TANZIA Thomas Mashali afariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

TANZIA Thomas Mashali afariki dunia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

Unaongea kitu ambayo ni halisi sema kuna watu hapa Dar Hawajuo hawa matembo.

Mkuu Tembo wapo kabisa na ni halisi, wanagawana maeneo.

Mimi hawa niliwafahamu baada ya Tembo wa Ubungo kwenda kuvamia kituo kipya cha Mbezi Mwisho, kukatokea vita kali sana na wale wa Ubungo wakatimshwa, sasa baadae tena kukatokea mtafaruku wa Tembo wa pale Mbezi mwisho mpaka ikafikia kugawana stendi, mwingine alichukua stendi ya Malamba Mawili.

Mashali alikuwa ni Tembo wa Manzese, sina uhakika utawala wake ulikuwa unaishia wapi lakini jamaa alikuwa na eneo kubwa analomiliki kwa muda mrefu tu.
 
Siku hizi tumekuwa na jamii au watanzania wanaochukua sheria mkononi. Matukio ya kumshukia mtu kuwa mwizi au mchawi na kuanza kumpiga yamekuwa mengi sana. Tukio la dodoma na hili la Machale kama ni kweli yanazidi kutuogopesha jamii ya watanzania tulionao
Ukiwa mjinga hutopatwa na ttz lolote ila ukijifanya mjanja ndio utakutana na masaibu
 
Aisee, yaani watu wamemtoa mtu roho kirahisi rahisi hivo. Hata kama alikuwa analeta ubabe hakustahili kufanyiwa hivo, hao watu wa bar wakamatwe. Nakumbuka Mara ya mwisho Mashali alimdunda Cheka, r.I.p bro
 
kipigo tena? alikuwa Mwizi au wananchi kawakoses nn tena huyu jamaa?
iwe mwizi isiwe mwizi. kumpiga mtu yoyote ni kosa la kisheria. na statements kama hizi ndio husababisha watu kupioteza maisha kwani wakati wa kupiga mwizi ' kwakuwa tu mtu kasema mwizi' kinatokana na ' kuhalalisah eti wezi kuuwawa. Sipendi vitendo vya wizi lakini matokeo ya kujichukulia sheria mkononi ndio haya. Ml. Nyerere aklikwisha sema, dhambi moja ikianza basi huja na nyingine. Watu zamami walikwa wanawapiga wezi, wakahamia watyu wakifumaniwa ( mind you hao watu wote ni watu wazima), mara dreva akigonga mtu, mara sijui nini imetuvikissha hapa.

'SAY NO TO MOB JUSTICE AS IT IS INJUSTICE'
 
Tatizo la Celebrities wengi wa Tanzania hawajui kuishi kistaa..kuna vitu kama Staa hutakiwi kuvifanya,kuna sehemu hutakiwi kwenda....kuna Bar za kwenda kunywa,za watu wenye pesa zao...hata akitokea Chizi mmoja na mawivu yake akakupigia kelele basi watu watakukamata wakupeleke Polisi,Sio Unaingia Bar za Kiswahili kama hizo mapanga yako karibu,sio kila bar unaingia kunywa.

Usipojua thamani yako utaondoka hapa duniani mapema sana!!
R.I.P Thomas Mashali,nilikuwa nakukubali sana..pengo lako kubwa sana
Bar za uswahilini shida. Uptown bar mtu akileta zogo wateja wanalipa bill yake na kushurutisha management kumtimuwa. Watu na fedha Zao hawataki bugdha.
 
Nimesikiliza vizuri radio wametangaza hivi

Alikua kwenye bar moja kimara anakula masanga[emoji481][emoji481] na washikaji zake sasa pale kwenye meza akawa amepishana maneno na jamaa mmoja, ndio huyo aliyekua akijibizana nae akaita mwizi.... Na hapo ndio watu waliokua eneo hilo wakamvaa na kuanza kumpiga na mapanga, malungu mpaka bondia huyu nguli kupoteza uhai.

Ikumbukwe alitoka morogoro juzi na jana mchana alikua kwenye kongamano la mabondia na jioni alipoenda kupooza koo[emoji481] ndio mauti yakamkuta.. Pia mashali alikua anatakiwa ajiandae na pambano lake siku za karibuni.

Bwana ametoa na bwana ametwa jina lake lihimidiwe[emoji24][emoji24]
HUYO ALIYETAMKA MWIZI AKAMATWE NA KUSHTAKIWA KWA MAUAJI. ILI HAYA MAUAJI YAKOMESHWE!
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana, ni rahisi zaidi kumuhukumu asiye na hatia na kumwacha huru mkosaji
 
Bar za uswahilini shida. Uptown bar mtu akileta zogo wateja wanalipa bill yake na kushurutisha management kumtimuwa. Watu na fedha Zao hawataki bugdha.
Kabisa yaani...Hizo bar zingine Panga nje nje yaani daah![emoji22]
 
Ubondia wa kwetu sio kazi, mpaka unshtukiwa ulikuwa unafanya "extra curricula activities" ni hatarious.. Anyway Rest In Peace.
 
Dah wauaji wenyewe hata ukimuuliza ana miliki nini? utakuta hata baiskeli hana, ila kukimbilia kutoa roho ya mtu hata chanzo chake mtu hukijui..... Uswahilini kuishi sometimes ni gharama sana... Ni bora nikanywe Beer 2 za 5000 sehemu yenye usalama kuliko beer 4 za elfu 2500 sehemu za ajabu ajabu kwaajili ya usalama wangu.... Hali ni mbaya sana sana huku kwetu uswahilini.. RIP Bondia Mashali Poleni sana wafiwa. Lazima uchunguzi ufanyike na wahusika waisome namba hopeless kabisa
 
Ivi watanzania sikuizi tupoje ule upendo aliotuachia mwalimu nyerere na uzalendo mbona tumeviacha tumekua wabaya kuliko wanyama jamani tabia ya kujichukulia sheria mkononi imekithiri izi roho za wenzenu mnazotoa na damu zisizo na hatia mnazo mwaga zinageuka laana kwenye nchi hii.
Pumzika kwa amani Marshall walioshiriki kukuua laana itawatafuna wao na vizazi vyao Amen[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Mkuu Tembo wapo kabisa na ni halisi, wanagawana maeneo.

Mimi hawa niliwafahamu baada ya Tembo wa Ubungo kwenda kuvamia kituo kipya cha Mbezi Mwisho, kukatokea vita kali sana na wale wa Ubungo wakatimshwa, sasa baadae tena kukatokea mtafaruku wa Tembo wa pale Mbezi mwisho mpaka ikafikia kugawana stendi, mwingine alichukua stendi ya Malamba Mawili.

Mashali alikuwa ni Tembo wa Manzese, sina uhakika utawala wake ulikuwa unaishia wapi lakini jamaa alikuwa na eneo kubwa analomiliki kwa muda mrefu tu.


Aisee kama ma drug sellers wa kimexico kwenye series za Queen of South au Power , kila mtu anakuwa na himaya yake
 
Apumzike kwa amani. Kila kiumbe kina ukomo wa kuishi hapa duniani haijarishi utapitia njia gani.
Mimi na wewe mwanaJF hatujui siku yetu lini but will face the DEATH.
Pole nyingi kwa wafiwa.
Acha kututisha wewe, rejea Zab: 118: 17 " Sitakufa bali nitaishi nami nitayasimlia matendo ya Bwana"
 
Back
Top Bottom