kamili
JF-Expert Member
- Feb 10, 2011
- 1,217
- 853
Baada ya takwimu hizi ungetupa conclussion yako mkuu kuonyesha ulilenga marekani isiongee nini na hizo takwimu zimeongea nini, mfano ulitaka kumaanisha utawala ulikuwa mzuri au mbaya kwa mujibu wa takwimu au marekani wamevuruga nchi iliyokuwa inastahili kuvurugwa nk nk.
Utawala wowote huhukumiwa kwa takwimu na wala si vinginevyo. Nimeona kuna mijadala mizuri inaendelea hapa. But wale wanaoamini Gadaffi amepata alichostahili hawatuoneshi wapi alipoboronga, maana demokrasia si kubadilishana madaraka tu kila baada ya miaka mitano, na hivyo kila anayeingia anatoka mifuko yake imetuna na kuwaacha wananchi wake wengi wakiwa hali mbaya. Na ndio maana malkia wa Uingereza ameingia madarakani mwaka 1959, na Uingereza haina katiba iliyoandikwa lakini kwa kuwa watu wake wanahudumiwa vizuri hatujawahi kusikia uingereza kuna vita ya kumtoa malkia. Kwa mfano Tanzania kuna demokrasia lakini mwalimu moja anafundisha watoto 53, kwa Libya mlm moja wanafunzi 8, au Tz DR. moja anahudumia watu 44133, Libya ilikuwa DR. watu 775 kwa mwaka.
Lakini pia wale wanaosema Gadaffi ameuwa watu hawajatupa takwimu, kwa sababu hata TZ watu waliuawa 2001 na 2011 na huenda mauaji yakaendelea Kwa sababu wale waliouwa walipewa vyeo badala ya kushtakiwa, (MUNGU APISHE MBALI)( kumbuka ni mahakama pekee ndio ina haki ya kuhukumu kifo.)
Saddam aliuwa watu wapatao 2000, lakini ili kumtoa madarakani Marekani na washirika wake waliua zaidi ya watu 500,000. Na baada ya kumyonga Saddam wamekufa wengi zaidi kutokana na mabomu ya wanaojitoa mhanga, njaa, na maradhi. Tukumbuke fedha za Iraq kwa sasa zinalipia vita pamoja na makampuni ya wakandarasi wa kigeni wanaoijenge upya Iraq kwani majumba, barabara na madaraja yalitwanga na Nato bila huruma wakijua ni dili la baadae.
Ni kweli baadhi ya Wairaq hawakumpenda Saddam kwa Ubabe wake lakini kwa sasa wanajuta maana kuna watu watakufa bila ya kuonja raha ya kuzaliwa Iraq.
Lakini pia tunasahau wauwaji wakubwa wa Africa walikuwa wamepata baraka kutoka kwa mataifa ya Magharibi, eg Makaburu wa SA, RENAMO ya Msumbiji, Jonas Savimbi wa Angola, Mabutu wa Zaire, Intarahamwe ya Rwanda nk.
Hitimisho langu ni kuwa Gaddafi alipaswa aondolewe madarakani kwa mbinu ambazo si za kumuua kikatili vile. Kama wauwaji wa SA au wa Rwandwa waliweza kukamatwa na kupelekwa mahakama ya kimataifa kwa nini kwa Gaddafi halikuwezekana.