Peter Madukwa
JF-Expert Member
- Sep 20, 2012
- 3,139
- 2,488
Aliyekuwa mbunge wa Iringa mjini kupitia CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa amempongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kazi uzuri na ubunifu wa Filamu maarufu ya kitalii ya THE ROYAL TOUR.
Kiongozi huyo wa CHADEMA wa nyanda za juu kusini amesema kuwa inawezekana labda kuna mapungufu madogomadogo lakini kimsingi kazi aliyoifanya Rais Samia Suluhu Hassani ni ya KIZALENDO na inahitaji kuungwa mkono na watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa kwa kuwa hata yeye mara kadhaa akiwa bungeni mara kadhaa ameshauri kutumika kwa nguvu ya ziada kuitangaza Tanzania na vivutio vya utalii.
Filamu ya The ROYAL TOUR ni filamu ya kihistoria inayoelezea kuhusu vivutio mbalimbali vya utalii vya Tanzania ambayo iliandaliwa na muandaaji Maarufu wa filamu PETER JOHN GREENBERG kutoka nchini Marekani.
Filamu hiyo mpaka sasa imezinduliwa ktk majiji makubwa matatu.. Jiji la LOS ANGELS na NEW YORK USA, Pamoja na jiji la kitalii ARUSHA, TANZANIA.
Filamu hiyo maarufu ya kitalii inatarajiwa kuzinduliwa ktk mji wa kihistoria wa Zanzibar na jiji kubwa la kibiashara DAR ES SALAAM.
ROYAL TOUR inatarajiwa kuleta matokeo makubwa ktk sekta ya utalii nchini Tanzania na kuongeza mapato yatokanayo na utalii.
Filamu ya The Royal Tour inapatikana ktk mtandao maarufu wa amazon.com na inatarajiwa kuoneshwa ktk vituo lukuki vya television duniani.
Hongera Mchungaji Peter Msigwa kwa kuweza kuchuja pumba na mchele na kutambua kuwa kuna tofauti kati ya itikadi za kisiasa linapokuja suala la ujenzi wa nchi yetu japo tegemea kushambuliwa na wafuasi mbalimbali wa upinzani kwa kuwa sera za chama chako haziamini ktk kupongeza jambo zuri linapofanywa na serikali lakini umeonesha ukomavu wa kisiasa...
MAMA SAMIA IMARA; KAZI IENDELEE👋🇹🇿