The Terminal List: Hii ndiyo series yangu pendwa baada ya PRISON BREAK na 24

The Terminal List: Hii ndiyo series yangu pendwa baada ya PRISON BREAK na 24

Ukawaida wake upo wap umeona jinsi mwamba alivyo tactic hii series nimeangalia episode mbili Tu lakini ni Moto

Movie imejaa akili za kijasusi na mbinu za vita [emoji2937][emoji110]
Hujaangalia bado muvi za mbinu wewe siries nyeupe sana hiyo...

Sema ndo series za kizazi haki ziko simpo simpo sana sababu hata watazamaji hawataki kutumia akili sana kufikiria
 
August 26 na ndio itakua ya mwisho eti [emoji3064][emoji20]
Yaap tu tunausubiria huu mzigo kwa hamu kubwa... mi siku hizi nachagua sana series za kuangalia... kuna sura ukiziona tu kwenye movie au series unajua ni moto wa kuotea mbali
 
Hujaangalia bado muvi za mbinu wewe siries nyeupe sana hiyo...

Sema ndo series za kizazi haki ziko simpo simpo sana sababu hata watazamaji hawataki kutumia akili sana kufikiria

Tupe angalau series 2 ambazo wewe unazikubali.
 
Naitafuta Viking season2 mwny nayo anisaidie tafadhali
 
Baadhi ya wadau walisifia Sana serial ya money heist nikaona isiwe taabu Acha niitafute nione kama hiyo ladha yake itafanana na prison break na 24 lakini cha ajabu humo ndani ilijaa ujinga mwingi na utoto nikaja na Uzi wangu juu ya hiyo movie ya kifala.

Nimeangalia serial nyingi Ila bado Ile ladha ambayo IPO kwenye series zangu pendwa(24 na PB) sikuwahi kupata, nashukuru weekend hii Kwa mara ya Kwanza baada ya miaka 13 iliyopita Jana nimekutana na hii CHOMBO kinaitwa THE TERMINAL LIST hakika hii series ni Tamu balaa ni zaidi ya burudani ndani ya Moyo.

Mara baada ya kupata trauma/ mental disorder iliyosababishwa na vita mbaya akiwa mashariki ya Kati hatimae ananusurika na kurudi salama ingawa Akili yake ineyumba anapata janga lingine la kupoteza familia yake yaani MKE wake na mtoto wake wa kike hapa ndipo Hali yake unazidi kuwa ngumu.. kwbb jamaa alikuwa hajui sababu iliyopelekea kupoteza familia yake wala washikaji zake pia hawajui sababu ya jamaa kupata majanga hapa ndipo utamu WA hii movie unapoanzia.

Sterling wa hii movie JAMES REECE comandoo aliyeiva na kukamilika kila idara anajua kucheza na bunduki huku akitumia mbinu zenye Akili kujua undani WA maisha yake kuwa hatarani ndipo anakuja kugundua shida ilianzia kipindi yupo vitani baada ya kukwanisha dili ambalo wapo viongozi wa serikali,wafanyabiashara wakubwa na CIA. Akili inayotumika kulipa kisasi Kwa hawa watu wazito wenye ulinzi wa kila Aina tena wakitumia nguvu ya jeshi la POLISI,wanajeshi na majambazi kuzima hii scandal isivuje panahitajika nguvu ya watu wengi Sana lkn jamaa anapiga kazi mwenyewe na analipa kisasi mmoja baada ya mwingine.

JAMES REECE anasimamisha nchi FBI na CIA hawalali wakimtafuta huku na yeye pia akiwatafuta wabaya wake ambao wanataka kumwangushia jumba bovu juu ya kashfa za kuliingiza jeshi kwenye biashara ya magendo, Kwa kadiri anavyotafuta ukweli ndipo idadi ya watu waliohusika wanazidi kugundulika yaani Kwa kifupi movie imebalance kwenye CRIME, MYSTERY,WAR na SPYING huku kote James Reece amafiti....
HII NI SERIES YA KIUME KWELIKWELI HUMO NDANI HAKUNA UJINGA WA MAPENZI ZAIDI YA KAZI TU

Moja kati ya series ya kijinga hakuna uhalisia na main character amepewa uwezo kuzidi theme ya movie.
 
Back
Top Bottom