The Royal Tour: Mchungaji Peter Msigwa wa CHADEMA ampongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kazi nzuri


Siku hizi anatoa maoni tofauti na wenzake wa chama, kisha anasema haogopi kufukuzwa chama! Unajua maana yake ni nini, tayari anataka kwenda ccm ila anaona aibu kwenda moja kwa moja, hivyo anatengeneza mazingira ya kufukuzwa ili aonekane kafukuzwa. Cdm wakitaka kumpatia inabidi wasimfukuze bali wampotezee lazima ataondoka kwa aibu.
 
CHADEMA haiwezi kumfukuza, ni Chama cha Kidemokrasia na moja ya nguzo zake kuu ni uhuru wa kutoa maoni (bila kuathiri haki za msingi za wengine). Anajistukia tu, unless kama anautaka Uenyekiti.
Historia inawahukumu

Rejea kufukuzwa kwa Zitto
 

..Naamini kuna mchangiaji amepotosha maelezo ya Peter Msigwa, mahojiano kamili yako hapa chini.

..Na hakuna mahali amezungumzia kumpigia simu Tundu Lissu.

..infact amesema anakubaliana namna Lissu anavyotoa challenge ya kutaka taarifa zaidi kuhusu Royal Tour.

..Msigwa pia ameeleza kwamba anakubaliana na baadhi ya hoja za Lema kuhusu approach iliyotakiwa kuchukuliwa kuitangaza nchi.

..amefafanua kwa kirefu kwamba anapingana na wale ambao wametoa hukumu kwamba kuna ufisadi, amesema yeye bado hajauona.

..sasa mtu aliyetoa maelezo hayo ataitwa vipi kwenye "kamati ya maadili"? mimi sijawahi kusikia Chadema wana kamati ya maadili, mara nyingi wanachama wao husulubiwa ktk Kamati Kuu.

 
Ahsante Mkuu

Nilisoma maoni huko tweeter halafu nikaona hapa JF
Nadhani angejitokeza au ange tweet kukanusha
 
Jambo jema but pengine hakukuwa na ulazima wa kuigiza yeye✍️
 
Nimemsikiliza Msigwa na naona ni kama amewekewa maneno. Ila kuna umuhimu wa yeye kuwa muwazi na kuya own yale maneno au kuyakataa.

Tofauti na ilivyokuwa kwenye suala la Ngorongoro, kwenye hili sikubaliani nae. Naona amekosea kwa kuwataka wenzake wote waikubali hii Royal Tour. Kwa kufanya hivyo anakuwa anawafunga mdomo. Kwa vile sidhani kama yeye atakubali kufungwa mdomo basi awaachie wenzake waseme. Cha kudai ni sababu zao za kupinga Royal Tour.

Mimi sikubaliani na tour kwa sababu zifuatazo:
1. Value for money. Sidhani kama hii ni the most cost effective way ya kuwavuta watalii. Haya mambo ya matangazo kwenye TV yamepitwa na wakati. Siku hizi social media ni much more effective. Tweet moja ya influencer katika social media itaangaliwa na mamilioni zaidi ya watakaokodisha documentary Amazon. Kuliko PBS bora wangewaomba wakina Netflix, HBO, Disney n.k. watayarishe contents ambazo watazistream kwenye app zao. Kukodisha bango Time Square na kumweka Ronaldo au Messi itakuwa ni kutupa hela chooni maana hawana huo mvuto Marekani.
2. Gharama za launching nazo hazi make sense. Hivi kweli the only "celebrity" waliyeweza kupata ni baba ya Rihanna? Kwa nini hawakumbembeleza Lupita Nyong'o? Au Daniel Kazuya? Hatuwataki kwa sababu ni wakenya na waganda? Hii inanipeleka kwenye point yangu ya 3.
3. Hii ngoma ya kusema kuwa watu wanadhani Mlima Kilimanjaro uko Kenya imepitwa na wakati. Tunatakiwa tuanze kushirikiana katika kutangaza nchi zetu. Kuna ubaya gani kuuza Afrika Mashariki kwa ujumla wake? Hivi mtu akija na Kenya Airways, akashukia Nairobi halafu akaja Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro tuna hasara gani? Tunaweza kutumia nyota ya Lupita na Daniel kuwavuta watu waje Afrika Mashariki na sisi tutafaidika maana kila nchi ina uvutio wake.
4. Tumeifanya hii Tour kama magic bullet ambayo itatuondolea matatizo yote badala ya kuangalia kwa dhati kwa nini watalii hawaji Tanzania ( sio kwa sababu ya Kenya). Huduma zetu zikoje? Je mazingira yetu ni rafiki kwa watalii ( nilizungumzia unyanyasaji tunaowafanyia wakitaka kupiga picha n.k.). Je tuna hoteli na makampuni ya kitalii ambayo yana global impact? Haya mahoteli na makampuni yanaweza kututangaza kuliko tunavyojitangaza wenyewe.
5. Usalama ukoje nchini mwetu? Tusidharau haya mambo ya panya road maana travel advisory moja ya State Department kuhusu hali ya usalama nchini inafuta faida zote za Royal Tour. Jawabu sio kuwalaamu kwa kutoa hizo taarifa bali ni kuhakikisha hao panya road wanabadilisha ajira.
6. Tunahitaji kupanua wigo wa utalii wetu. Tanzania ni zaidi ya Kilimanjaro na Ngorongoro. Kuna watu wanavutiwa zaidi na miji, na historia, na fukwe, na maisha ya watu wa kawaida, na masuala ya mazingira n.k. Tuangalie namna ya kuwarahisishia wao kutimiza ndoto zao. Sio mtu anakuja ili akae na wenyeji halafu tunamtaka anunue special visa ya bei mbaya! Au wanafunzi wanatembelea shule vijijini lakini immigration wanawasumbua ili wapate dawa za viatu.
7. Tuangalie kama ada zetu ni competitive. Tunaweka ada za kuua mtu kuingia kwenye mbuga zetu. Tuwatambue diaspora kama wenzetu ili wawe encouraged kuja na family na rafiki zao kutembelea mbuga zetu.
8. Tuwe wabunifu. Ghana walianzisha Year of Return ili kuwavuta African Americans kwenda kutalii Ghana na hata kuwekeza. Waliwapa masharti nafuu sana kama ndugu zao waliopotea. Kwa nini na sisi tusifanye hivyo? Tuwa target African Americans kuja kujifunza historia.
9. Tuachane na rhetoric za kijinga kama hizi za mashoga. Mashoga wapo na hata tupige kelele vipi haibadilishi ukweli huo. Wao pia ni binadamu kama sisi. State Department ikisema tu kuwa maisha yao yako hatarini wakiwa Tanzania, hawatakuja wao na sympathisers wao. Katika dunia ya leo impact ya kutokuja kwao tutaipata.
10. Tujiulize kwa nini mashirika ya ndege ya kimataifa kama British Airways, Lufthansa n.k. yaliacha kuja Tanzania. Dawa sio kununua ndege zetu.

Zoezi la kuuza Tanzania ni endelevu. Kwa hiyo badala ya kutumia mapesa kibao kwenye tour tungewekeza kwenye vitu ambavyo vitakuwa na impact kwenye maisha ya watu wetu ili wasione kukaba watalii ni dili.

Amandla...

Cc. JokaKuu Nguruvi3
 
"Wata msumaye" bado nacheeeka
 
 
SSH hafanyi biashara haramu ya kununua chadema ,afanye hivyo Ili imsaidie nini?

Ujue nyie Chadomo ni hamnazo kichwani kwenu, endeleeni kupinga tuone mwisho wenu.
Kwani jiwe alikuwa anafanya biashara hiyo? Si mlisema waliounga mkono juhudi wanamkubali uchapakazi wake?
 
Mama anaupiga mwingi

Mch Msigwa ameona siasa za kupinga kila kitu ni za kizamani hazijengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…