TANZIA Thomas Mashali afariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

TANZIA Thomas Mashali afariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

Nimesikiliza vizuri radio wametangaza hivi

Alikua kwenye bar moja kimara anakula masanga[emoji481][emoji481] na washikaji zake sasa pale kwenye meza akawa amepishana maneno na jamaa mmoja, ndio huyo aliyekua akijibizana nae akaita mwizi.... Na hapo ndio watu waliokua eneo hilo wakamvaa na kuanza kumpiga na mapanga, malungu mpaka bondia huyu nguli kupoteza uhai.

Ikumbukwe alitoka morogoro juzi na jana mchana alikua kwenye kongamano la mabondia na jioni alipoenda kupooza koo[emoji481] ndio mauti yakamkuta.. Pia mashali alikua anatakiwa ajiandae na pambano lake siku za karibuni.

Bwana ametoa na bwana ametwa jina lake lihimidiwe[emoji24][emoji24]
Marungu na mapanga yanafata nini BAR?
 
nimjuavyo mimi huyu mashali sema alikuwa kalewa pombe jamaa anapgana sana hata mkiwa 10 kweli pombe hatari
 
Inamaana wananchi hawamjui Mashali mpaka wamgombanie mpaka kifo!!au kitu nje ya box

Mtu awezi kuwa ndani ya Bar alafu baada ya ugomvi kidogo wakiwa humo humo ndani akasigiziwa wizi then watu from nowhere wakaja na mapanga na nondo wakamshambulia na kumuua bila ya kuuliza tatizo kwanza!

Maoni yangu: Kisa hiki kinanikumbusha stori moja ya golikipa mahili wa Ghana wa club ya Asante Kotoko naye aliuwawa kwenye mazingira ya kutatanisha - jamaa walianzisha ugomvi kwenye Bar alipokwenda kuwahamulia wakamchoma kisu akafa, baada ya uchunguzi wa kina wa Polisi ikaja gundulika kwamba kumbe ugomvi ule ulikuwa ni mpango mahususi wa kumuua yeye baada ya wauuaji kulipwa na Club Shindani!

Binafsi naona kisa cha Mashali akina tofauti na cha golikipa wa Ghana, kwanza wahojiwe aliyo ambatana nao kwenda Bar, hao naona walihusika kuhandaa watu mapema ili aje kuuliwa, haya mambo ya kusema Mashali alipishana kiswahili na jamaa hiyo ni gheresha tu za kutoa kisingizio cha kumshambulia kwa mapanga na marungu - walicho tafuta pale ni kuondoa ushindani katika fani za ngumi au Mashali alikuwa kwenye kikundi cha umafia labda katika harakati zake za mambo ya ndiyo sivyo aliwahi kudhurumiana na wenzake, hivyo kusababisha na wao kutafuta njia mbadala za kulipiza kisasi - hili alikuwa tukio la kawaida hata kidogo, Watanzania hawawezi kumvamia mtu bila ya kuhoji ukweli wa mambo kwanza. Hayo ni maoni yangu I might be wrong.
 
Clauds wametangaza aliitiwa mwizi baada ya kutokea ugomvi Baa Na rafiki yake.

Hivyo wananchi wenye hasira wakamshambulia Na mapanga baadae watu wa bodaboda wanaomfahamu wakamkimbiza Mhimbili ambako mauti yalimkuta.

R.I.P.
Mbona mleta post anasema amepigwa risasi?
 
Hii kimara hii inahitaji maombi
Yaani siku ya jana ilikuwa giza nene mara magari yanateketea kwa moto just 12km away from national fire attacking post who arraived about two hours later. Asubuhi hapo over nako kuna wawili walikata kamba wakigongwa kwa roli kwenye noah huku nako mashali kumbe wamemfupisha uhai wake.
Jaman dhambi ya hii dunia imeilemea maana inawayawaya kama machela
 
Back
Top Bottom