sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Degree yake ya kwenye CV inayoonyesha kasomea chuo kikuu cha Chicago nchini Marekani ilizua maswali, wananchi wakatuma maombi Marekani kutaka kujiridhisha elimu ya Rais wao.
Wamarekani wapo Direct, siku ya jana Jaji wa Marekani aliamuru taarifa za uhalali wa cheti zitolewe leo na imebainika kwamba ni kweli alisoma hapo lakini alitumia cheti cha Mwanamke kutuma maombi ya kujiunga.
Ni sawa na huku kwetu mtu kafeli form 6, atumie cheti cha mtu wanaefanana jina kutuma maombi ya kujiunga chuoni.
Siku ya jana baada ya jaji wa Marekani kutoa agizo la kuweka mambo wazi, nae Rais wa Nigeria akatoa agizo la kuongeza mishahara.
Baada ya kupata ushahidi usio na shaka kwamba kakiuka kanuni za integrity (uaminifu), je kutakuwa na accountability (uwajibikaji)?
JE ATAWAJIBIKA?