Aisee naweza nikasema uko misinformed.Look my friend, hakuna kundi la kigaidi Duniani liliwahi kuwa Tishio kama Alqaeda ya Osama binLaden. Lili lilikuwa baya sana kwa kipindi kile na walikuwa hawana makazi maalum kama Hezebolah na Hamas. Umeshawaona tena? Hata kama waliswitch over kujiita Boko Haram, seleka, Alshabab etc lakini walishakatwa makali. Believe me, Hezebolah iko terminal stage ya kutoweka. Russia na Iran wanalijua hilo. Vikombora vinavyorushwa sasa ni non- tactical na misguided! The same kama ilivyokuwa kwa Hamas siku za mwisho.
Kumbuka kipigo cha Israel kwa Houth na Iran na Syria cha hivi karibuni kilikuwa mshindo mkubwa. Hivi kwa makeke yote yale ya Houths, umeshaona anarusha kombora lolote Israel siku za karibuni? Jiulize.
Usifananishe Hizbollah na Alqaeda,kwanza hiyo Alqaeda iliundwa na hao mabwana wakubwa,hivyo ilikua ni sawa na kinyago ulichokichonga hakiwezi kukutisha.
Pia Hizbollah ni kundi la washika silaha lenye WAPIGANAJI wengi kuliko kundi lolote duniani.
Hizbollah wana wapiganaji zaidi ya laki moja na nusu.
Pia Hizbollah ni political organization ndani ya Lebanon.
Sio kundi la washika silaha tu.
Wewe una uhakika gani kama mashambulizi wanayofanya Hizbollah ni misguided hayana madhara?
Una habari kama raia wa kaskazini wamehama kukimbia mashambulizi ya Hizbollah!?
Hao Houthi unaowasemea lengo lao kuu ilikua kuzuia Red sea isipite meli kuelekea Israel,je Kuna meli yeyote inayopita kuelekea Israel kupitia red sea!?
Jibu ni HAPANA.
Usiyachukulie mambo kiwepesi mkuu.
Hizbollah sio mfupa rahisi kama unavyodhani,Alqaeda ni kundi dogo sana mbele ya Hizbollah.
Hizbollah ni jeshi la Iran la pili ndani ya Lebanon,pia Hizbollah ni sehemu ya serikali ya Lebanon,sio rahisi kujimaliza kama unavyodhani.