TANZIA Thomas Mashali afariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

TANZIA Thomas Mashali afariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

Bongo ni ndogo ila mtu anaweza fanyiwa unyama bila chombo chochote cha usalama kumtetea
 
Duuuh
May his soul rest in peace,hivi hizi pombe nyumbani hazinyeki eeeh
 
Mtu awezi kuwa ndani ya Bar alafu baada ya ugomvi kidogo wakiwa humo humo ndani akasigiziwa wizi then watu from nowhere wakaja na mapanga na nondo wakamshambulia na kumuua bila ya kuuliza tatizo kwanza!

Maoni yangu: Kisa hiki kinanikumbusha stori moja ya golikipa mahili ya Ghana wa club ya Asante Kotoko naye aliuwawa kwenye mazingira ya kuatanisha - jamaa walianzisha ugomvi kwenye Bar alipokwenda kuwahamulia wakamchoma kisu akafa, baada ya uchunguzi wa kina ikaja gundulika kwamba kumbe ugomvi ule ulikuwa ni mpango mahususi wa kumuua yeye baada ya wauuaji kulipwa na Club Shindani!

Binafsi naona kisa cha Nashali akina tofauti na cha golikipa wa Ghana, kwanza waojiwe aliyo ambatana nao kwenda Bar hao naona walihusika kuhandaa watu mapema wa kumuua Mashali mambo ya kupishana kiswahili na jamaa hiyo ni gheresha tu ya kuoata kisingizio cha kumshambulia kwa mapanga na marungu - walicho tafuta pale ni kuondoa ushindani katika fani za ngumi au Mashali alikuwa kikundi cha umafia wakiwahi kudhurumiana wajatafuta njia mbadala za kulipiza kisasi - hili alikuwa tukio la jawauda hata kidogo, na,Watanzania hawawezi kumvamia mtu bila ya kuhoji ukweli wa mambo kwanza. Hayo ni maoni yangu I might be wrong.
Hichi kifo kina utatanishi lkn marehemu pia ana background mbaya

Sidhani kama huyo goli kipa wa Ghana alikuwa na background mby
 
uko bar unakunywa halafu unaitiwa mwizi hao watu walitoka wapi ndani ya muda mchache
Inabidi watu wa hiyo Bar waulizwe ukweli ndio utajulikana sidhani mteja kwenye bar hata aitiwe mwizi from no where apigwe lzm wangeuliza kwanza

Watu wa kimara jibu ndio wanayo
 
Clauds wametangaza aliitiwa mwizi baada ya kutokea ugomvi Baa Na rafiki yake.

Hivyo wananchi wenye hasira wakamshambulia Na mapanga baadae watu wa bodaboda wanaomfahamu wakamkimbiza Mhimbili ambako mauti yalimkuta.

R.I.P.
Mob Justice?Hapo Mwenye Bar Lazima Aseme Ukweli Hawa Wananchi Wenye Hasira Kali Ni Kina Nani?Lazima Kuna Ki2 Nyuma Ya Pazia,wananch Wenye Hasira Kali Wametumika Kama Chambo.Upelelezi Ndyo Utakaoufumua Yote Yaliyokuwa Nyuma Ya Pazia
 
Kuna kitu sijakielewa hapa. Yaani wamekaa Bar, akiwa na rafiki zake wakinywa, anatokea mtu wanapishana maneno, kawaida katika kupishana maneno hapo kumbuka lazima watakua wali buy attention za watu. Halafu huyo wanayepishana naye maneno anaamua kpiga kelele za mwizi, ghafla wanatokea watu wakiwa na mapanga na marungu na kuingia sehemu hiyo ya biashara na kuanza kumshambulia mteja, hapo bar hakuna wahudumu? hakuna ulinzi? wale rafiki zake walikwenda wapi?
Mwandishi makini hawezi ku report vitu vya aina hii, kama angejiuliza haya maswali niliyojiuliza mimi basi angeendelea kuutafuta ukweli au ange report kifo badala ya kutoa details zilizopoteza radha kwa wingi wa ukakasi.
Ndo mana Nape anawakomalia wawe na degree. Mana wanapost nonsenses. Haiingii akilini
 




Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali, hatunaye.
Taarifa zinaeleza ameuwawa kwa kupigwa risasi na mwili wake kuokotwa vichakani maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Yassin Abdallah maarufu kama Ustaadhi, mmoja wa viongozi wakongwe wa mchezo wa ngumi amethibitisha na kusema mwili wa Mashali upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

"Tumethibitishiwa hizo taarifa za majonzi kabisa, mwili upo Muhimbili na msiba upo kwao Tandale," alisema Ustaadhi.
CHANZO - SALEHE JEMBE BLOG
Ameuawa kwa risasi au mapanga kwa kuitiwa mwizi? Very confusing!
 
Mashali alikuwa m2 poa sana mm nilikuwa nakutana nae sana maeneo ya Meridian M'nyamala na kama humjui ilikuwa sio rahisi kuja km ni boxer hakuwa na ubabe jinsi watu wanavyoelezea
 
Hichi kifo kina utatanishi lkn marehemu pia ana background mbaya

Sidhani kama huyo goli kipa wa Ghana alikuwa na background mby

Ni kweli, mimi nilitoa mifano tu ya baadhi ya vifo tatanishi vilivyo wahi kutokea - sikusema kwamba Mensah licha ya kuwa golikipa mahili wa Ghana alijishugulisha vile vile na vikundi vya kiharifu. Lakini kwa Mashali umafiosa ndiyo inaweza kuwa ni a plausable reason behind the crime/muder kuliko masuala ya ngumi za kulipwa.
 
Mashali alikuwa m2 poa sana mm nilikuwa nakutana nae sana maeneo ya Meridian M'nyamala na kama humjui ilikuwa sio rahisi kuja km ni boxer hakuwa na ubabe jinsi watu wanavyoelezea
Mkuu hebu pitia na hizo posts zilizotangulia Kuna watu nao wanamfahamu alikua na vikundi vyake vya uporaji,wengine wamesema alikua mtemi na akilewa nilazima awe mkorofi Sasa hebu tuweke vizuri upoa wake ulikuaje kwa unavyomfahamu wewe!!!
 
Mashali alikuwa m2 poa sana mm nilikuwa nakutana nae sana maeneo ya Meridian M'nyamala na kama humjui ilikuwa sio rahisi kuja km ni boxer hakuwa na ubabe jinsi watu wanavyoelezea

MASHALI ALIKUWA MTU MBAYA.....
Mtetee tu kwa sababu ulikuwa unakutana naye hapo

PROMOTA WAKE ameiambia Clouds360 kwamba MASHALI akilewa huwa "MBABE" jana alipgiwa cm na rafk yake kwenda kimara,baada ya kufika huko wakawa wanakula MVINYO,baada ya kulewa wakaznguanana na mtu mwingn,MASHALI akamtandika[NGUMI KALI] huyo jamaa baada ya kupewa kichapo akaanza kupiga kelele za mwiz,,,Wakatokea wananchi wenye hasira na silaha wakamchakaza[bila kujua kama ni Mashali] baadhi ya watu wakasema sio mwizi huyu ni mashali raia wakamuacha lakini alikua tayar ashaumia sana na kumwaga damu nyingi...BODABODA wa hapo kimara wakamchukua na kumpeleka hospital then wakaanza kutoa taarifa kwa WANAOMJUA.
 
Back
Top Bottom