekea uone ni nani
wananialika kuzungumza na ni wachapaji gani wanachapa hizo
''takataka'' zangu.

Hii ni jibu tosha kwako:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
2. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press 2006, Nairobi. (Children’s book).
3. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
4. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
5. Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
6. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
7. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
8. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
9. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
10. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
11. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
12. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
13. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
14. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA)Morogoro 11th April 2004).
15. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
16. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.
17. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg. The paper was also presented at Islamic Propagation Centre International (IPCI) Durban.
18. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.

Visiting Scholar: (2011)
University of Iowa, Iowa City, USA
Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin, Germany.

Kahollya,
Umenitukana kwa kuniita ''mjinga'' na ''shetani.''

Sijui nini kimekukasirisha kiasi hicho lakini naamini ukitulia utarejea katika
mjadala bila matusi.
 
Mzee Mohamed hayo machapisho yako ni ya kuwateka wajinga waone uislam unaonewa ndani ya Tanzania. Mimi nayachukia sana maandiko yako ya kipotoshaji. Kuna nyakati gazeti la Raia mwema hunikosea sana kwa kuweka makala zako zisizoeleweka.
 
Ikiwa unayachukia maandishi yangu yapite usiyasome utakuwa umesalimika
Raia Mwema wananichapa kwa kuwa makala zangu zinavutia wasomaji wengi.

Kuwa sieleweki si kweli.
Nina fasaha ya kutosha katika lugha ya Kiswahili.

Hili la ''kuonewa,'' sijui msamiati huo kama uko katika maandishi yangu.
Sikumbuki wapi na lini nimeandika neno hilo.

Vyuo Vikuu vyote nilivyohadhir Marekani, Afrika na Ulaya kuna wajinga?
 
Back
Top Bottom