Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Mchungaji Msigwa
Nipo katika rekodi nikikutetea kuhusu sakata la Ngorongoro. Nilisema una haki ya kutoa maoni kama Mtanzania na kiongozi uliyeongoza shughuli za chama chako Bungeni
Niliwashauri wanaotaka usiseme waache kwani demokrasia ina upana na gharama zake ikiwemo kuvumiliana kwa misimamo tofauti nikitoa mfano wa Democrats kule US na Conservatives UK
Kwa hili la Royal tour nipo katika rekodi nikisema ' kilichofanyika kina nia njema' tatizo linalowasumbua watu ni jinsi gani imefanyika. Nilipongeza mjadala wa mawazo tofauti
Leo Msigwa unaandika kwamba viongozi wenzako hawajui utalii. Una haki ya maoni lakini maoni hayo yana stara zake. Kutofautiana kimawazo hakufanyi wewe au wenye mitazamo tofauti wawe wajinga. Kwa hili unawakosea wenzako! Omba radhi
Pili, ukiandika na kusema huogopi kuitwa hata kabla ya tendo kutokea ni self defense.
Katika mazingira ya kawaida halifai, tumia uhuru wako hadi vinginevyo si kujenga 'uncertainty'
Picha unayoipaka kwa wenzako si nzuri na hulazimiki kujitetea pasipo na tuhuma! unahofia nini?
Tatu, mawasiliano kati yako na wenzako ni yenu si kila mawasiliano ni 'for the public consume'
Lakini kama unaona kuna mazingira usiyoyapenda kwanini usijiweke huru bila kusubiri kibali cha kutumia kinywa chako au kutumia kinywa chako kwa hofu!
Fundi Mchundo JokaKuu Pascal Mayalla
Siku hizi anatoa maoni tofauti na wenzake wa chama, kisha anasema haogopi kufukuzwa chama! Unajua maana yake ni nini, tayari anataka kwenda ccm ila anaona aibu kwenda moja kwa moja, hivyo anatengeneza mazingira ya kufukuzwa ili aonekane kafukuzwa. Cdm wakitaka kumpatia inabidi wasimfukuze bali wampotezee lazima ataondoka kwa aibu.