Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 182,097
- 1,099,383
Siku hizi nikiona maandishi yako wala sihangaiki kusoma. Najua kuna chuki kali kwa Nyerere na mfumo Kristo na jinsi ulivyoonea Waislamu. Hii ndiyo constant pekee katika maandishi yako mengi (hapo juu). Cha ajabu hata hutoi any suggestions au masuluhisho ya kuwakwamua waislamu wenzio. OK, Prof. Malima aliuawa na Nyerere na mfumo Kristo then what? Tufanye nini sasa hasa ukizingatia kuwa Nyerere mwenyewe naye alishakufa? Unataka Waislamu wafanye nini? Na Wagalatia (makafiri) nao wafanye nini? UNATAKA NINI?Shimba...
Tutakwenda hatua kwa hatua In Shaallah.
''Maandishi yangu yote...''
Hata mimi mwenyewe sijui nimenadika kiasi gani ukiacha vitabu na ''papers.''
Nakuwekea hapa chini baadhi ya machapisho yangu uangalie ni ngapi Nyerere yumo:
PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
2. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press 2006, Nairobi. (Children’s book).
3. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
4. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
5. Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
6. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
7. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
8. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
9. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
10. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
11. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
12. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
13. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
14. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA)Morogoro 11th April 2004).
15. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
16. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, and Nairobi.
17. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg. The paper was also presented at Islamic Propagation Centre International (IPCI) Durban.
18. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.
Sasa tuje kwenye ''mtu hatari...''
Miaka yote hiyo naandika nahadhiri, nachapwa na ''publishers'' ndani na nje ya nchi ''mtu hatari,'' naalikwa kwenye mikutano, nakwenda kwenye vyuo kama ''visiting scholar'' ''mtu hatari...''
Umeniuliza nini lengo langu.
Kila kitabu, kila ''paper'' niliyoandika ina lengo lake maalum sitoweza hapa kukueleza yote ila nitakwambia kuwa kitabu cha Abdulwahid Sykes lengo lake lilikuwa kuonyesha mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Historia hii ilikuwa imefutwa kwa kukusudiwa.
Ukitaka ushahidi wa hilo na mengine fungua uzi makhsusi.
Angry person?
Soma unavyoandika na nisome mimi kisha jiulize nani anaandika ameghadhibika.
Au ukipenda tunaweza kuwaachia wanaukumbi watuamue.
Unazungumza kuhusu chuki.
Ushamsoma P van Bergen (1981), Sivalon (1992), Njozi (2002) wanasema nini?
Kuhusu ''Taliban'' wapi nimesema ni sifa mbaya?
Nilichokueleza ni kuwa umenipa jina ambalo si langu.
Waingereza wanasema, ''name calling.''
Naamini unatambua kuwa watu hapa JF hupewa ''kifungo'' kwa kosa la ''name calling.''
Look. Uislamu wa kweli naujua na nimefaidika nao sana. Na mimi ni MTETEZI mkuu wa Uislamu hasa katika jamii ambazo hazina imani nao. Pale Stanford University niligombana na watu wengi nikitetea Uislamu kuwa ni dini ya amani na upendo kwa sababu wema huu na upendo huu wa Waislamu nimeuona na sijasimuliwa.
Tatizo la uislamu kwa sasa (inawezekana na dini zingine katika vipindi tofauti) ni kutekwa na watu wachache na kuanza kutumiwa kwa maslahi binafsi. Kila Mwislamu wa kweli anakubali kuwa uislamu unaohubiriwa na Al Qaeda, ISIS, Boko Haram, Al Shabaab na magaidi wengine siyo uislamu wa kweli. Uislamu wa kuua wanawake na watoto; na watu wengine wasio na hatia.
Nasikitika kusema kwamba hata wewe unaingia katika upande huu. Juhudi zako hizi za kujaribu tena bila kuchoka kueneza chuki non stop siamini kama ndiyo uislamu wa kweli. Unautumia uislamu tu kwa faida zako za kibinadamu na hata ujaribu vipi kujificha katika uanahistoria na usomi watu makini bado tunaweza kuona unachojaribu kufanya. Na kama nilivyosema acha tu waendelee kukuchekea na kukusifia eti unafanya investigative history wataona utakakowafikisha siku moja.
Jaribu sana angalau kutoa mwongozo. Ndiyo Waislamu wameonewa sana na Nyerere na Mkapa (na wakafaidika sana na Mwinyi na Mrisho), sasa nini kifanyike? Hapa chini nakuwekea angalizo kuhusu matokeo mabovu ya kidato cha nne katika seminari nyingi za Kiislamu. Toa angalau mwongozo jinsi seminari hizi zinavyoweza kuboresha elimu na kuhakikisha vijana wake wanafaulu vizuri. Hii itasaidia zaidi kuwainua Waislamu mara bilioni kuliko kuwaambia tu Kigoma Malima wetu aliuawa na Nyerere halafu huwaambii wafanye nini. Allah Akufungue moyo wako uhame kabisa kutoka upande wa giza ili ukawe kurunzi itakayowaonyesha njia Waislamu wapendwa wa Tanzania hasa katika kipindi hiki ambacho uislamu wa kweli umetekwa na magaidi. Molla na Akusaidie na hata usiponisikia tena KAMWE usijivike kiburi cha usomi na kuusahau ushauri huu wa kibinadamu na kizalendo. Maisha ya watu wengi sana yako mikononi mwako kupitia kalamu yako hiyo inayotema sumu kali bila kuchoka.