The New York Times lasambaza uongo Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, ladai haukuwa huru na wa haki. Je, ni kweli tunyamaze, au uongo tukanushe?

Ulianza kama swali na umemaliza kama swali, lakini katikati umejibu maswali yote uliyoyauliza. Tubaki tu na majibu yako inatosha. Sasa tujenge nchi.
 
Kwenye hilo andiko uliloambatanisha sijaona uongo unaousema. Tatizo lako Pascal umepoteza uwezo wako wa "objectivity" kutokana na ushabiki. Jaribu kujirudi kidogo.
 
Nakuelewa Sana Pascal unavitu vingi vya kuongoe ila ndio hivyo ni kama umejazwa maji mdomoni umebaki kuongea kwa ishara.

Maana ukifafanua vyema utaambiwa umesambaza habari ambayo haijadhibitishwa na mamlaka sheria ya mtandao itakuandama.

Zaidi nimependa ulivyojipa mamlaka ya usemaji wa TCRA kwamba mtandao ulizidiwa kutokana na Watanzania wengi kufuatilia Uchaguzi hivyo kupelekea mtandao kuwa chini, japo hakuna mamlaka iliyotoa kauli ya kueleweka mtandao kuwa down.

Hofu yangu serikali itaanza kuchunguza nani Mwandishi wa hizi makala kama ilivyokuwa kwa Kabendera, halafu lawama zitarudi kwako kuwa umemchomekea... wakati wewe lengo lako zuri tu kuwapasha Watanzania dunia inavyotuona.
 
Kwa nini katika history ya nchi yetu tunaishi Kwa mashaka sana?

Mbona kabla Magufuli hajawa Rais tulikuwa hata hatujulikani ughaibuni!

Mtu mwenye akili anatakiwa aende kwenye kioo kujitazame kuliko kupuuza kila kinachosemwa

Sadam Hussein alikua na Scud pamoja na makombora mengi sana lakini Kwa dhulma alizowafanyia wakurdistan siku moja alitolewa kwenye shimo kama paka na akanyongwa hadharani huku viombo vya Habari vikiwa LIVE

Kuna mtu anacheza na damu za Binadamu Kwa kusingizio ni Wazanzibari au wasaliti mpe muda Hao mabaunsa wake watajamkimbia

Albashir yupo jela baada ya kukamatwa kitu cha kwanza alisema hii ni Kwa sababu ya dua za nilizo wadhulumu

Kuna mtu hajifunzi Dawa yake inachemka
 
Pascal, kwako kuna mambo mawili inawezekana kweli ukawa umeunga jitihada mkono au imekuwa ukiipiga CCM fimbo kwa kupitia mgongoni wenye akili wamesha kugundua.
 
Pascal Mayalla, Acha kutafuta upendeleo toka Kwa Magufuli, Kwa kutoa ushuhuda wa uongo.

BIBLIA ina kuonya hapa:

"Watu wengi hutafuta upendeleo wa mkuu; Bali hukumu ya kila mtu hutoka kwa Bwana" (Mithali 29:26)

Pascal, Acha kishi Kwa kumtegemea Mwanadamu kwani yeye naye iko siku atakutana na mkono wa Mungu.

BIBLIA ina onya:

"Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana." (Yeremia 17 :5)
 
Hakuna uwongo hapo, walichoandika ni ukweli mtupu. Kituo nilichopigia kura mimi wakala wa Chadema alizuiwa katakata kuingia ndani, hii nimeona kwa macho yangu kabisa sijaambiwa na mtu! - Sasa uchaguzi gani huo!
Pascal Mayalla Mungu akurehemu. Yaani huu uchafuzi unasema ulikuwaje? Mauaji, kura feki, wizi wa kura, kupigwa wapinzani, kutekwa etc vimekufurahisha Hadi unatetea hasharani?
Kile ulichomfanyia Eric Kabendera kitakutesa hadi mautini
 
Hata trump anadai uchaguz wa Marekana haukua huru na haki ivyo hata wao ni Sawa na chadema tu wasitutishe
 
Uchaguzi Tanzania haukuwa wa huru na haki. Wewe unaesema ulikuwa wa huru na haki ndio muongo. Na kama ungekuwa huru na haki, sirikali isingetumia risasi za moto kwa raia wake, kuteka na kuwatesa watu. Ukhanithi mkubwa sana kuona kikosi cha kulinda amani kinapita njiani na kuparaza Jembe ili kutisha wananchi. Tumeshindwa kujua tofauti ya Polisi mlinda raia na akina alshabbab.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…